Anyang’anywa silaha kwa kukutwa kalala kwenye gari

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
266
MFANYABIASHARA, Pascal Matunda (50), mkazi wa Mikocheni amenyang’anywa silaha yake aliyokuwa akiimiliki kihalali, baada ya polisi kumkumata akiwa amelewa na amelala ndani ya
gari alilokuwa akiendesha katika foleni huku akiwa na silaha hiyo.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi, Suleiman Kova alisema jana kuwa mfanyabiashara huyo alisababisha foleni ya magari katika eneo la Selander baada ya kushindwa kuendelea kuendesha gari hilo.

Alisema baada ya raia kumshtukia kuwa yupo katika hali hiyo, waliwataarifu polisi ambao
walifika na kumtoa na walipompekua, walimkuta na bastola aina ya Browning namba A.
558567 ambayo imetengenezwa nchini Czechlovakia.

“Hali hii ni hatari sana kwa sababu kama watu wabaya wangempekua na kumkuta nayo, wangeifanyia uhalifu, hivyo tumemnyang’anya na hatutamrudishia tena ingawa anaimiliki kihalali, lakini inaonekana ameshindwa kuiweka kwa usalama,” alisema Kova.

Alisema kuwa katika uchunguzi wao, wamebaini wamiliki wa silaha wamekuwa wakihifadhi silaha zao sehemu ambazo si salama ikiwemo kuweka katika gari iliyoegeshwa nje, kuwakabidhi watumishi wa ndani au walinzi ambao hawana mafunzo maalum ya silaha na
wengine huziazimisha.

Alisema mwaka huu jeshi hilo limejipanga kuwadhibiti wamiliki wa silaha kihalali na kuwanyang'anya wale ambao wanashindwa kuzitunza katika sehemu salama.

Pia Kova alisema wamewakamata Awadhi Mtambo (33), mkazi wa Tandika kwa kosa la kufanya ujambazi wa kutumia silaha na kukiri kumiliki silaha aina ya Shotgun Greener yenye namba 23103 iliyokatwa kitako aliyokuwa ameificha kwenye mfereji wa maji machafu, maeneo ya barabara ya Yombo.

Katika tukio lingine askari wamekamata silaha aina ya Pistol Revolver yenye namba E. 38 S & W CTG.3 iliyotengenezwa nchini Marekani ambayo iliibiwa kwa mfanyabiashara mmoja baada ya gari lake kuvunjwa kioo cha nyuma.

Pia Kamanda Kova alisema kuwa wanawashikiliwa watuhumiwa 104 kwa makosa mbalimbali ya uhalifu ikiwemo ujambazi wa kutumia silaha, unyang’anyi na ubakaji na wengine 23 kwa makosa ya kufanya ukahaba katika maeneo ya Kijitonyama.
HabariLeo | Anyang’anywa silaha kwa kukutwa kalala kwenye gari
 
huyu alikua Geji tena nzito sijui kinyaji gani mpaka unazima barabarani
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom