Anne Kilango asoma biblia kuhalalisha rais kuunda tume ya katiba

Izack Mwanahapa

JF-Expert Member
Apr 21, 2011
497
236
Leo asubuhi katika Jambo Tanzania TBC, Anne Kilango Malechela amesema kati vifungu ambavyo havitabadilika katika muswada wa katiba ni kile cha Rais kuunda tume ya Katiba na kuhalalisha hilo amesoma Bibilia mstari unaosema kwamba tiini mamlaka iliyopo akisisitiza kuwa ni lazima mkuu wa nchi kuteua baraza la katiba.
 
Mama Kilango kagundua kambi zilizopo sasa anaangalia wapi aegemee, nina wasiwasi sana na hii katiba tunayoitegemea from teh current contingency
 
Tatizo tumekuwa na wabunge wasiokuwa na uwezo wa kufikiri. Wanaishia kutoa mipasho na maneno ambayo ni kawaida kuyasikia kutoka kwa

wanawake waswahili wasiokuwa na kazi wala waume. Unapomchagua mtu halafu anaongea upuuzi bungeni inakera sana. Badala ya kujadili hoja ya

msingi watu wanaunga mkono hoja chap chap then wanaanza kuponda Chadema. Hatuwezi kupata katiba mpya kwa kupashana bungeni au

kuiponda chadema na wanaharakati. Wabunge wetu wasipowaza sahihi watakuwa wanatengeza maafa kwa nchi hii.
 
Leo asubuhi katika Jambo Tanzania TBC, Anne Kilango Malechela amesema kati vifungu ambavyo havitabadilika katika muswada wa katiba ni kile cha Rais kuunda tume ya Katiba na kuhalalisha hilo amesoma Bibilia mstari unaosema kwamba tiini mamlaka iliyopo akisisitiza kuwa ni lazima mkuu wa nchi kuteua baraza la katiba.

Kasomea theolojia wapi na lini? Hana mamlaka ya kutafsiri maandiko matakatifu kwa umma. Kama anataka kuwa mama mchungaji akaanzie katika ngazi ya familia ama akasome theolojia. Kwa nini wanasiasa wanalewa power hadi kufikia hatua ya kuchezea maandiko matakatifu ili kufanikisha dhamira zao chafu?
 
leo asubuhi katika jambo tanzania tbc, anne kilango malechela amesema kati vifungu ambavyo havitabadilika katika muswada wa katiba ni kile cha rais kuunda tume ya katiba na kuhalalisha hilo amesoma bibilia mstari unaosema kwamba tiini mamlaka iliyopo akisisitiza kuwa ni lazima mkuu wa nchi kuteua baraza la katiba.
huyo mama ana matatizo.
 
Leo asubuhi katika Jambo Tanzania TBC, Anne Kilango Malechela amesema kati vifungu ambavyo havitabadilika katika muswada wa katiba ni kile cha Rais kuunda tume ya Katiba na kuhalalisha hilo amesoma Bibilia mstari unaosema kwamba tiini mamlaka iliyopo akisisitiza kuwa ni lazima mkuu wa nchi kuteua baraza la katiba.
Anna Kilango alikua anajiita mpinga mafisadi ila sasa juu ya mswada huu amegeuka na kuwa wakili wa mafisadi, hakika Anna kilango kwa sasa anatokwa povu kuhakikisha mianya ya ufisadi inaachwa wazi ktk mswada huu ili ufisadi,dhuluma,unyanyasaji uzidi kutafuna taifa letu.
Laiti kama Mama Anna Kilango angeacha kujifungia ndani na kukaa na commoners angegundua kuwa dhamira huru na ya ukweli haitishwi na maji wa kuwasha,virungu wala risasi za moto.
Kaa macho mama Jumanne.
 
Hata ukimuuliza huo mstari unapatikana kitabu gani katika biblia hawezi kukuambia, amekariri tu tiini mamlaka, huyo sio bure kuna kitu anakitafuta

Huyu mama ni POPO. sikutegemea angeongea upuuzi kama ule aliousema bungeni. na siku zote biblia haisomwi mstari mmoja
 
Back
Top Bottom