Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
VITA vya kuwania ubunge Jimbo la Same Mashariki vimechukua sura mpya baada ya mbunge wa jimbo hilo, Anne Kilango-Malecela kudai mpinzani wake anataka kumaliza maisha yake na uzao wake.
Kilango amekimbilia makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutaka kiinglie katika vita hivyo.
Tayari Kilango amemshitaki Dk. Michael Kadeghe, aliyejitokeza kuchukua jimbo hilo, kwa Katibu Mkuu Yusuf Makamba.
Anadai mwalimu huyo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam anaandaa mazingira ya kutaka kumfunga.
Mpaka sasa Dk. Kadege ndiye amejitokeza waziwazi kupambana na Kilango katika kinyang'anyiro cha ubunge wa Same Mashariki.
"…Nina uhakika mkubwa huu mkakati nisingeugundua ungenimaliza maisha yangu na uzao wangu," anaeleza Kilango katika barua yake kwa Makamba.
Kilango amedai katika barua yake kwa Makamba kwamba Dk. Kadeghe na watu asiowajua, wamefanya njama za kutaka kumfungulia kesi ya jinai ili wamfunge.
Mbali ya barua, Kilango ambaye ni mmoja na wabunge machachari, amewasilisha kama ushahidi, mkanda wa CD wenye sauti anayodai ni ya Dk. Kadeghe.
"Nawasilisha kwako kanda yenye mazungumzo yenye mkakati uliotayarishwa na Ndugu Dk. Kadeghe na wenzie nisiowajua katika mazungumzo ambayo yamerekodiwa," anaeleza katika barua yake.
"Hapa kuna kauli anayosema ‘tuna mkakati wa kumshitaki yule mama, lakini tunaona sasa siyo wakati mwafaka tutaleta malumbano," imesomeka sehemu ya barua ya Kilango iliyotiwa saini Mei 4, mwaka huu.
Kilango anahoji, "Swali, kama nina makosa yanayostahili nishtakiwe kwa nini wasifanye hivyo, wafanye kusubiri wakati mwafaka ni upi?"
Sehemu ya barua hiyo ambayo MwanaHALISI imeona inasema, "Ni moja kwa moja wananitengenezea kesi ya jinai, wanayoijua wao. Mwenyezi Mungu ni mkubwa sana na ndiyo maana anaitwa Mungu. Nina uhakika mkubwa huu mkakati nisingeugundua ungenimaliza maisha yangu na uzao wangu."
Nakala za barua hiyo zimetumwa kwa mwenyekiti wa kamati ndogo ya udhibiti na nidhamu, Pius Msekwa na mwenyekiti wa CCM (W) Same, August Kessy.
Makamba hakupatikana kuzungumzia tukio hilo, lakini Makamu Mwenyekiti CCM, Pius Msekwa amesema suala hilo halijafika mezani kwake. Amesema kiutaratibu mambo kama hayo huanzia kwa katibu mkuu.
Naye Dk. Kadeghe alinukuliwa na vyombo vya habari wiki iliyopita akisema CD ya Kilango ni "feki."
Katika CD yenye sauti inayodaiwa kuwa ni ya Dk. Kadeghe, kuna maneno, "…opposition (upinzani) walishinda lakini ukafanyika ujanja". Kama hivyo ndivyo, Peter Kuga Mziray aliporwa ushindi.
Siku Kilango alipoandika barua kumshtaki Dk. Kadeghe, ndiyo siku uliposambazwa ujumbe wa simu ya mkononi ukidai mbunge huyo amesambaza kadi feki kwa lengo la kupata watu wengi zaidi wa kumpigia kura za maoni.
"Huu ni uzushi. Leo nimezungumza na mwenyekiti wa CCM wilaya," anasema Kilango baada ya kuonyeshwa ujumbe unaosambazwa.
"Uongo mtupu," aling'aka Kilango alipokuwa akihojiwa na mwandishi Ijumaa iliyopita.
Ujumbe huo, ambao ulikuwa kiini cha habari nzito kwenye vyombo mbalimbali vya habari Jumamosi unasema, "Leo ukaguzi wa daftari la wanachama wa CCM umefanyika katika Jimbo la Same Mashariki.
"Kadi feki kibao zimegundulika katika matawi yaliyo katika ngome Kilango. Kadi zimepatikana katika tarafa ya Mamba/Vunta; huko Goha, Myamba, Mbinji, Kirangare, na Vunta," ilisema sehemu ya ujumbe.
"Mwenyekiti wa CCM (W) Same, makatibu na madiwani wametajwa kuhusika na kashfa hiyo ya kugawa kadi za CCM bure kwa lengo la kumsaidia Kilango ili apite katika kura za maoni," ulisema ujumbe ambao pia ulitumwa kwa Kilango.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, kadi feki zilipelekwa na Kilango mwenyewe na kuzikabidhi kwa watendaji wa CCM (W), madiwani, makatibu kata na matawi.
Sehemu ya mwisho ya ujumbe huo mrefu inasema, "Ni mradi wa Kilango. Uhakiki ulifanywa na Katibu wa CCM (M) na Katibu CCM (W), Sofia Kilingo."
Alipoulizwa Kilingo kuhusu madai hayo, alisema naye amesikia tu maneno ya kuwepo kadi feki lakini hajaona kadi hizo.
"Huyo anayeeneza hayo maneno kuwa kuna kadi feki sijui alifanya ukaguzi wake lini na wapi. Mimi ndiye ninayefanya uandikishaji na uhakiki wa sasa," alisema Kilingo.
"Hivi ninavyozungumza na wewe niko huku milimani katika eneo la Miamba na nikitoka huku nitakwenda Kihurio," alifafanua.
Kilingo alitupilia mbali pia madai ya kilichoitwa kusudio la Kilango kushitakiwa.
Tangu enzi za chama kimoja, kumekuwa na ushindani mzito wa kuwania nafasi ya ubunge katika majimbo mengine nchini. Kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, kulifuatiwa na mbinu za kuchafuana zilizoshika kasi 1995.
Jimbo la Same Mashariki lilipata mtikisiko wa aina yake mwaka 2005 wakati Kilango, Dk. Kadeghe, Naghenjwa Kaboyoka na wengine watatu walipoonyesha nia ya kumng'oa Mbunge wa wakati huo na Waziri wa Madini na Nishati, Daniel Yona.
Kilango aliibuka mshindi katika kura za maoni ndani ya CCM, akifuatiwa na Kaboyoka, waziri Yona, huku Dk. Kadeghe akishika nafasi ya nne.
Lakini, baada ya kuangalia alipojikwaa na njia ya kupita aweze kuibuka mshindi ndani ya CCM, Dk. Kadeghe, ambaye ni Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari ya Perfect Vision iliyopo Dar es Salaam ameonyesha nia tena.
Alipoulizwa iwapo hapendi ushindani jimboni, Kilango alisema, "Hapana. Hapa ninachosema ni kwamba zisiwepo hila. Dk. Kadeghe amepiga kambi mwezi mzima jimboni anajifananisha na mbunge aliyeko madarakani."
"Twendeni kwenye uchaguzi kwa hoja zenye msingi; tutawafanyia nini wananchi, tutapambana vipi na umaskini wa wananchi na kumaliza kero zao," ameeleza Kilango.
Amesema anataka watu wajue tofauti ya mbunge aliyeko madarakani na mwanachama wa CCM ambaye ameonyesha nia ya kugombea ubunge.
"Sasa hivi, wakati wowote, napaswa kufanya mikutano ya hadhara na ya ndani kutatua kero za wananchi na kuibua miradi mpaka Bunge litakapovunjwa," anaeleza Kilango.
Huku akionyesha kitabu kiitwacho "Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi na Serikali yake: Jimbo la Same Mashariki 2005-2010", Kilango anasema mbunge makini anapaswa awe anafanya kazi kubwa sasa, hasa kama ni wa CCM.
Anasema kupitia chama chake ngazi ya wilaya, anapaswa apite, kuanzia kwenye vitongoji, akieleza amefanya nini; madiwani wamefanya nini na serikali yake imefanya nini katika kipindi cha miaka mitano
Anakiri kwamba kila mbunge ana staili yake. "Staili yangu ni hii, nimeandika kitabu na ndani yake nimeeleza nilivyotekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM kwa maandishi; na kila diwani nimemwambia aeleze amefanya nini."
"Kitabu hiki ndiyo silaha ya CCM katika jimbo langu. Akija Chadema au nani silaha ni hii hapa. Nakala 10,000 ziko mikononi mwa wananchi," anaeleza kwa njia ya kujigamba.
Kilango anasema alikuwa na kikao na mwenyekiti wa CCM (W) wiki nne zilizopita kupanga mikakati; lengo likiwa kutompa mtu yeyote fursa ya kudai kuwa CCM haijafanya kitu.
"Kwa hiyo, yule aliyeonyesha nia ya kugombea kupitia CCM yuko mbali na mbunge aliyeko madarakani," alijinasibu.
Katika kitabu hicho cha kurasa 54, MwanaHALISI ina nakala yake, Kilango ameeleza alivyoshiriki kubuni na kuchangia miradi ya ujenzi wa shule za msingi, sekondari za kata za kidato cha nne, sekondari za kata za kidato cha sita, zahanati, kuchimba visima na kujenga barabara.
Kwa mujibu wa kitabu hicho, Kilango amechanga fedha taslimu, matofali, mabati, saruji, mbao, kuwalipa mafundi na kugharimia usafirishaji na ugawaji wa vitabu vya kiada na ziada. Vilevile amechanga fedha na vifaa kwa wakazi waliokumbwa na mafuriko.
Hata hivyo, anakiri kwamba CCM ilifanya kazi ya ziada kupata ushindi mwaka 2005 kutokana na mgombea wa ubunge kupitia PPT Maendeleo, Peter Kuga Mziray kujikita hadi ngazi ya chini. CCM ilishinda kwa asilimia 62 tu.
"Kwa mwanasiasa yeyote aliye makini, PPT Maendeleo mwaka 2005 ni vyema tukubali ilisumbua Jimbo la Same Mashariki na isingetumika siasa ya uhakika na iliyopevuka jimbo lingeweza kuathirika zaidi," anasema.
Tangu wakati huo Kilango alichukua ajenda za chama hicho cha upinzani na kuziweka kama dira yake.
Anasema, "Ndugu Kuga agenda zake zote nilizichukua kama dira yangu ya kufanyia kazi jimbo langu na pia kama dira yangu kubwa ya kukidhoofisha chama chake jimboni."
Chanzo: Mwanahalisi
My take: Kaza uzi mama, you are a real fighter among many. Hii ndiyo price one pays kupambana na maharamia wa ufisadi. You will succeed.