Anne Makinda: Sitogombea tena ubunge 2015

..ina maana hakuchukua nyumba wakati wa mgao wa Magufuli?

..hata asipogombea ubunge bado anaweza kugombea nafasi ya Spika wa Bunge.
 
Madam Speaker, wacha hizo! Nadhani umechuma vya kutosha kule Mjengoni! Mama, usile na kipofu ukamshika mkono!
 
Mh. Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano amesema kuwa hato gombea ubunge chaguzi mkuu ujao. Amesema anataka kukopa pesa arudi kujenga nyumba.

Sorce: ITV, HABARI YA SAA MBILI


Ngoja tuone muda ukifika.
 
Kwanini huyu mama anataka kupindisha ukweli? Eti ametumikia watu wake wa Njombe kwa miaka 17! Lakini najua amekaa mjengoni ktk vipindi nane (8) mfululizo kwa miaka mitano mitano! Ukweli uko wapi wakuu?
 
Kwanini huyu mama anataka kupindisha ukweli? Eti ametumikia watu wake wa Njombe kwa miaka 17! Lakini najua amekaa mjengoni ktk vipindi nane (8) mfululizo kwa miaka mitano mitano! Ukweli uko wapi wakuu?

Vipindi vingine alikuwa anaingia kupitia vijana...sio jimbo!!kwa jimbo ndio miaka 17
 
Si unajua spika si lazima awe mbunge,labda ana uhakika wa kugombea tena uspika japo hatakuwa mbunge.
 
anastaafu ubunge then anaenda kukopa atalipa na masaburi yake? Mbona anatufanya hatuna akili? Hili gorofa analojenga hapa kijitonyama mpaka anafunga njia alikopa wp? Mungu yupo upande wa wananchi maskini wa Iringa anaowaacha bila hata panado, inauma sana niliwaangalia jana kupitia ITV na nyuso zao za kukata tamaa mama kawakazia uso eti anaenda kukopa ajenge jamani jamani, eeh Mungu unajua kuingia kwetu na kutoka kwetu, yakumbuke maombi yetu ya kuwaombea viongozi wetu na udhalimu wanaotufanyia utujibu upesi.
 
Nikiwa primary sch. miaka ya 1980, huyu mama tayari alishakuwa mbunge! Leo hii eti akakope pesa ya kujengea nyumba! Alikuwa wapi muda wote? Na hizo fedha za ubunge alikuwa anapeleka wapi?
Kuhonga ili apate ubunge kipindi kijacho na kadri unavyotoa hongo ndivyo unabakia kuwa mbunge wa ccm. na ndo maana si yeye tu hata mibunge mingene ya ccm sasa hivi imechoka sana kipesa ndo maana wanalilia sana posho! Pesa zote wanazozipata zinaishia kulipa madeni waliokopa ili kutoa rushwa wachaguliwe! hii kweli ni biashara kichaa ya wabunge wa ccm. Kwa mbunge aliyekwenda kwa kuchaguliwa na wananchi kwa mapenzi yao hana haja ya kufilkisika kiasi hicho kwani hatakuwa ametumia pesa kuhonga watu zaidi ya ile pesa ya kununua mafuta tu ya gari labda lakini hawa watu wanatumia pesa nyingi sana kuhonga watu kanga vitenge kofia na pia kuwapa keshi.

CCM msiba wa taifa
 
KAMA VIONGOZI WETO WOTE WAMEAMUA KWA DHATI KUSALITI 'HAKI YA KUISHI NA USALAMA WA MALI ZETU' KIASI HIKI SASA SERIKALI YENYEWE INAKUA NA MAANA KWA VIONGOZI WENYEWE AU SISI WANANCHI WALIPA KODI???????

Kijana umeongea kwa uchungu wa hali ya juu sana na yote ulioyataja humu ni ROBO TU ya jinsi gani tunavyowaona zaidi ya asilimia 98 % ya mbegu ya viongozi tulionao hivi sasa katika nchi yetu.

Mpaka hapa hakika mjue ya kwamba pindi mnapoendelea hata kwa robo hatua kwa kutuambia eti mchote tena kodi zetu ziwe posho zaidi kwenu, eti maisha Tanzania hii sasa ni magumu tu kwa hawa viongozi wanaofilisi taifa letu ...,

... nasema tunapoendelea kusikia eti hata MAFISADI waliokubuhu nao bado wanaendelea kuonekana wakirandaranda mitaani kutaka wakatuongoze tena badala ya kujivua gamba ...,

... kwa uhakika pindi vijana wa taifa hili tunapoendelea kushuhudia eti wengine wakiagiza polisi watuue raia na kutubandika nembo za WAHUNI pindi tunapoandamana kudai HAKI YA KI-KATIBA NA JUKUMU NAMBA MOJA YA serikali kutulinda na mali zetu ...

Mpaka hapo wenzetu ni kama vile akili zinataka kuturuka vile, ni kama vile wengine tunatamani kwenda kuondoa kabisa uozo wa aina hii kwa mikono yetu bila kuendelea kuhesabu vifo zaidi nchini; mkoa baada ya mkoa. Rai Kikwete kwa uhakika, kachukuwe hatua za dharura KUKOMESHA hii hulka mpya ya DOLA kuwaua raia kinyama kiasi hiki.

Mpaka hapa ni kwamba tungependa ieleweke kwamba HATUTOPENDEZEWA kuona vifo zaidi ya raia hata mmoja wakati kodi zetu polisi na jeshi letu wakiendelea kulipwa kila mwezi.

Nasema kwamba wala haitusaidii kitu kuendelea kuwa na viongozi sanamu sawa na picha tu ukutani kwa jina la Vuai Nahodha, Saed Mwema, Mkuu wa Mkoa, Wilaya na RPC huko Ruvuma wakati raia tukiendelea kuchinjwa na waajiriwa wetu wenyewe kwa mtaji wa kodi zetu!!

a.
Wanaharakati mko wapi au mnasubiri tu kuja kuandika mi-ripoti ndefu mara baada ya familia kadhaa nchini kupoteza zaidi y nusu ya ukoo wao?

b.
UDASA huu ukimya wenu tafsiri yake ni kujiunga na mdhulumishi au tuwaelewe vipi?

c.
Tangnyika Law Society ndio tuseme mpaka O'Campo awe ametoa neno ndio mtiririko wote huu wa mauaji katika mkoa mmoja baada ya nyingine ipate kuwagusa?

d.
Akina Mama kwenye taasisi zenu zote kama vile UWT inamaana uchungu wa mtoto wa mke mwenzio wala haukuhusu kitu isipokua ni jukumu la Mama Nkya na Kijo Bisimba peke yao sio?

e.
Enyi wanafunzi wa vyo vikuu nchini mliopata kua VIWAKILISHI VYA SAUTI YA HAKI KATIKA JAMII, mnaona ni vema hadi afe mtu wa ngapi tangu Mauaji ya raia Mwembechai, Pemba, Arusha, Igunga, Musoma, Uyole-Mbeya, na sasa Songea, ndio mpate hata kuguna tu juu ya mwenendo wote huu wa mambo?

f.
Kamisheni na taasisi zote za haki za binadamu nchini, inamaana hata kukemea tu muaji haya yote ni mpaka kupatikane mfadhili kutoka nje ya nchi ndio akawape fedha ndio mpate kutekeleza majukumu yenu?

g.
Vyombo vya maamuzi ya Juu nchini kama vile NEC-CHADEMA, NEC-CCM, Baraza la Mawaziri na Taasisi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivi kweli vikao vya dharura mtaweza kuviitisha tu pindi mambo ya kisiasa yanapowaendeeni vibaya kwa njia moja au nyingine na wala si kule KUTOLEWA ROHO Mtanzania mwenzetu??

h. Hivi kweli Tanzania tumefika mahala ambapo uhai wa raia ni sawa tu na uhai wa inzi na wala halichukuliwi kwa uzito wake kama ambavyo tumewahi kusikia enzi hizo Mzee Mwinyi alipokua Waziri wa Mambo ya Ndani?

i.
Wazee wetu tunaowaheshimu saaana katika taifa hili; Joseph Sinde Warioba, Salim Ahmed Salim, Benjamin Mkapa, Edwin Mtei, Bob Makani, Mufti Mkuu Sheikh Simba, Mwashamu Askofu Polycarp Pengo, Jenerali Ulimwengu, Rejnald Mengi, Mzee Bahresa ...

... je ukimya wenu wote huu wakati Dola ikiendelea kuua mkoa hadi mkoa ndio tuseme ni usaliti au usahihi wa msimamo wenu kutetea jukumu mama kikatiba kulinda uhai wa kila Mtanzania na mali zake au mpaka vurugu zije zitukumbe ndio mje kuanza kukatisha kushoto kulia.

Kamati ya kutumu ya Bunge kuhusu ulinzi na usalama, tunaomba maelezo kuhusu mauaji yote haya huku Rais Kikwete yeye akiendelea tu na safari zake za huko na kule kama vile hakuna cha ajabu kinachotokea ndani ya nchi yetu.

Kwa kweli kwa jinsi mambo yanavyoeneda hivi sasa na kwa usahihi ambao huyu Ndugu KweleaKwelea wa JF ameweza kubainisha kero za ndani kabisa wa kila kijana ndani ya nchi hii, napenda kusema kwamba NAUNGA MKONO karipio kali kwenye hotuba ya Mhe Dr Slaa, alioitoa hapo jana jijini Dar es Salaam, neno kwa neno na nukta kwa nukta bila ajizi!!


Well, simlaumu sana mama yetu lakini anawakilisha mawazo ya kizazi kilichopita chenye uvivu wa kujituma na kumtumikia kafiri bora mkono uende kinywani....

Ni kizazi ambacho hakina matumizi makubwa ya kichwa.... hakiwezi hata kuset priorities za taifa..... ni kizazi cha hunters and gatherers...... hakijafikia hata stage kuitwa horticultural societies.........

1. Kizazi hiki huona bora kiue kiwanda cha kiatu ili kinunue viatu vya ulaya.....
2. kizazi hiki huona bora kiue ginerry na vyama vya ushirika ili products zikawe processed ulaya.....

3. Kizazi hiki hudhani kuwa kutembelea 4 wd za gharama kutainua uchumi kuliko kujenga barabara bora....
4. Kizazi hiki hupenda kwenda kupumzika ulaya na si kuendeleza mambo mazuri ili kipimzikie nyumbani....

5. Kizazi hiki hupenda sana dili za muda mfupi mfupi hata kama zina gharama kwa taifa...
6. Kizazi hiki hakioni umuhimu wa huduma ya reli kuwa bora na umuhimu wa huduma hii kuwa chini ya state.....

7. Kizazi hiki ni hopeless.... ni hopeless kuliko kile cha chifu mwangunga kwani kimeenda shule lakini mambo yao kama kinavuta bangi mbichi......

NOTE: it is high time tulijipanga kwenye forum zetu kuwa tupigane mshahara wa mbunge uwe as high as the university professor....ili ONLY COMMITED PEOPLE TO GET IN PALE MJENGONI.........

Kwa heshima na taadhima NINAWAOMBA WABUNGE WOTE WAZEE WAFUNGASHE NA WAIGE MFANO WA MAMA MAKINDA (ambaye kwa kauli hii nimemuheshimu sana)....

Pia nawaomba wale wabunge vijana wanaofikiri kwa kutumia masaburi pia waunge bogi.....
lets leave the brilliant DOT COMs produce the new cadre to save our sunking Tanzania....
such that hakutakuwa na KULOGANA tena kwa ajili ya hii position......

kiasi kwamba B**** letu limekuwa kambi la wachawi.....

mAMA YETU KASOMA ALAMA ZA NYAKATI...she is brilliant!

Mungu mbariki Makinda...

Mungu ibariki Tanzania...
 
vichwa vya magazeti ya mwez flan 2010 yalisema: spika makinda afunga barabara inayopita karibu na nyumba yake mwenge dsm, wengne,mwenyekti wa mtaa mwenge amuumbua makinda kwa kufunga barabara, ...manispaa ya kinondoni yamruka makinda kwa kufunga barabara ipitayo kwenye nyumba yake maeneo ya mwenge...wananchi watahabika kwa kuzunguka uzio wa nyumba ya spika,badala ya kutumia dakika5 sasa kuzunguka dak30...mwishon wakasema..hatimaye wananchi wamzidi kete makinda,abomoa uzio wenye utata...TAFAKARI,
 
Jf funguka kwa upana kingereza wanasema read between lines. Ana maanisha tutegemee appartments zenye majina kama makinda tower, semamba tower anna makinda tower, ama majina ya wanawe hela aliyopewa na rostam bilion moja cha mtoto kumbuka amepindisha mengi zao lake ni ufisadi

Hapo ninakubali Bubu Msemaovyo, hiyo zuga ya kukopa pesa (atakopa wapi hata hivyo?) ni sape goat ya kufanya money laundering. Najua there is no any financial institution that’ll guarantee loan recovering if extended to her: she is in an advanced age, she can not live beyond other 25yrs - come what may!

Zaidi ya yote si tu kasoma alama za nyakati ila akina Lema, Zitto na Lissu wamechangia kumyima raha ya uspika na ubunge - naona kila akilala anawaota ndotoni, she can not face their music again, it needs someone speedy and energetic to dance their music.

Ila kanichefua kwa kusema ubunge ni umaskini, yale yale ya kusema posho zimepanda kwa sababu maisha ya Dodoma yamepanda pale Dodoma! Kwa wabunge tu? Kama ubunge ni umaskini mbona kuna maprofesa wameacha taaluma zao na kukimbilia mjengoni?

Hata hivyo kapima kima cha maji, kaangalia perfomance yake toka enzi yake ya unaibu spika mpaka uspika kamili, kaangalia graph ya umaarufu wake na kuona inadondoka saaana akaamua kutamka hayo alotamka. Ameona jinsi CCM inavyopoteza mvuto kwa wanachi naye akiwa part of killing process, akaona ajikoshe.
 
Naona wengi mnakosa point anayo iongea makinda.
Kasema hata gombea tena ubunge,............Kauli kama hii alisha itoa Sitta pia.

Wote hawa wana maanisha kwamba watakuwa kwenye mchakato na mchanyato
wa kuingia Ikulu,.......
..subirini watakavyo kwaruzana huko............

WHAAAAAAT????? Say that again, this old mamma seeking to become Commander in Chief of the armed forces? Dear LORD save us from another malicious presidential term starting 2015.
 
Back
Top Bottom