Anne Kilango achukua fomu ya kuwania spika wa bunge

Tutaongea weee... lakini ukweli uko palepale, Anna/Anne hafai, hawezi na hatapata uspika wala unaibu spika... labda kubeba ile fimbo kila siku

Unajua Kikwete kaharibu kila kitu nchi hii, Kikwete alivyofanikiwa kuwa rais basi kila mtu anataka kuwa kila kitu, kuanzia Zamaradi kutaka kuwa mbunge kama feel good confidence building therapy mpaka Anna Kilango-Malecela anapotaka kuwa Spika wa bunge.

It's open season, kinachotakiwa ni ambition tu, ambayo kila mwanasiasa na mtoto na mjukuu wake wanayo. Uwezo si jambo la msingi.
 
Anne Kilango hafai kwa post ya uspika hawezi kutawala maono yake ni mtu wa kulipuka na kile kiti kinahitaji mtu mstahimilivu , msikivu na mwenye hekima vinginevyo na mapepe aliyonayo hataweza kuhimili misumari mizito toka kwa vijana machachari walioingia bungeni , kwa kifupi mimi nimewahi kufanya kazi maeneo ambayo kilango alikuwa ni mswaaa

- Mtu wa kulipuka, si-mstahamilivu, si-msikivu, mapepe hataweza kuhimili misumari mizito toka kwa vijana wanaoingia bungeni sasa, mkuu hizi ndio FACTS zinazokufanya useme Mbunge wa Same East, asifae kuwa Spika? Lakini ameweza kuchaguliwa na wananchi wa jimbo lake mara mbili mfululizo, amekua Mwenyekiti wa kamati ya maadili ya bunge wka miaka mitano, ambako hatujasikia tatizo lolote!

- Mkuu unajua una raise a very interesting ishu ya kama wananchi wa Same East nao wana matatizo kama ya Mama Kilango uliyoyasema, eti inaewezekana kua ndio maana wanamchagua kuwa mbunge wao maana wanafanana? Na kwamba wabunge wanaokubali kuongozwa naye bungeni on maadili na nidhamu na wao pia wanafanana naye au?

William.
 
Right,

Kama vile kujua kwamba William Malecela hawezi kuwa objective katika ku asses uwezo wa Anna Kilango-Malecela.

- Na kama sheria ya jamhuri na JF inavyosema siruhusiwi kumpigia kura Mama Kilango akigombea nafasi ya taifa maana siwezi kuwa objective!

William.
 
Unajua Kikwete kaharibu kila kitu nchi hii, Kikwete alivyofanikiwa kuwa rais basi kila mtu anataka kuwa kila kitu, kuanzia Zamaradi kutaka kuwa mbunge kama feel good confidence building therapy mpaka Anna Kilango-Malecela anapotaka kuwa Spika wa bunge.

It's open season, kinachotakiwa ni ambition tu, ambayo kila mwanasiasa na mtoto na mjukuu wake wanayo. Uwezo si jambo la msingi.

- Sheria ya jamhuri inasema wananchi wawachague wabunge wao, ni uamuzi wa wananchi kuamua nani anawafaa halafu waliochaguliwa wakiingia bungeni sheria inasema wanaruhusiwa kugombea nafasi zozote as long as ni wabunge, hapo ni uamuzi wa wabunge kuamua nani anafaa na nani hafai kwa kutumia kura zao,

- Sisi wananchi tulioko huku kwenye uwanja wa Great Thinkers ni wajibu wetu kujadili anayefaa na asiyefaa kwa kutumia FACTS ili tuweze kuwasaidia wabunge watakaowapigia kura wanaogombea U-Spika huko ndani ya bunge.

William.
 
Willam usitupotezee muda kujadili vitu ambavyo havipo kama Kilango kachukua fomu mwache achukue uspika haupati, demokrasia unayoiongelea haipo ndani ya CCM, muulize mzee Malecela atakueleza. Makamba and his company they know who is going to be next speaker, Kilango does not have credentials, CCM will always pick person who loyal to the party machine.
 
- Well, ninakupotezea muda maana nimekuwekea bunduki kichwani kusoma huu mjadala au mawazo yangu, mwananchi yoyote aliyechaguliwa ubunge anaweza kugombea U-Spika, kama ataupata au haupati sio tatizo langu,

- Ninachosema ni kwamba sheria ya jamhuri inasema mbunge yoyote anaruhusiwa kugombea U-spika na akawa iwapo atashinda kura za uchaguzi ndani ya bunge, mimi ninaongela taifa na katiba hapa siongelei Mama Kilango maana taifa la Tanzania ni kubwa sana kuliko anybody sasa kama tunajadili uwezo wa Uspika, then ninaamini tunaweka njia ya Spika wote watakaokuja huko mbele ya safari kwamba wawe na sifa gani, pole sana kwa kutonielewa.

- Halafu unasema wanachagua mtu ambaye ni loyal to the party machine, hebu tuelimishe kidogo kuhusu Spika Sitta, alichaguliwa kwa sababu ni loyal to the party machine?

William.
 
Bwana malecela unafaa kuwa great thinker, maana haubishi bali unatohoa hoja na kujibu hoja, kwanza lazimatulitanbue hili la kuwa hero ktk group ya watu flani na bogus kwa wengine, siku zote huwezi kujumlisha kila siku ili tupate alama ya = ktk hesabu ni lazima matendo yote yakamilike,hata same mama kilango hajapata 100% kuna waliomkataa ambao kwao ni bogus, lakini ukweli utabaki kuwa amepita coz kura zimetosha for the same. Kuwa spika ni haki yake na anonyesha ni kiasi gani alivyo shujaa huyu mama, tunamjaji vibaya wakati kamati alizoziongoza bungeni zinakubalika, sas kama kiranja anaweza kuwa kiranja mkuu next term kwa nini m/kiti wa kamati bungeni asiwe spika baadae, tuwe wwerevu katika kudadavua hoja watu wamekalia ucc na chadema utadhani nini cjui
 
- Ahsante sana mkuu, hii yako ninaikubali kwamba ni pure Great Thinking na by the way I am having a blast na this kind of discussions, ndio maana onetime nilimuambia Waziri Sophia simba kwamba kwa nini CCM haileti watu wake hapa jamvini kwa nia njema ya kuelimishana with FACTS maana inaweza kusaidia sana kupunguza mis-leading nyingi zinazotokea hapa kuhusu CCM, na malumbano yasiyo na faida kwa taifa.

- Na juzi nimewakumbusha tena CCM kwamba viongozi karibu wote wa Chadema walioshinda ubunge majuzi, huwa wako connected na internent, either wana web zao binafsi, au wanashirki kwenye mijadala ya wananchi mitandaoni, maana yake ni kwamba Tanzania tunasogea pole pole na siasa za internent, infact nimewakumbusha kwamba ukiangalia hotuba nyingi za Dr. Slaa utakuta hoja nyingi sana ambazo zinatokea hapa JF, hope CCM somo litaeleeweka.

-Otherwise, thaanks mkuu!

William.
 
Sheria ya Jamuhuri inasema mtanzania yeyote mwenye sifa zinazokubalika anaweza kuogombea nafasi ya spika wa bunge la jamuhuri na si lazima awe mbunge hata wewe William kama unajiona una sifa unaweza kugombea nafasi hiyo, kama unaongelea suala la mtu kuchukua fomu na kugombea hiyo ni haki ya kila mtu kikatiba , hapa tunachojadili ni Anna Kilango kuchaguliwa kuwa spika. Umeongelea suala la wananchi kusaidia kuwashauri wabunge wetu nani kumchagua kuwa spika hiyo haijawahi kutokea. Kuhusu Sitta kuchaguliwa kuwa spika, wakati wa kuteua mgombea wa CCM 2005 kulitokea mgawanyiko ndani ya CCM, kulikuwa na kundi la Malecela na kundi la kina Mkapa ambalo limsimamisha Kikwete. Kilichotokea baada ya chaguzi za bunge msuguano uliendelea ndani ya CCM kundi la kina Malecela ndilo lilomsaidia Sitta kushinda uspika, Kikwete alikuwa ni mwenyekiti mchanga wa ccm hangeweza kulizuia hilo, hiyo demokrasia unaoyoingelea haipo Tanzania kama ipo ipo kwenye vitabu, sifa za spika zipo kwenye sheria za bunge, hapa najadili CCM watamtaka mtu gani awe spika nadhanai wewe ndio hunielewi.
 
Mapepe matupu, Spika kazi inataka mtu aliyetulia ile. Mama ana ma beef kibao ndani na nje ya chama chake, mimi nilikuwa nataka mtu aliyetulia kuliko hata Sitta, kama choice ni huyu mama na Sitta bora hata Sitta.

Ultimately, tatizo la bunge letu na Uspika, ni institutional sheepism, na wala si swala la personality, kwa hiyo as long as CCM wana majority, hata aje Spika gani kutoka CCM atashikishwa adabu na the party machinery tu, kwa hiyo hesabu za personality change wala hazina maana. I hope the control will gradually slide away from CCM to balance power within parliament.

Upinzani wana candidate gani? Hardly a realistic shot for them though, with the current numbers.

huyo mtu aliyetulia una maana gani? ivi spika ana kazi gani hasa mpaka awe mtu aliyetulia?
 
Sheria ya Jamuhuri inasema mtanzania yeyote mwenye sifa zinazokubalika anaweza kuogombea nafasi ya spika wa bunge la jamuhuri na si lazima awe mbunge hata wewe William kama unajiona una sifa unaweza kugombea nafasi hiyo, kama unaongelea suala la mtu kuchukua fomu na kugombea hiyo ni haki ya kila mtu kikatiba , hapa tunachojadili ni Anna Kilango kuchaguliwa kuwa spika. Umeongelea suala la wananchi kusaidia kuwashauri wabunge wetu nani kumchagua kuwa spika hiyo haijawahi kutokea. Kuhusu Sitta kuchaguliwa kuwa spika, wakati wa kuteua mgombea wa CCM 2005 kulitokea mgawanyiko ndani ya CCM, kulikuwa na kundi la Malecela na kundi la kina Mkapa ambalo limsimamisha Kikwete. Kilichotokea baada ya chaguzi za bunge msuguano uliendelea ndani ya CCM kundi la kina Malecela ndilo lilomsaidia Sitta kushinda uspika, Kikwete alikuwa ni mwenyekiti mchanga wa ccm hangeweza kulizuia hilo, hiyo demokrasia unaoyoingelea haipo Tanzania kama ipo ipo kwenye vitabu, sifa za spika zipo kwenye sheria za bunge, hapa najadili CCM watamtaka mtu gani awe spika nadhanai wewe ndio hunielewi.

- Well, mkuu nenda uanze upya na huu mjadala utaona tumefikiaje hapa tulipo otherwise, naomba nikuelewe unasema wewe unajua CCM wanamtaka mtu mwenye sifa zao ambazo wewe unazijua kuwa Mama kilango hana au?

- Halafu kuhusu Sitta kuwa Spika 2005, labda ukaangalie tena FACTS of how he became one!

William.
 
hakuna atakayepata uspika kama hana mtandao, lazima uwe na wanamtandao wengi ili uweze kupata hiki kiti
 
labda kama FACTS zako unazipata kwenye michuzi nitakubaliana na wewe, Kilango hana sifa zinazotakiwa na CCM; kwani CCM wameshafanikiwa kuizima kambi ya Malecela, Jemedari Makamba is one who run the show, whether you like it or not she will never be speaker, CCM had enough of Malecela crap.
 
Huyu mama hafai kabisa kuwa mbunge yeye abaki tu kuleta hoja na kuzipambanua tu ila uspika she is not the chosen one.

Mama Anne Kilango inasemekana amechukua fomu za kuwania uspika wa bunge,huyu mama alin'gaa sana kipindi kilichopita kwa ujasiri wake (sina uhakika) aliounyesha ,sasa huyu mama kaamua kuingia kwenye uspika , sijui kitu gani kimemshawishi kuingia huko
source:
Sitta, Anne, Anna... wachukua fomu kugombea Uspika -
 
Mkusanyiko wa viongozi waliojiteua kwa uwezo wa pesa zilizizoibwa kwa wananchi na kuzitumia kujijengea uimara wa kiuchumi na kisiasa huwa siku zote unatumia kila aina ya mbinu kurubuni wavuja jasho ambao ama hawakupata elimu ya kutosha kuweza kukokotoa hoja kukdhi haja ya wanaojiita wasomi waliopata elimu kwa gharama za kodi za hao hao wavuja jasho ambao siku zote huomba na kutumaini kuwa siku moja atatokea kiongozi asiye mbadhirifu na mwenye uchungu na nchi atakaye kuwa radi kuwakomboa katika hii minyororo mikubwa ya kifisadi.

Fedha za wavuja jasho (kodi) zimetumika kuwapa elimu nzuri ya ndani na hasa nje ya nchi vijana wa viongozi ambao mara wapatapo elimu hiyo hawaitumii kuliendeleza taifa lao kama ambavyo kwa mtu mwenye busara angefanya bali wengi wao huitumia elimu hiyo kujenga hoja za kulinda maslahi ya kisiasa na kiuchumi kwa niaba ya baba na mama na utitiri wa wa mali walizofisadi. Hivi ni kweli tusomeshwe kwa gharama kubwa nje ya nchi kwa kodi za wavuja jasho kisha tuitumie elimu hiyo kuwaona wasioweza kuchangia hoja kama nyie (wasomi wa fedha za kifisadi) kuwa hawajui kujenga hoja??? ni haki hiyo? eti kwa sababu mnatetea maslahi ya baba au mama? tafakuri....

Pili, majambo haya na mengineyo yanayojionyesha wazi katika utajiri uliokithiri wa wanasiasa ambao kabla ya kuwa siasani walikuwa sawa na wavuja jasho wengiwalivyo lakini ghafla baada ya kuingia madarakani wameweza kuwa na ama mahekalu ya mabilioni pesa ambazo hata kama ungejumlisha mishahara na mapato halali ya uongozi usingeweza kujenga hata banda la nyuma la mahekalu hayo. Lingine ni umilikaji wa mali ambazo zilikuwa za umma kwa viongozi wa kisiasa, familia zao. Pia umilikishwaji na kuwa hisa kubwa katika mali adimu kama madini na migodi yake, wizi wa mabilioni katika benki zetu, ukopaji wa mabilioni ktk benki za nchi yetu kisha kuyakimbia madeni kwa njia za mkato.

Mambo haya na mengineyo ndo humfanya mwananchi wa kawaida kushindwa kuelewa nini kinaendelea katka nchi yake yenye kila aina ya utajiri kuanzia madini, ardhi, bahari mito na utawala wa chama kimoja kwa miaka 50 tangu kuchukua uhuru kwa mkoloni msimamizi (Great Britain)...chakula mlo mmoja, huduma duni za afya uadimu wake , elimu duni, kazi hakuna, mishahara haikidhi mahitaji muhimu n.k
Ujumla huu wa hali duni za maisha wananchi na utajiri wa asilimia zaidi ya 200000 % kwa miaka 50 ya uongozi wa chama kimoja zimewafanya wananchi kutaka mabadiliko ya uongozi na viongozi ili walau wapate kuchangia kufaidi matunda ya nchi yao.Kura wamepiga kwa moyo mmoja ila matokeo yanachujwa au kwa msamiati mzuri zinachakachuliwa ili kulinda maslahi ya wachache na kudharau au kukejeri matakwa ya wengi....
 
Unajua Kikwete kaharibu kila kitu nchi hii, Kikwete alivyofanikiwa kuwa rais basi kila mtu anataka kuwa kila kitu, kuanzia Zamaradi kutaka kuwa mbunge kama feel good confidence building therapy mpaka Anna Kilango-Malecela anapotaka kuwa Spika wa bunge.

It's open season, kinachotakiwa ni ambition tu, ambayo kila mwanasiasa na mtoto na mjukuu wake wanayo. Uwezo si jambo la msingi.
ni kweli kabisa... Kikwete ahs made Anne look good...

we left politics to politicians and that exactly the punishment, it is a serious game to be left to formeR tejas, players, thieves, and fisadis...

Anne KiLango Malecela fits no frame in our set-up except ubunge, PERIOD
 
huyo mtu aliyetulia una maana gani? ivi spika ana kazi gani hasa mpaka awe mtu aliyetulia?

Spika ni moderator, atadeal na party politics katika ku deal na miswada, na hata katika parties kuna factions e.g, CCM Mtandao na wengine. Halafu hapo hapo kuna drama za kudeal na personalities kibao zenye egos za aina tofauti bungeni, kuanzia masela kina Mr. II Sugu mpaka ma profesa Tibaijuka wanaofikiri wamesoma mpaka kuona kibao kilichoandikwa "Hapa ndipo mwisho wa usomi".

Zaidi ya hapo kuna politics na mihimili mingine ya dola kama mahakama na uongozi, jaji mkuu mara anamrushia mpira Spika hoja ya mgombea binafsi si suala la kisheria ni suala la kisiasa lijadiliwe bungeni, mara rais kaunda kamati ya bunge sijui kuchunguza kitu gani, mara Rostam anataka ku influence vitu bungeni kwa habari za ufisadi kwa kupitia ofisi gani ya serikali, hapo hata sijaingia kwenye wapinzani watakaosema Spika anapendelea CCM na kudai equal, if not special treatment, bado sijaingia Wazanzibari na Wazanzibara, huyu mama atasnap na kututia aibu tu, hana staha wala uhimilivu unaotakiwa na hii kazi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom