Anne makinda amdhalilisha Sitta

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,034
28,201
Hivi karibuni spika wa zamani mzee sitta alitoa tuhuma nzito na kumhusisha spika makinda na mafisadi.kitendo cha spika anne makinda kuamua kukaa kimya dhidi ya shutuma hizo kutoka kwa mtangulizi wake, kimeonyesha ukomavu wa kisiasa wa mama huyu.yawezekana mama huyu akajibu tuhuma hizo hapo baadae lakini atafanya hivyo bila jazba wala kukurupuka kama alivyofanya sitta.nimewahi kutoa thread hapa jamvini na kumuonya sitta kwamba kubwatuka,kulalamika na kulaumu sio kazi yake kama kiongozi,anahitaji kuchukua hatua
 
Unajuaje, labda hana la kujibu kwa vile tuhuma hizo huenda zina ukweli.

jibu la kwanza kwa mtuhumiwa yoyote duniani ni kukana tuhuma ziwe za kweli au za uongo.makinda analo jibu lakini kaamua kumdharau sitta na kumuona ni kama wapiga kelele wa mtaani.
 
sitta unahitajika kuhama chama achana na mapambano feki !
 
walewale tu, sina la kuongeza, kama keli amegundua nyumba inaungua si atoke analialia nini mara kubenea mara dowans mara.....
... ahh.... mi nimechoka.... ni mtazamo wangu lakini....
kweli eenh?
 
Kuhusu makinda kuwekwa uspika na mafisadi, alishakiri mwenyewe kwamba RA alimshawishi. Ndiyo maana hana la kumjibu mzee 6
 
CCM wanajuana wenyewe!! Cha msingi ni wapiganaji wetu kuwa makini, tusiwape mwanya wa kutufanya wanavyotaka.
 
Hivi karibuni spika wa zamani mzee sitta alitoa tuhuma nzito na kumhusisha spika makinda na mafisadi.kitendo cha spika anne makinda kuamua kukaa kimya dhidi ya shutuma hizo kutoka kwa mtangulizi wake, kimeonyesha ukomavu wa kisiasa wa mama huyu.yawezekana mama huyu akajibu tuhuma hizo hapo baadae lakini atafanya hivyo bila jazba wala kukurupuka kama alivyofanya sitta.nimewahi kutoa thread hapa jamvini na kumuonya sitta kwamba kubwatuka,kulalamika na kulaumu sio kazi yake kama kiongozi,anahitaji kuchukua hatua

Unajuaje ni kawaida yake kukaa kimya hata kwenye mambo ya msingi? Si unakumbuka hata masaburi aliwaambia wabunge wanatumia 'nanihii' kufikiria na wala hakuna aliyejitokeza walau kukanusha tu leave aone kumtaka approve!
 
Asingeweza kumthibiti masaburi kwasababu moja kubwa; kundi la mafisadi wakina Rostam na Lowassa waliompa uspika ndio hilo hilo la masaburi na makongoro mahanga!! WHOEVER PAYS THE PIPER CALLS THE TUNE!!.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom