Ansbert Ngurumo amchana Kikwete live...

Kwakweli hapo kaka umesema, tatizo hili litaendelea mpaka pale tutakapo badili mfumo wetu wa utawala kwa kuandika upya katiba yetu.
 
natumaini kikwete atakuwa amesoma hii. Na kama amesoma tu kama barua kama alivyosema yule mama mkuu wa bunge basi naomba arudie kusoma ili aelewe.

rais hatakiwi kufanya propanganda katika masuala ya uongozi wa nchi.
 
I like Ansbert Ngurumo.

His articles are well researched,written and scientifically presented. Well done Ansbert.
I know from the moment JK reads the article he shall send his UWT team to pursue on you for this article.
To JK this article is a threat to his party and government as well. We really know that ''Semina Elekezi'' is just a wastage of time and monie!!!!!!
 
Well analyzed and well put! Big up Ngurumo! Tanzania needs people like you! Tupo nawe!
 
Ansbert has said it all

Hakuna propaganda hapa. Huu ndio mtizamo wa mtu aliye makini na anayeweza kutazama mambo kwa uhalisia. Sio wale waandishi waliopewa vyeo kwa kupiga propaganda tu zisizo na mbele wala nyuma, halafu leo wamekuwa wakurugenzi wa ikulu....

Tanzania haipendi watu makini, sijui kwanini aisee
 
Sielewi kigumu kwa JK kuelewa ni nini!
Watu ambao ndio tunaonja bitterness ya maisha huku nje ya system tunamwambia kuwa waache maneno na semina zisizo na mwelekeo, wawatumikie wananchi, waache kupoteza fedha za kusimama majukwaani na kutumia spika yao NAPE kuongea njonjera zisizoeleweka!
CCM ndiyo inayoshika dola kwa sasa, kwahiyo kupoteza muda kujibishanna na akina Dr.Slaa ni kujiharibia kusikopimika!
Dr. Slaa kwa namna yoyote ccm hamumuwezi kabisa, maana watu wameshamwelewa 100%, cha kufanya kwenu sasa hivi ni vitendo tu!
Ndo nishawacheza hivyo!
wakati mwingine ninasema hakuna haja ya kutoa ushauri wowote popote kwani kama anayeshauriwa ni mjinga/mpumbavu hataweza kuulewa ushauri wako na kama anayeshauriwa ni mwerevu basi haihitaji ushauri.
 
Ansbert anaandika kishabiki sana na chuki binafsi kwa JK (amepersonalise) mambo kuhusu JK na si kama Rais (kama taasisi) hivyo anakosa objectivity kwenye makala zake

Ukisoma between the lines amesukumwa na hisia za kidini (ukatoliki) wake na chuki zake kwa Uislamu na waislamu hana lolote

Wenye akili hawajishughulishi na uandishi wake..hakuna tofauti na magazeti ya nyakati, kiongozi etc...
 
Ansbert anaandika kishabiki sana na chuki binafsi kwa JK (amepersonalise) mambo kuhusu JK na si kama Rais (kama taasisi) hivyo anakosa objectivity kwenye makala zake

Ukisoma between the lines amesukumwa na hisia za kidini (ukatoliki) wake na chuki zake kwa Uislamu na waislamu hana lolote

Wenye akili hawajishughulishi na uandishi wake..hakuna tofauti na magazeti ya nyakati, kiongozi etc...

Wanadai rais hataki kuambiwa asichotaka; nao hawako tayari kupoteza kazi zao.

Kwa mantiki hii, haiwezekani kwamba baadhi ya wasaidizi wa rais wana nafuu kuliko yeye? Kwanini tusiamini, basi, kwamba rais ndiye anawaangusha wasaidizi wake?


Jamaa atakuwa Muislam mwenzetu huyu!
 
  • Thanks
Reactions: GY
I like Ansbert Ngurumo.

His articles are well researched,written and scientifically presented. Well done Ansbert.
I know from the moment JK reads the article he shall send his UWT team to pursue on you for this article.
To JK this article is a threat to his party and government as well. We really know that ''Semina Elekezi'' is just a wastage of time and monie!!!!!!

Duh unazi huo sasa! ame research nini? unajua maana well researched article?

Article zake zimejaa hisia badala ukweli, chuki binafsi badala usahihi wa habari

Sijaona wala kujifunza chochote zaidi ya kuwa ni pandikizi la chuki kwa Tanzania mwenye mfuto na maono ya kikatoliki
 
Wasaidizi wana nafuu kuliko rais?

Ansbert Ngurumo

BAADHI yetu hatujaelewa ari, nguvu na kasi ya Rais Jakaya Kikwete. Nina hakika naye ameiimba, lakini hajaielewa barabara.

Kaulimbiu hii iliyoasisiwa na kina Samuel Sitta mwaka 2005, ilitumika kumtafutia urais mgombea wa CCM, Jakaya Kikwete, kwa ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya.

Waliomjua vema uwezo na udhaifu wake walidokeza mapema kwamba maisha ya Watanzania chini ya CCM ya Kikwete yangedorora na kuwa magumu zaidi - kwa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya.

Baadaye, sisi na baadhi ya watani wa CCM tuliifupisha kaulimbiu hiyo, tukaiita ANGUKA. Ni kweli! Miaka mitano baadaye, wameangukia pua.

CCM imeanguka. Rais Kikwete ameanguka. Mtandao wake umeanguka. Na kwa bahati mbaya, hata serikali yake imeanguka, ikaishia kuwa serikali kopa-kopa – hata mishahara ya watumishi – licha ya kodi kubwa tunazolipa.

Kuanguka huku, ndiko kumekuwa chanzo cha kura chache za mgombea urais wa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010. Kuanguka huku ndiko kumekuwa kichocheo cha vilio vya wananchi dhidi ya ufisadi. Kuanguka huku ndiko kumesababisha hata usanii mpya wa CCM wa ‘kujivua gamba.’

Kuanguka huku ndiko kumemkosanisha Rais Kikwete na maswahiba wake wa siku nyingi. Kuanguka huku ndiko kumemfanya Rais Kikwete aogope maandamano ya wananchi yanayoratibiwa na CHADEMA hata akalialia kwamba “wanataka kuniondoa kabla ya wakati.”

Kuanguka huku ndiko kumemwondoa Yusuf Makamba katika ukatibu mkuu wa CCM, yeye na sekretariati na Kamati Kuu. Kuanguka huku ndiko kumerutubisha na kukuza fitina na vita ya makundi ndani ya CCM.

Kuanguka huku ndiko kumewafanya Watanzania kuikataa CCM waziwazi kuliko wakati wote katika historia, na ndiko kumemwingiza Nape Nnauye (Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM) katika migogoro mipya ndani ya makundi ya CCM na kumwandalia anguko lake huko tunakokwenda, hasa baada ya Rais Kikwete kuondoka madarakani.

Anguko hili la ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya limewagusa wananchi wenyewe. Sasa wanakabiliwa na ukali wa maisha usiofanana kabisa na ahadi kemkemu walizopewa na CCM mwaka 2005 na 2010.

Bahati mbaya waliosababisha anguko hili, bado wanajitapa kwamba wameleta maendeleo. Vipofu!

Na kwa sababu ya upofu huu, wanakosa mikakati mipya ya kujikwamua. Wanarudiarudia yale yale yaliyoshindwa kuwanusuru miaka mitano iliyopita.

Kwa mfano, mwaka 2006 mwanzoni, Rais Kikwete aliingia na mbinu ya kutembelea wizara moja moja, kutoa maelekezo na kupiga picha na watumishi wa wizara hizo. Ilikuwa propaganda na mapambo ya magazeti na televisheni.

Baadaye, aliwaita mawaziri na watumishi waandamizi wa serikali (mara mbili) katika semina elekezi kwenye Hoteli ya kifahari, Ngurdoto, Arusha.

Leo tunapotazama nyuma, ni nani anaweza kujivunia semina elekezi za Ngurdoto?

Lakini watu wasiojifunza hawafichiki. Mwaka jana, rais yule yule akagombea kwa kaulimbiu ya ari zaidi, kasi zaidi na nguvu zaidi. Yaani, hawa jamaa hawakuridhika na ’anguko jipya’ la 2006. Waliona hilo halitoshi, wakatuandaa “kuanguka zaidi” mwaka 2010!

Haikumwongezea kura mgombea wao. Haikuvuta hisia za vijana wala kina mama. Ili kupata watu wa kuhutubia ilibidi CCM itumie pesa nyingi kuchapisha na kugawa sare, kuwagawia watu na kuwapakia kwenye magari kuwapeleka kwenye mikutano ya mbali.

Haikuwaunganisha watawala wawe na sauti moja, hata baada ya kurejea madarakani. Haikuwasaidia kupata hekima ya kumaliza matatizo ya muda mrefu, kama ukosefu wa umeme ambao umezungumzwa tena na tena bila ufumbuzi.

Sasa kwa ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi, watawala wamerudi tena katika semina elekezi, chini ya mwelekezaji yule yule.

Walidhani zile zilishindikana kwa sababu zilifanyika Arusha. Sasa wamekimbilia Dodoma. Kwa wiki nzima, serikali iko Dodoma, imelala; inakula posho. Kazi zinakwama.

Rais naye, badala ya kuwaelekeza kwa hekima na ustadi, “akawananga” wasaidizi wake hadharani, kana kwamba huwa hapati fursa ya kukutana nao – wakati amekuwa akikutana nao kila mwezi katika vikao vya Baraza la Mawaziri. Ndio hao aliowatembelea na kuwasema wizarani kwao miezi miwili iliyopita, hata akawaamuru wengine waache ubabe.

Alitaka kuonewa huruma. Alitaka kuwashitaki kwa wananchi – waonekane wabaya, awe mzuri.

Rais anawasema mawaziri wake kama watoto wadogo wanaohangaika kuelewa kitu kidogo anachowafundisha. Anawaonyesha wananchi kwamba ana mawaziri mizigo, mbumbumbu – ambao kazi pekee wanayofanya ni “kumwangusha” rais.

Anataka turudi kwenye propaganda za kijinga walizoimba miaka mitano iliyopita, kwamba rais pekee ndiye anachapa kazi, bali mawaziri wake wanamwangusha.

Anawaambia mawaziri wake kuwa kama hawawezi kazi “waondoke,” kana kwamba hajui uwezo wao, hajui waliingiaje, wakati ndiye aliyewateua na ndiye ana mamlaka ya kuwaondoa.

Anataka “watoke” waende kwa wananchi kufafanua mafanikio ya serikali yake. Haamini kwamba wananchi wana uwezo wa kuona mazuri na mabaya ya serikali – bila kusubiri taarifa za mawaziri.

Haoni kwamba serikali inayofilisika na kulazimika kukopa hata mishahara ya watumishi wake, inahitaji kubana matumizi na kupunguza ziara na posho nono za viongozi hao waandamizi.

Lakini pia, tunapowatazama watu wenyewe aliokuwa anawapa somo, tunabaki kujiuliza: Rais amepata wapi hekima hii ya kudhani ana uelewa mpana kuliko mawaziri wake?

Amesomea wapi huko wasikojua wao, alikopata hicho cha kuwafunda? Tunapowatazama baadhi yao tunagundua kwamba kama rais angekuwa na busara ya kujifunza kutokana na miaka mitano iliyopita, asingewaita mawaziri kuwafunda, bali angewaita ili wakae kama timu, awaombe ushauri, awasikilize, wampe mang’amuzi yao na mipango mkakati; naye baada ya kuwasikiliza na kuongeza maono yake, awapangie kazi na kuwadai matokeo baada ya muda kadhaa.

Au basi angeunda kikosi kazi cha wasomi waliokubuhu kutoka taasisi mbalimbali zinazoheshimika, akawakutanisha na wasaidizi wake, wote pamoja wakavuna maarifa ya ziada katika kuboresha kazi zao na kukosoa kasoro za huko nyuma.

Angejenga mazingira ya kuambizana ukweli, naye akaambiwa kasoro zake; hasa kwamba serikali imekosa mipango mkakati mbadala na hata hiyo iliyopo imekosa msimamizi makini.

Kitendo cha rais kulialia mbele ya wateule wake na wananchi kupitia vyombo vya habari si ishara ya ushupavu anaostahili kuwa nao kiongozi mkuu wa nchi.

Ndiyo! Tuliona wameinama na kushika tama alipokuwa anafoka. Lakini ana uhakika gani kwamba walikubaliana naye? Ana uhakika gani kwamba walimwona shujaa?

Na kwa kiongozi ambaye ameongoza nchi kwa miaka mitano kwa hotuba na matamko yasiyotekelezeka, anadhani mawaziri wake watamwamini na kumheshimu baada ya kufokewa hadharani Dodoma?

Labda, watamshukuru kwa kuwatengenezea mazingira ya kula posho za safari. Lakini naamini mawaziri wenyewe wanajua fika kwamba hawana sababu ya kusafiri hadi vijijini kila mara, maana huko kuna watendaji wa ngazi za chini wanaopaswa kusimamia kazi na kuleta taarifa kwa ngazi za juu.

Sasa kama rais anaagiza mawaziri waende wenyewe vijijini, hao watendaji wa mikoani, wilayani na vijijini kwenyewe watafanya kazi gani?

Hivi waziri aliyekaa katika wizara ile ile kwa miaka mitatu au zaidi, ana kitu gani cha kujifunza kwa rais aliyekaa madarakani kwa miaka mitano bila maono na mafanikio yanayoshikika?

Rais Kikwete ana mfano gani wa utendaji uliotukuka anaoweza kuutumia kuwasuta mawaziri wake? Aliacha urithi gani katika wizara alizowahi kuongoza kabla hajawa rais?

Ni nani anayejua matatizo, changamoto, na suluhisho la matatizo yake, kati ya waziri aliye kwenye wizara hiyo hiyo, na rais “anayeishi kwenye ndege?”

Baadhi yetu tunajua kwamba mkwamo mkubwa wa kiutendaji unatokana na madaraka makubwa ya rais, nidhamu ya woga ya wasaidizi wake na utovu wa uzalendo wa baadhi yao.

Zipo taarifa kwamba siku hizi wasaidizi wa rais wameamua kumwambia yale anayotaka kusikia, kwa sababu anawafokea hovyo hovyo wanapomweleza asiyotaka, au wanapompa mapendekezo magumu.

Wanadai rais hataki kuambiwa asichotaka; nao hawako tayari kupoteza kazi zao.

Kwa mantiki hii, haiwezekani kwamba baadhi ya wasaidizi wa rais wana nafuu kuliko yeye? Kwanini tusiamini, basi, kwamba rais ndiye anawaangusha wasaidizi wake?

Kwa bahati nzuri sana na mie nakufahamu ww pia kiundani Bw. Ngurumo. Ww mwenyewe familia yako ilisambaratika kwa kukosa uongozi wako, je waweza kutumbia nn juu ya hili ? uongozi hauwezi kuwa na mazuri yote , kumbuka wanaongoza ni binadamu sio malaika (ref. hotuba ya mwalimu)
 
Wanadai rais hataki kuambiwa asichotaka; nao hawako tayari kupoteza kazi zao.

Kwa mantiki hii, haiwezekani kwamba baadhi ya wasaidizi wa rais wana nafuu kuliko yeye? Kwanini tusiamini, basi, kwamba rais ndiye anawaangusha wasaidizi wake?


Jamaa atakuwa Muislam mwenzetu huyu!

Wanadai? kina nani kwa mfano?, hii inakuwa hisia ya mwandishi ambayo hakuna reference wala evidence..hisia, hisia, chuki binafsi period!

Lakini tumewapa uhuru ambao tukishamuweka mkatoliki 2015 tutamwambia auchukue na wakae kimya ok.
 
Ngurumo mie pia namkubali sana kwa msimamo usio yumba wala kubabaishwa....kama kina (M Mjengwa)
Raisi gani analia lia tuu eti hawana konidensi!, hwawajibiki! n.k sasa anatuambia sisi tufanyeje? kwani tuliwapigia kura ili wawe mawaziri!? hivi kaumbwaje huyu mheshimiwa!
Jambo hili hata watoto wa miaka minne wamemshangaa.........!!
 
well done ansbert. but alas, mbuzi hapigiwi gitaa! right message but wrong receipient! just another wasted effort. but constructive contribution to subartens who should think twice when voting for their political leaders. we stand to loose big for every wrong leaders we choose
 
Ansbert anaandika kishabiki sana na chuki binafsi kwa JK (amepersonalise) mambo kuhusu JK na si kama Rais (kama taasisi) hivyo anakosa objectivity kwenye makala zake

Ukisoma between the lines amesukumwa na hisia za kidini (ukatoliki) wake na chuki zake kwa Uislamu na waislamu hana lolote

Wenye akili hawajishughulishi na uandishi wake..hakuna tofauti na magazeti ya nyakati, kiongozi etc...


Hizi propaganda za udini zina wamaliza wenyewe,ndio maana kutwa mmekaaa pale manzese kutukana tu laaana hizo.
 
Kwa bahati nzuri sana na mie nakufahamu ww pia kiundani Bw. Ngurumo. Ww mwenyewe familia yako ilisambaratika kwa kukosa uongozi wako, je waweza kutumbia nn juu ya hili ? uongozi hauwezi kuwa na mazuri yote , kumbuka wanaongoza ni binadamu sio malaika (ref. hotuba ya mwalimu)

Huu sasa ni ujinga mwingine. Inawezekana wewe umemsoma lakini hujamwelewa Ngurumo. Alichojadili hapa hakina uhusiano na FAMILIA ya Kikwete, wala hajasema Kikwete ana wake na vimada wangapi, na katelekeza wangapi... Kama angetaka mada hiyo ingekuwa tamu zaidi, lakini ungekuwa udaku. Ngurumo hakujielekeza kwenmye udaku, yeye anazungumzia UTAWALA WA NCHI unaotegemea KODI ZETU. Familia ya Ngurumo haimtozi yeyote kodi... Sana sana anatumika yeye kwa jasho jingi, tena baada ya kulipa KODI kibao serikalini. Anchohoji hapa ni matumizi ya KODI ZETU... Familia ya Ngurumo ni private business.... Usitupeleke kwenye udaku. Hili linalojadiliwa hapa ni suala linalotumia jasho la Watz, na limepatikana kwa kura za watz. Sisi tunahoji wanavyotumia kura zetu, jasho letu na kodi yetu. Ndicho anachohoji Ngurumo hapa. Sawa?

Hata huyo Nyerere unayemnukuu, alikuwa na matatizo makubwa ya kifamilia, tena anapashwa kumshukuru sana hayati Kardinali Rugambwa. Watanzania wanapomuenzi Nyerere, si kwa kuwa alikuwa na familia bora (familia yake tunaijua vema), bali alisimamia vema kodi zao - HAKUWAIBIA. Na alikuwa na maono mapana kwa taifa lao. Jifunze kujadili hoja iliyo mbele yako...Hii ya JK na wasaidizi wake. Au na wewe ni mmojawapo?
 
Back
Top Bottom