Anne Kilango ametusaliti Same Mashariki

Kayabwe

JF-Expert Member
Jan 8, 2012
355
51
Mbunge wetu wa Same Mashariki ametusaliti baada ya kutuahidi Kiwanda cha tangawizi kitaanza kufanya kazi msimu huu wa mavuno na kupandisha bei kutoka 1200 hadi 2500.

Kutokana na ahadi yake sisi wananchi tukatumia juhudi kubwa ya kulima tangawizi kwa feza za mikopo kutoka SACCOS zenye riba kubwa na maduka ya watu binafsi kwa riba kubwa.

La kushangaza hadi leo kiwanda hakijaanza kazi na bei imeshuka hadi 700. Linalouma zaidi Wabunge wenzake wanaotoka sehemu wanazo lima Pamba, Korosho mpaka Alizeti wanatetea Wananchi wao Bungeni yeye yupo kimya.

Au na Swala hilo liko Mahakamani?.... Halipaswi kuongelewa Bungeni?
 
Bado mnamategemeo ya Ahadi za CCM ......si huyo mama mnamuonea sema CCM imewasaliti kwani hizo si irani za Chama chenu cha magwepande
 
yupo zake New York atawakumbuka saa ngapi?
409436_3178707585829_2089635103_n.jpg
 
Back
Top Bottom