Anthony Diallo aibuka mshindi - Uenyekiti CCM mkoa wa Mwanza

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,006
2,667
Wadau,

Muda si mrefu ndugu Anthony Mwandu Diallo ametajwa kuwa mshindi wa nafasi ya Uenyekiti CCM mkoa wa Mwanza. William Ngeleja (msimamizi wa uchaguzi) amemtangaza rasmi.

More updates to follow...

* Kuna kituko kimetokea hapa, Mbunge wa zamani wa Kwimba - Bujiku Sakila ameibiwa simu yake na wana CCM katika uchaguzi ndani ya ukumbi; anahaha kuitafuta. William Ngeleja ametangaza kuwa aliyeichukua airudishe!

Habari hii inapatikana hapa: Anthony Diallo kidedea Uenyekiti wa CCM Mwanza | Fikra Pevu
 
Wadau,

Muda si mrefu ndugu Anthony Mwandu Diallo ametajwa kuwa mshindi wa nafasi ya Uenyekiti CCM mkoa wa Mwanza. Neleja (msimamizi wa uchaguzi) amemtangaza rasmi.

More updates to follow
Neleja au Ngeleja?Nchi hii bwana,hivi kuna watu bado wana hamu na Magamba mpaka leo hiii?
 
Pamoja na ajali!!! pamoja na waliumia vibaya wapo hosptalini bado wamelazimisha kuchaguana!!! Duuuh kweli linapokuja suala la uchaguzi kwa sisimenu kama fisadi ndo anatakiwa kushinda basi ushindi lazima nyie kufeni tu na ulofa wenu!!!
 
Wadau,

Muda si mrefu ndugu Anthony Mwandu Diallo ametajwa kuwa mshindi wa nafasi ya Uenyekiti CCM mkoa wa Mwanza. Neleja (msimamizi wa uchaguzi) amemtangaza rasmi.

More updates to follow
Mkuu acha hizo ! uchaguzi wao ni kesho. Leo coaster moja iliyokuwa ikileta wajumbe toka wilayani kwa ajili ya kikao cha kesho imepata ajali nje kidogo ya Mwanza na kuna habari za kifo/vifo.
 
Mkuu wangu si unajua kama amekuwa Mkiti wa Magamba ataitumia TV yake kuisafisha Magamba huko Mwanza na kupambana na CDM?
Kamanda mimi nipo Mwanza hapa takribani wiki 2 sasa. Magamba kushinda Mwanza ni sawa na Ponda kuwa Kardinali
 
Umeona eeh..chadema semeni BYE BYE STAR TV.
Bado ITV.

Kwa diallo ninayemjua mie sidhani saaaana katika hili maana amekaa kibiashara zaidi. Hata alipokuwa waziri aliacha mikutano ya cdm inayomuingizia pesa itangazwe na kulipiwa

LAKINI

Huwa ana chuki kwa kiasi kikubwa sana. Aliwahi kumpiga BAN Lowasa katika TV yake wakati huo Lowasa akiwa PM na dialo akiwa waziri mara walipotofautiana. Hivi sasa amepiga Ban kwa Mbunge Kiwia kuonekana Star TV awe anachangia bungeni au akiwa kwenye shughuli zake mwanza. Kwa hizi chuki Binafsi huyu jamaa DIALO ni kiboko!
 
alikua anajenga mazingira iwapo angeshindwa aweka hali ya kuweza kwenda chadema.si unajua tena watu madaraka wanayatafuta kwa kila njia.

Hiyo kwenye nyekundu, thubutu mkuu! Kwani hataki biashara zake ziendelee? Maana anajua fika kuwa akihama chama tu anafilisiwa na CCM. Hukumbuki kauli ya Sumaye akiwa waziri mkuu aliposema "ukitaka biashara yako iende vizuri peperusha bendera ya CCM" unafikiri alikuwa anatania? Japo leo anajifanya mstari wa mbele kuyaona maovu ya wanaCCM wenzake, kisa anataka cheo tu.
 
Back
Top Bottom