ANTIBIOTICS ni dawa zinazopigana na vijidudu vidogovidogo vinavyoitwa bacteria. Zipo za aina mbili, zinazozuia bacteria asikue na kuzaliana, yaani bacteriostatic, na zile zinazoua kabisa bacteria yaani bactericidal.
Kuna aina nyingi sana za antibiotics na kila moja wapo ina aina fulani ya bacteria ambazo huwadhibiti kwa ufanisi zaidi, na nyengine hazidhuru kabisa baadhi ya bacteria.
Kuna ambazo zinadhuru ama kuua aina nyingi sana za bacteria na hizi kitaalam wanaziita broad spectrum antibiotics, mfano ni kama ceftriaxone na wenzake.
Ili kudhibiti ukomavu wa dawa wa bacteria, inashauriwa watu wasitumie dawa hizi ila kwa ushauri wa daktari, na pale ngonjwa anapopewa dawa hizi, basi ahakikishe anamaliza dose/atumie dawa kama alivyoshauriwa na wataalamu.
Hili ni somo refu sana, ila kwa kifupi nimeeleza ni nini antibiotics.
Ahsante
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.