Anne Kilango asoma biblia kuhalalisha rais kuunda tume ya katiba

Biblia inaposema 'Tiini Mamlaka' haikumaanisha za siasa za kidunia bali 'Mamlaka' au nguvu ambazo Mungu aliziweka duniani kama vile; Force of gravity, Friction force, Low of floatation, water cycle etc ambazo ni muhimu kwa maisha duniani
 
ccm inamlevya. Huyu mama sometime yes, sometime no. ccm wanaogopa kuwa katiba ikiundwa kinyume na matakwa yao basi madaraka kwao yatakuwa ndoto
 
Mama mshenzi yule,kwanza mwanake anaitwa nyange amemaliza India ila kanunua Cheti feki hana lolote kama mama yake..Shenzi kabisa
 
Asome tena kifungu katika bible kinachohalalisha unafiki.
Unahitajika kuheshimu mamlaka sawa lakini ukuu na nguvu za mamlaka hutoka kwa wananchi na huu ni wakati wetu kupima na kuamua ni nguvu kiasi gani tuzipe mamlaka zetu kabla hatujaanza kuzitii,
so aache kukurupuka na kuitumia Bible visivyo, kwa ufahamu aliounyesha hana wito wala mamlaka ya kiroho kuweza kuhubiri, kurefer au kuyafafanua maandiko matakatifu.
Pia Akumbuke kuwa unafiki na ufi.raji vimewekwa kundi moja.
 
Kwa maoni yangu binafsi ingekuwa na faida kwetu na wasomaji wote wa Jamii Forum kama tungejadili hoja alizozitoa Mh. Kilango badala ya kujadili nafsi yake na haki yake ya kusema akiwa ameshikilia Biblia au hakushikilia. Mh Kilango ni mtanzania kama sisi na ana haki kama sisi ya kutoa maoni anayoona ni sahihi. Pili, ni mwakilishi wa watu wa jimbo lake la uchaguzi. Ana haki ya kuwasemea pia. Kama mkristo pia ana haki ya kuitumia biblia. Hamna mtu mwenye haki miliki ya Biblia atakayemzuia au kumfundisha namna ya kuitumia. Labda viongozi wetu wa diini.

Mh Kilango katika muda wote aliotumia kuchangia amejaribu kuonesha uhalali wa Raisi kama Taasisi kuunda Tume ya Kukusanya Maoni Juu ya Katiba Mpya. Amejaribu kuzichambua na kuzipinga hoja za upande wa pili. Kuna maeneo anawezakuwa alikosoea na kuna maeneo anaweza kuwa alipatia. Mjadala wenye faida ungekuwa ni kuonesha mapungufu katika hoja zake kwa kujenga hoja na kwa lugha ya kuheshimiana kuliko kumtupia taka machoni bila hoja ya kuhalalisha. Tungejadili hoja zake tungewasaidia watu kuelewa makosa yake au ukweli wake
 
Back
Top Bottom