Recta
JF-Expert Member
- Dec 8, 2006
- 855
- 38
Sijaona sababu za kuwa na Mawaziri ambao wanachaguliwa moja kwa moja na wananchi. Sioni tija itakayotokana na uamuzi wa Baraza la mawaziri la namna hiyo.
Ni vyema uteuzi wa mawaziri ukapitishwa na Bunge kwa kuzingatia mabo kadhaa. Baadhi ni kama yafuatayo;
1. Uwezo wao kiutendaji wa kazi
2. Majukumu na vipaumbele vilivyopo
3. Elimu
4. Nidhamu
5. Historia yao
6. Mengineyo
Kwa utaratibu wa sasa,ambao waziri ni rafiki wa Rais na uteuzi wake unazingatia hilo pekee, ndio chimbuko la udhaifu wa serikali ambao tunaushuhudia katika awamu zote za uongozi wa nchi.
Ni vyema pia Rais akapata usaidizi wa namna ya kufanya uteuzi wa Mawaziri. Namna ninayoona ni bora, ni kuwa na mawaziri wasio na wadhifa mwingine wowote (hata Ubunge), wafanyiwe tathmini kabla ya kuteuliwa (kwa kuangalia CV zao, n.k)