Another short story:INGEKUWA WEWE UNGEFANYA NINI?

Che Kalizozele

JF-Expert Member
Jul 20, 2008
777
49
Bwana Juma,mkazi wa Mwanza maeneo ya mabatini mlango mmoja aliamua kwenda kwao kijijini kuoa.Alifanikiwa kupata binti mzuri wa sura na tabia na kila mtu alikuwa akikubali ya kuwa kweli bwana Juma kapata mke.Juma akachuka mke wake na kuja kuanza maisha mapya Mwanza mabatini.Bwana juma anafanya biashara za kuuza mitumba katika soko la mlango mmoja,hivyo kutokana na ukaribuni wa nyumbani kwake na sehemu yake ya kazi alikuwa anarudi nyumbani saa za mchana kupata chakula cha mchana wenyewe wanaita lunch.
Wenyewe wanasema mjini mjini tu bwana,mkewe bwana juma akaanza kuzoea mji wa Mwanza na mwishowe akajikuta amedondokea katika penzi zito la kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la John.Kumbe mkewe bwana Juma ambae kwa jina alijulikana kama Regina,alikuwa amelazimishwa na wazazi wake aolewe na bwana juma lakini mwenyewe alikuwa hampendi.na alikubali kwa sababu aliogopa radhi za wazazi wake.Sasa mwenyewe alikuwa anasema amempata mtu ambaye nafsi imemkubali na kumpenda kwa dhati.Penzi lilipokolea John na regina wakaamua kufanya taratibu za kuishi pamoja.Pamoja na haya aliyokuwa anayafanya lakini Regina bado alikuwa hajasahau kuwa anatakiwa kuwa na muonekano mzuri katika jamii,hivyo alikataa katakata kuishi na John bila ya kufunga ndoa.Kuona hivyo John akamwambia basi tufunge ndoa.Tatizo likaja Regina ni mke wa mtu,John akamwambia amfanyie vituko mumewe mpaka ampe talaka.Walichokuwa wamesahau ni kuwa pamoja na bwana juma kuwa na jina la kiislam lakini yeye ni mkatoriki safi,na kwa wakristo kinachounganishwa na Mungu mwanadamu hawezi kukitenganisha.Licha ya hayo,bwana juma anampenda sana mkewe na Regina analijua hilo hivyo suala la kwamba bwana juma atatoa talaka si rahisi kiasi hicho.Baada ya majadiliano ya muda mrefu,Regina na John wakakubaliana watafute jinsi ya kumuua bwana Juma ili asije kuwa kikwazo pindi watakapotaka kufunga ndoa.
Katika kupeana majukukmu katka harakati zao za kufanikisha azima yao,John alitakiwa kutafuta sumu ambayo Regina atamuekea bwana Juma katika chakula.Kwa maelezo ya john,sumu hiyo atakayoleta itakuwa ni vigumu watu kujua kwamba ni Regina ndio muhusika mkuu wa kifo cha bwana juma,Regina akaridhika.
Kama unavyowajua akina dada,hawawezi kukaa sehemu wakakosa kuwa na mashoga,basi siku moja Regina alikuwa ametembelewa na rafiki zake.Basi wakatia stori kwa sana tuu,baada ya muda akatoka kuwasindikiza wageni wake.Akiamini kwamba hatochelewa,hakuona umuhimu wa kufnga mlango.
Hapo Mabatini mlango mmoja palikuwa na kijana mmoja akijulikana kwa jina la Khamisi.Huyu bwana alikuwa mwizi maarufu wa redio.Wapo waliokuwa wanaamini kwamba bwana Khamisi anatumia dawa katika shughuli zake hizi za wizi wa redio.Huyu jamaa utafikiri uwa ananusa,kwani hata ukinunua redio leo,basi jioni atakuwa na data zote,ina ukubwa gani na ya aina ganiNafikiri unakumbuka kipindi kile redia za cd zimeanza kuingia,ilikuwa kuwa nayo ni ujiko mtaani.Bwana Juma alikuwa nayo moja.Muheshimiwa Khamisi alikuwa ameshaipigia misele,lakini wapi bwana kila siku kulikuwa na mtu na mazingira yalikuwa hatarishi kwa maisha yake kama angejaribu kufanya jaribio la kuiba redio ya bwana Juma.
Sasa wakati Regina anatoka kwenda kuwasindikiza rafiki zake Khamisi alikuwa anauona mchezo mzima na kitendo cha Regina kuacha mlango bila ya kutia kufuli,bwana Khamisi akajua ile siku aliyokuwa akisubiria kwa hamu ndio hii imefika.Ile Regina anakata kona tuu,Khamisi akaangalia kushoto na kulia na kuchoma ndani.Bila ya ajizi,moja kwa moja hadi chumbani,akanyanyua redio na bila ya kuchelewa akaanza safari ya kutoka nje.Ile anafungua mlango tu,anamuona Regina yule anakuja,akajua lilishaharibika.haraka haraka akarudsha redio chumbani na yeye kuingia chini ya uvungu wa kitanda huku akiamini nafasi itatokea ya yeye kutoka humo ndani salama.Muda si muda John akaingia,akiwa na sumu mkononi,hao moja kwa moja hadi chumbani bila ya kujua kwamba bwana Khamisi yuko chini ya uvngu wa kitanda.Katika majadiliano yao wakakubaliana kwamba,Regina amuwekee mumewe sumi ile aliyokuja nayo bwana John katika chakula cha mchana ili baada ya msiba nao wapate muda wa kujiandaa na harusi yao.Baada ya mabusu ya hapa na pale,John huyo akaaga.Kule chini ya uvungu khamisi likaanza kumkaba kifuani huku akihisi ana maisha ya mtu mkononi mwake,akaweka nia ya kutokuondoka mpaka auone mwisho wa picha hii.Mchana ukafika,chakula kikaandaliwa tena vizuri sana kuzidi siku zingine zote na bwana juma nae akafika.
Akakaribishwa chakula,nae bila ajizi wa la kwekwere akajongea mezani na maji akaanza kunawa.kule uvunguni,khamisi anasikia kila kitu,kwani bwana juma alikuwa ana chumba na sebule tuu.Aliposikia ananawa,khamisi mapigo ya moyo yakaanza kumwenda mbio,aliposikia anavuta sahani ya ugalli,akajikuta bila hata ya kujielewa sauti inamtoka:

Khamisi; Bwana jumaa eeeeeee

Juma kwa kutokujua na kuchanganyikiwa na wapi hasa sauti ile inatokea,hakuitikia mwito ule.Alipoona kimya,khamisi akaaita tena.

Khamisi;Wee juma weee

Juma;Naaam

Khamisi;usile hicho chakula kina sumu

Juma;Kwani we nani

Khamisi;nisubiri nakuja.

Bwana Khamisi akatoka kule uvunguni na kuelekea kule sebuleni.Akaanza kwa kumuhakikishia ya kuwa chakula kile kina sumu ingawa Regina alipinga vikali.Na ndipo bwana khamisi akaanza kuelezea ilikuwaje akaaingia mule ndani na alikuwa anafuata nini na kwa nini alikuwa na uhakika chakula kile kina sumu.

Khamisi;Kama unabisha mwambie huyo mkeo akile hicho chakula,uone kama atakubali.

Bwana juma alipojaribu kumlazimisha mkewe ale chakula kile japo kidgo alikataa katakata,hapo bwana juma akaanza kuamini inawezekana kweli cha kula kile kina sumu.Kujiridhisha zaidi,akamwita paka wake na kumtupia kipande cha nyama,kweli baada ya muda wa dakika kadhaa paka yule akaanza kugalagala huku povu jeupe likimtoka mdomoni.Hapo bwana juma akawa na uhakika kweli chakula kile kina sumu.Sasa naomba uchukue nafasi ya bwana juma,ungekuwa wewe ungechukua maamuzi gani kwa mkeo na yule mwizi wa redio.
 
Wote wawili Mke na bwana Khamisi ningewasamehe, kuepuka kifo ni jambo kubwa kuliko mengineyo, lakini roho ingeniuma kusababisha kifo cha paka. Halafu ningewapeleka Hoteli ya La Kairo tukaondoe njaa kwa Sato na Ugali wa Udaga.
 
Bwana hamisi angesamehewa...na mke angetafutiwa usafiri wa haraka kuelekea kwao.akaue na wengine.hata kama ningekuwa na upendo gani jaribio la kuniua....latosha.
 
Back
Top Bottom