Anne Kilango ataka mawaziri wachaguliwe na wananchi

MBUNGE wa Same Mashariki, ameponda mfumo wa kuwapata mawaziri na kupendekeza kuwa wachaguliwe na wananchi kama ilivyo kwa rais.

Soma habari kamili hapa:
http://tzlivenews.com/blogs/blog/3405-anne-kilango-ataka-mawaziri-wachaguliwe-na-wananchi.html
HILI NDIYO TATIZO LA UNGA UKIZIDI MAJI
Hivi mawaziri waziri [at least most of them] si wabunge waliochaguliwa na wananchi???
Sasa hali kama ikiwa hivyo anavyopendekeza huyu mama uwajibikaji wa serikali utakuwaje??? Maana kwa hivi sasa Rais ndiye anayewajibika kwa wananchi kuhusu utendaji wa serikali. Hivi hawa wakubwa huwa wanatafakari kauli zao kabla kuzitoa au ndiyo wakati wa kampeni umefika????
 
Wasiwasi wangu ni kwamba tukiwa na mawaziri wengi na wabunge wengi tutatumia pesa nyingi sana za walipa kodi.

Ila tutafute mfumo ambao utatuletea maendeleo, mfumo ambao utabana wizi na ufisadi uishe au upunguwe kutoka sehemu zote na hasa serikalini. Mfumo ambao wakulima wetu na watu wa hali ya chini watapata huduma muhimu - basic needs zipatikane kwa urahisi na kwa watu wote.

Tutafute njia ambayo watanzania sasa waanze kuipenda nchi yao toka moyoni na kikweli kweli.
Ufisadi umekithiri kila sehemu serikalini watu ni kufoji risiti na safari saa zote, pesa zinaibiwa kila kona TRA kila siku pesa mabilioni yanaibiwa, BOT ndiyo balaa, huko TIC mambo ni hovyo hovyo.
Watanzania tufanyeje sasa.

Mtu anaanza kazi leo baada ya mwaka ana ghorofa la thamani ya milioni 500, gari la milioni 200, watoto wanasoma chekechea SOUTH AFRICA, hii ni kazi gani inayolipa mapesa yote haya tena mfanyakazi wa serikali!!!!!!, biashara gani anazofanya????? je kama ana mahela yote haya KODI ZA TRA analipa ipasavyo???!!!!

Kuna wafanya biashara wengi sanaaaaa rafiki zao, ndugu zao ni maboss TRA na hawalipi kodi ipasavyo.

Sasa tutafute ni uongozi gani utakuwa imara na makini kusimamia mambo yote haya bila kuogopa.
Je mawaziri watakaochaguliwa na wananchi wataweza kufanya kazi vizuri bila uoga?? au mawaziri watakaochaguliwa na wananchi ndiyo walio bora???!!!.

Mimi binafsi bado sina jibu.

Ila tungepata raisi mmoja akasaidiana na jeshi kuondoa uovuuuuu na ujinga woteeeee kwa muda wa miaka 3 tu itatosha.

Tuwe kama China, tusichekecheke ovyo bila mpango watanzania wengi wanaumia.
 
sasa Anne naye anakosea... ikiwa wabunge kama chenge, ngeleja, masha, rostam ni machaguo ya watu, hao mawaziri si itakua balaa??

tutaishia kupoteza muda kukampenia wizara fulani kwa interest ya watu fulani, nadhani hili ni wazo mgando
 
Wakati mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete anaingia madarakani alisema kuwa atakuwa na baraza la mawaziri dogo lenye kuwa na tija katika Taifa
Kinachonishangaza ni huu mfumo wa Baraza la Mawaziri wa awamu hii ya nne. Wizara moja kuwa na mawaziri wawili na manaibu waziri zaidi ya wawili. Je mfumo huu unaongeza tija na kuharakisha maendeleo ya nchi au ni mzigo kwa walipa kodi wa nchi hii?
Mfano Wizara ya fedha ina manaibu waziri wawili na BOT ina naibu Gavana watatu. Je kuna mantiki yeyote ya kuwa na idadi kubwa ya watu katika wizara hizi? Au ni ulipaji fadhila na urafiki ndio unatawala?
 
Pasco,
Kwa FMES huyu mama ni kama vile huwa hakosei, hatelezi na wakati mwingine anafikiri na kuamua kwa niaba yake!

- Great Thinker, siongozwi na wivu, chuki, a majungu, yaani kila anachosema Mama Super K Mhesmimiwa mbunge ni kibaya tu hakiwezi kuwa kizuri,

- Glad kwamba sifikiri kwa niaba yako maana siwezi beba hizo sumu as you do! Bwa! ha! ha! haya sema sasa kwamba FMES ni mtoto wa Malecela kama ulivyofanya last time Bwa! ha! ha! eti ukada wa upinzani, mara Chadema mara CCM, sasa ni kushambulia watu hapa badala ya kulisaidia taifa Bwa!
ha! ha!


Es!
 
Nimewahi kusema wewe ni mtoto wa Malecela! Wapi ndugu yangu? Sina sumu yoyote kwa yeyote. Niko huru kwelikweli. Sifungamani na yeyote, kikundi chochote, chama chochote. Ndio maana utaniona CCM, utaniona CHADEMA, utaniona kwa JK, kwa Mbowe, kwako, ili mradi tu uongee hoja yenye mshiko, inayojitosheleza bila matusi, kejeli....
 
Kamati za bunge zinatakiwa ziwe na nguvu,rais akimteua waziri,lazima apelekwe kwenye kamati kupitishwa.tatizo bongo CCM ni powerful,kuna corruption,nepotism hivyo kamati hizi hazikop powerful kuchunguza mteuliwa.

kwa mfano ,Kamati ya Fedha(PAC) kama ipo,ingemweka chini Mr Mkulo na kuangalia CV yake,utendaji wake toka PPF,scandal zako na mtoto mdogo etc.
Wangecheck MBA Almeida ni genuine au vipi.

Huyu Kilango ni populist and hypocrite!Hakuna mwanachi anachagua waziri popote duniani.Kwanza ajibu suala la millioni 200 yeye na mumewe.
 
sasa anne naye anakosea... Ikiwa wabunge kama chenge, ngeleja, masha, rostam ni machaguo ya watu, hao mawaziri si itakua balaa??

Tutaishia kupoteza muda kukampenia wizara fulani kwa interest ya watu fulani, nadhani hili ni wazo mgando



wabunge ni mawaziri na wanachaguliwa na wananchi,sasa huyu mh.kilango anataka nini tena.nadhani upeo wake kwa mambo mengine zaidi ya ufisadi ni mdogo sana.
 
Mfumo huo hauna tija yoyote zaidi ya kupeana bakshshi na ahsante kwa kazi haramu baada ya uchaguzi.Ndo maana wengi wa mawaziri mademu wamegawa ur....kabla ya kupewa cheo, shame on them!
 
wabunge ni mawaziri na wanachaguliwa na wananchi,sasa huyu mh.kilango anataka nini tena.nadhani upeo wake kwa mambo mengine zaidi ya ufisadi ni mdogo sana.

Ni kweli, samtaims ni bora abaki na anachojua... sio kila wazo basi lazima aliweke public!!! Mama amechemka

Kura zenyewe za wizi halafu tupige kura??

Mimi nadhani ni bora hata kupunguza admin structure yetu, mawaziri wawe wanafanyiwa interview na kushinda uongozi wa wizara kutokana na competency na si siasa...kama ni waziri wa miundombinu basi awe na qualifications sahihi na aombe kazi na achujwe ka mamati za bunge au bunge lenyewe
 
Nimewahi kusema wewe ni mtoto wa Malecela! Wapi ndugu yangu? Sina sumu yoyote kwa yeyote. Niko huru kwelikweli. Sifungamani na yeyote, kikundi chochote, chama chochote. Ndio maana utaniona CCM, utaniona CHADEMA, utaniona kwa JK, kwa Mbowe, kwako, ili mradi tu uongee hoja yenye mshiko, inayojitosheleza bila matusi, kejeli....
Thats the spirit bro.
 
Katiba ya Nchi ndiyo itakayotusaidia kuliweka sawa Baraza letu la Mawaziri itakapoainisha ni wizara gani na ngapi tuwe nazo. Vinginevyo mambo yataendelea kuwa hivi kishikaji tu.
 
Mama Kilango mwenyewe itabidi akanushe hili. Yaani mwandishi anataka kusema mama hajui kabisa maana ya uwaziri.

Jamani labda tukumbushane kuwa baraza la mawaziri ndiyo Rais mwenyewe. Yaani Rais ni Kichwa na baraza la mawaziri ni sehemu ya viungo vyake.

Sasa mawaziri wachaguliwe na wananchi ili iweje? yaani tuunde sasa chombo kingine cha dola?

 
May be she has any other logic on this. Lets us try to understand her idea first.
 
Mama Kilango mwenyewe itabidi akanushe hili. Yaani mwandishi anataka kusema mama hajui kabisa maana ya uwaziri.

Jamani labda tukumbushane kuwa baraza la mawaziri ndiyo Rais mwenyewe. Yaani Rais ni Kichwa na baraza la mawaziri ni sehemu ya viungo vyake.

Sasa mawaziri wachaguliwe na wananchi ili iweje? yaani tuunde sasa chombo kingine cha dola?

Mimi nina imani kabisa kwamba mama aliteleza au hakueleweka... tumpe bebefit of a doubt, labda ataweka mambo sawa very soon

Hivi yeye ni member wa JF?
 
Mimi nina imani kabisa kwamba mama aliteleza au hakueleweka... tumpe bebefit of a doubt, labda ataweka mambo sawa very soon

Hivi yeye ni member wa JF?

Kwa jinsi alivyo mwanamapinduzi lazima tu atakuwa hapa. Na ndo mana nikasema akanushe. Inawezekana hakueleweka.
 
May be she has any other logic on this. Lets us try to understand her idea first.

labda anahisi kwamba itapigwa naional vote na wale wanaopata za juu ndio wanaunda baraza la mawaziri... Mh!!
 
He makubwa,kwanza Raisi si anachaguliwa na wanannchi?so Tukichagua Raisi bora ni moja kwa moja kuwa atateua mawaziri bora.Sasa gharama zingine tena za kupigia kura mawaziri.Huyu mama hapa sikubaliani nae kabisa hapa kachemsha
 
Back
Top Bottom