Antivirus mixtape yatinga ndani ya jumba la BBA

Brooklyn

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
1,459
284
Mixtape maarufu hapa nchini inayokwenda kwa jina la AntiVirus yenye nyimbo zaidi ya nane zilizoimbwa na wasanii mbalimbali wanaojipambanua kama wapambanaji dhidi ya wizi wa kazi za wanamuziki wa kizazi kipya wanaoongozwa na mbunge mtarajiwa Mr. II aka Sugu imetinga rasmi katika jumba la Big Brother Africa (BBA).

Katika hatua isiyotarajiwa, mshiriki kutoka Tanzania Mwisho Mwampamba aliwaeleza washiriki wenzake maudhui ya albam hiyo na kina nani wamelengwa.

Alieleza pia namna ambavyo hata yeye alivyotaka kunyonywa na wadosi alipowapelekea movie yake aliyocheza akiwa Nigeria mara baada ya BBA1. Alisema alienda na master kwa mdosi na kwa mshtuko mdosi alimwambia atampa Tsh. 1 mil tu alafu haki zote za kuuza hiyo movie zinakuwa za mhindi huyo.

Aliendelea kusema, alipokwenda kwa mdosi mwingine (tanzania kuna distributors 2 tu ambao ni mtu na mdogo wake) naye alimwambia atampa kiasi hicho hicho.

In short ali support sana move ya Mr. II na wenzake ingawa alihofu na kutilia shaka kufanikiwa kwa vita hiyo kwani wasanii hawana ushirikiano.

Source: BBA All Stars
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom