Another Joke from Kikwete: Every student to have computer in five years time

Mi wajameni huyu mkulu siku hizi simuelewi kabisaaaa, ananiboa mbaya na haya maahadi yake ambayo sijui anapotoa anafikiri kuwa anaongea na watoto au majingajinga hivi, real sielewi kabisa hao washauri wake wanafanya kazi gani, lakini labda hashauriki.Kila kitu kwake ndoto ndoto ndotooooo.
 
Sehemu kubwa ya hotuba hiyo iliandaliwa na Shekh Yahya! Inawezekana kila shule kuwa na computer lab na sio kila mwanafunzi kuwa na komputa yake. Je, laptop, ipad au desktop? Umeme gani utatumika? Solar? Hajadandia kweli habari za One Laptop per Child project?

Hujakosea, watoto watatumia dustproof floortop. Madawati hakuna zitakaa kwenye udongo
 
WE STILL HAVE A VERY VERY VERY LONG WAY TO HAVE good and visionary LEADERSHIP
 
Shule ambazo

1: Hazina Vyoo
2: Hazina Maabara
3: Hazina Vitabu ( Nasikia Pesa ya MMEM haijaenda Mashuleni Bado kwa Mwaka huu)
4: Hazina Walimu wa kutosha na waliotaalumika vizuri
5: Hazina Umeme
6: Hazina Madawati

Halafa ghalfa bin Vuu Kila Mwanafunzi atakuwa anabofya Key board yake Mwenyewe? Tutakuwa ni Taifa lilioendelea Kuliko Hata Marekani
 
hivi huyu jamaa anafikiri sisi bado tumelala, ahadi za nini wakati huwezi kuzitimiza, we kama mchapakazi toka lini ukaenda kwa bosi wako et oh mimi nafanya kazi hii kesho nitafanya hivi, hata bosi wako ataona una walakini fulani, so the guy is trying rip his shoulders whilst been broken already, we dont want all those craps--anaongea kompyuta wakati madawati yenyewe hakuna vyumba vya kusomea hakuna, walimu wa kufundisha hizo kompyuta hakuna, walimu kila siku hawalipwi mishahara yao---

Mr President might not be serious, kuna ishu kibao ziko on the table with pending solutions halafu anakuja na computer--lol!!
 
Hivi mtu anavyotoa ahadi kama hizo huwa hata amefikiria? Hizo computer katika kila shule ya sekondari na kwa kila mwanafunzi, zitatumia umeme wa mafuta ya taa

narudia tena kusema, nnchi hii inabahati mbaya kuwa imepata Rais mwepesi kimantiki, mzito kufikiri wakati anaongea, anaongea huku akili ikiwa iko likizo.
kwakweli huyu ni kiongozi asieweza hata kusimamia maneno yake, hakika mi nimeishiwa maneno.
 
Ok JF members, read the attachment what do you think about that, if it will be so our country will be better in the future to come!
 
Ok JF members, read the attachment what do you think about that, if it will be so our country will be better in the future to come!

Wameshindwa kununua madawati tu ili wanafunzi wakalie ndo waweze mambo makubwa hayo thubutu.
 
Aache bla bla zake. Hata huo umeme, vitabu, walimu, madawati nk ni tatizo kwa shule zetu leo JK anaongelea computers ili nani awafundishe hao wanafunzi hizo computer? Kampeni jamani zitatufikisha pabaya na wananchi watadanganywa wakubaliane na propaganda fake za CCM
 
Hii ya leo Kali, eti katoa milioni kadhaa ili kukamilisha pesa iliyokuwa imebakia kwa wanakijiji kukamilisha ujenzi wa kitu fulani.....huko huko aliko kwenda ziarani...hivi wachaga ni wepesi kumbe wakudangaywa...heheheeee....sikujua kumbe mkwere na mchaga, mjanja ( muongo) ni mkwere....
 
Mie nadhani mkulu kuna jambo limemwelemea akilini kiasi cha kuwa anaongea bila kufikiri. Anahitaji kusaidiwa au aamue tuu yeye mwenyewe kupumzika na sisi tutampa pension mpaka atakapoondoka duniani. Sio lazima uraisi ufanye miaka 10
 
Mtazamo wangu

Maneno haya ya JK yamenifanya nikubali maneno ya wahenga, " akili ni nywele kila mtu ana zake." Hivi Rais anapozungumzia kila mwanafunzi kuwa na kompyuta ndani ya miaka mitano, wakati vijiji vingi vya Tanzania havina umeme anamdanganya nani ?

Pia watoto wengi hawana madawati yeye anazungumzia kompyuta? Hata kama ukimpatia kila mwanafunzi kompyuta wakati walimu hawapo na mitaala ni ya mwaka 1967 itasaidia nini ? Nadhani JK hajui extent ya matatizo ya watanzania , na ndio maana anatafuta short term solutions for long term problems.

Kweli nchi ikiwa na Rais of the likes of JK, basi haihitaji adui.
 
Wadau, mmeamini kale ka-thread sasa nilikowatumia kuwa Kiranja mkuu ni Mtata
Nashangaa kwa nini anawatania na kuwadanganya Wachaga wa watu hivi.....kwani Mkwele na Mchaga ni watani....hebu apunguze utani wake huyu jamaa, ajifunze kutofautisha, kifo na usingizi.

sasa nakumbuka vyema hadithi ya Shabani Robert ya NCHI YA KUSADIKIKA....MUNGU amlaze pepa peponi kwani huyu mzee hakika alioona mbali sana...hii ndio nchi yenyewe ya kusadikika
 
pumba zake ataongea huko huko kwa hao wanaoitwa wana ccm wenzake hawezi kuzungumza pumba kama hizi mbele ya watu wenye akili zao.


mambo ya uchaguzi hayo jitu linaropoka tu hata kutumia akili aliopewa na Mungu hataki,wape madawati kwanza wewe acha utani watoto wanapinda migongo kwa kukaa chini.
 
"...Investors from the US had agreed to help in the distribution of the gadgets and technology, the President said..." ...He said the government was aware of the problem of the inadequate number of laboratories in most of the secondary schools and that it was working with the African Development Bank (AfDB) to build the science facilities and install modern equipment in every secondary school.
On the problem of teachers, he said:..."

Rais amesema na itakuwa! But then if only he had referred solving the problem using our own sources would I have inclined to start believing in him! If the donors are already withdrawing from supporting the budget, how else will they come from the backdoor to support the un-workable computer-for -all kids project? Maskini
 
Huyu jk anafanya kazi ambayo siyo yake, mimi namshauri angeingia kwenye ze comedy search angeshinda hata mimi ningempigia kura kwenye ze comedy search
 
nasema mmemnukuu vibaya,kwanza hawezi kusema hivyo.nakama amesema hivyo alikuwa usingizini.na kama alikuw usingizini wa kulaumiwa ni mwandishi wa habari. kwa sbabu najua ni lazima ameisomea kazi yake nahivyo kujua tofauti ya ndoto na habari ya kweli.kwanza alienda kufanya nini kwa rais wakati alikuwa amelala?theguardian naomba hiyo mwandishi afukuzwe kazi mara moja kwa sababu atakuja siku atuambie kasema kila mwanafunzi atapata bajaji ya kwenda shule.ingawa sina imani na rais siamini kama kafika huko ila wana jf tuunde tume ya kuchunguza kama ni kweli nashauri apelekwe h.......li ya m........e
 
Back
Top Bottom