Anzisha Radio kwa Tshs 10,000,000/= usikivu ni KM 45.

Radio Producer

JF-Expert Member
Feb 4, 2011
724
295
Wadau,

Offer kuuuuubwa! Tunashawishi mtu anayetaka kufanya biashara ya radio TUNDUMA kuna soko kubwa sana.

Gharama
Vifaa vya studioni Milion 3 (Vitanunuliwa katika maduka ya Tanzania)
Transmitter Watts 300 Milion 7 pamoja na Antena set.

Usajiri TCRA Tshs milion 3.

Utengenezaji studio pamoja na uaandaaji wa feseability study Tshs milion 3.

Daily Management
Unatuachia sisi tunaisimamia nawewe utakuwa ukipewa faida yako kila mwezi.

Jumla pesa yote ni Tshs 16,000,000/=

Karibu tuwasiliane
Radio Consult Company Limited

Email: consultancy@radiotz.com
 
Vipi maneo ya kusini (Mtwara, Lindi etc) kuna potential yoyote? Naangalia dynamics za gas industry.

Hii mikoa bado haijawa na radio nyingi, potential bado ni kubwa ila ukiweka lazima uwe competence kwelikweli.
 
Umesema "anzisha radio kwa shiling milion 10" lakini hesabu yako na ufafanuzi unaonyesha jumla ya shiling milion 16 zinahitajika. hadi hapo nimeanza kupoteza imani na hiyo kampuni yako ya consultancy. kuna dalili za utapeli hapa. Kuna uwezekano wa kufanya makubaliano ya bei fulani halafu baadae ukageuka kuwa hela haitoshi iongezwe nyingine. Uwe mkweli mkuu kama unataka kujenga jina la kampuni yako. Ni ushauri tu unaweza endelea vile wewe unataka.
 
Heading yako umesema 10 mill humu kwa thread unasema 16 mill

Daily management tunawaachia nyie?? Haujaweka gharama..

Minara hujaweka gharama ila unasema utajua jinsi ya kutusaidia
Sijui kwanini ila kila nikiona post yetu NAHISI HARUFU YA UTAPELI...

Samahani lakini... Anyway ngoja tuendelee kuwasikilizia
 
Mkuu Asante kwa ushauri.

Katika radio tunaaangalia vitu ambavyo vinaweza kukuletea package kamili ya transmission. Ni kwamba ukiwa na milion hiyo kumi unaweza kwenda hewani mkuu. Hakuna makadirio kila kitu ni miktaba ukisainiana mkataba namimi wa kuanzisha radio ninawezaje kuongeza bei nje ya mkataba?

Nimekuelewa asante.
 
Heading yako umesema 10 mill humu kwa thread unasema 16 mill

Daily management tunawaachia nyie?? Haujaweka gharama..

Minara hujaweka gharama ila unasema utajua jinsi ya kutusaidia
Sijui kwanini ila kila nikiona post yetu NAHISI HARUFU YA UTAPELI...

Samahani lakini... Anyway ngoja tuendelee kuwasikilizia

Mkuu mengine ni siri ya kampuni, unaona watu wanapelekana mahakamani kwasababu ya copy and paste? Siwezi mengine kukueleza hapa moja kwa moja inabidi twende kwa mazungumzo. Kama unahisi harufu ya utapeli hakuna anyekulazimisha kufanya nasi mkuu.

Samahani.
 
heading yako umesema 10 mill humu kwa thread unasema 16 mill

daily management tunawaachia nyie?? Haujaweka gharama..

Minara hujaweka gharama ila unasema utajua jinsi ya kutusaidia
sijui kwanini ila kila nikiona post yetu nahisi harufu ya utapeli...

Samahani lakini... Anyway ngoja tuendelee kuwasikilizia

mkuu nikweli 10m to 16m aaah!
 
Mkuu mengine ni siri ya kampuni, unaona watu wanapelekana mahakamani kwasababu ya copy and paste? Siwezi mengine kukueleza hapa moja kwa moja inabidi twende kwa mazungumzo. Kama unahisi harufu ya utapeli hakuna anyekulazimisha kufanya nasi mkuu.

Samahani.
Najua naweza kuwa hakuna mtu anayenilazimisha kufanya kazi na nyie basi naomba fursa hii KUWAONYA watu wanaotaka kufanya kazi na nyie wawe makini
samahani lakini....
 
Asante mkuu! Wamekuelewa na ujumbe wako umeeleweka.
 
matapeli hawa

Samahani mkuu, mimi huwa najiuliza sana, hivi inakuwaje mtu ambaye hajakufanyia kazi na humfahamu, na ametangaza yeye mwenyewe kwa ajili ya kazi zake unapata ujasiri wa kuanza kumwita tapeli? Hivi huwa mtu anapata ujasiri wapi wa kumwita mtu tapeli? Tumekutapeli nini mkuu? Tumefanyia kazi watu wangapi? Unamfahamu hata mteja wetu mmoja ambaye alikupa evidence kuwa tumemtapeli?

Wakati mwingine wabongo tujifunzeni adabu kwa watu. Si wote wako kama wewe na si wote wanafikira kama za kwako, na si wote walioJF wamo kwa lengo kama lako na nia kama yako na maneno kama yako. Kwa hali hii maendeleo ni magumu sana kwa hapa TZ sababu kila kitu kwetu sisi ni utapeli utadhani anayeuzungumza ana evidence nao, kwa mtindo huu tutabaki kuwaona Wakenya wanapeta tu na sisi wabongo tumekalia kuponda biashara za watu tukiwa nyuma ya keyboard bila kufikiria vizuri. Samahani mkuu, ila wewe ni mtu wa ajabu sana.
 
katika thread hii kila mtu ana negative review na nyinyi na ukiona kila mtu ana mashaka na wewe jua kabisa there is something kwako it is not right .....
na ukishaanza kupata negative reviews katika stage ya kwanza ya biashara kama hii biashara ambayo mtu anatumia pesa nyingi kuwekeza jua kabisa kuna tatizo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom