Aneth Msuya ambaye ni dada wa bilionea Erasto Msuya auawa kinyama Dar

Nimepata taarifa hii ya mauaji ya kinyama ambayo imekuwa ikizunguka kwenye makundi ya WhatsApp....

Anathe Msuya mdogo wa Erasto Msuya bilionea wa Arusha aliyeuawa, amechinjwa usiku kuamkia leo nyumbani kwake eneo la Kibada block 16. Katika tukio lenye mazingira ya ujambazi lakini hakuna kilichoibiwa..


Inasomeka...

Anaitwa Annate, ni mdogo wake marehemu Erasto Msuya aliyepigwa risasi 22 Kia. Nimepigiwa simu asubuhi majirani walikuwa wanatafuta ndugu zake. Sidhani kama ni majambazi kwa sababu inasemekana hakuna kilichoibiwa. She was found lying naked on a pool of blood huku amechinjwa. Alikuwa anaishi na mtoto wake mwenye miaka mitano na dada wa kazi. Mtoto amekutwa akiwa amevaa sare za shule bado ikimaanisha hakuwa amebadili toka jana alivyotoka shule.

Yaani Aneth hata siamini, jana tulikua nae kazini, kaondoka kufika home kakuta housegirl katoroka, akapiga simu kwa mwenzetu akamueleza kwamba leo hatokuja ili angalie logistics. Ndio asubuhi Himalaya hizo taarifa. Mtoto wake ana miaka minne ndio anahojiwa anasema hiyo jana walikuja watu watano weusi, wakavunja mlango ni majira ya saa tatu usiku, akakimbia chumbani, walipoingia wakamkuta mtoto wakauliza mama yuko wapi akasema chumbani, wakamfuata huko mtoto hajui kilichoendelea hadi saa 1 asubuhi school bus imekuja anajaribu kutoka kashindwa ikamwacha, ndo akafanikiwa kutoka kaenda kwa jirani kawaambia school bus imemuacha, mama kalala haamki na mimi nasikia njaa. Ndio jurani kwenda wakakuta kachinjwa yuko uchi (seems walimbaka) kisu kipo hapohapo na hawajaiba kitu.

=======================

Dada wa bilionea Msuya auawa kinyama Dar

DADA wa marehemu Erasto Msuya aliyetambuka kwa jina la Anathe Msuya, ameuawa kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana Dar es Salaam.

Anathe aliuawa nyumbani kwake eneo la Kibada block 16, Kigamboni, ambako inaelezwa wauaji hao hawakuchukua kitu chochote ndani ya nyumba yake.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro, alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kuahidi kutoa taarifa kamili leo.

“Ni kweli kuna tukio hilo la kifo, lakini taarifa kamili kwa undani nitazitoa kesho (leo), ninaomba muwe na subira,” alisema Kamanda Sirro.

Anathe ni dada wa marehemu Erasto Msuya ambaye alikuwa mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite aliyeuawa kwa kufyatuliwa risasi.

Msuya aliuawa Julai 7, mwaka 2013 katika eneo la Mijohoroni, kando ya barabara ya Arusha – Moshi wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, akiwa ameitika wito wa kwenda kununua madini ya Tanzanite baada ya kupigiwa simu na vijana wawili waliomtaka wakutane maeneo hayo.

Inaelezwa kuwa alifika katika eneo hilo akiwa na gari lake aina ya Range Rover T 800 CKF na kuwakuta vijana hao wakimsubiri.

Baada ya kuteremka, Msuya aliekea kumsalimia mmoja wa vijana hao, hata hivyo kabla hajamfikia kijana huyo aliitoa bunduki ya SMG namba KJ 10520 aliyokuwa ameificha kwenye koti na kumfyatulia risasi takribani 22 mwilini.

Bilionea huyo aliyekuwa akimilika vitega uchumi mbalimbali jijini hapa na maeneo mengine nchini aliuawa saa 6:30 mchana.

Taarifa za polisi zilisema katika eneo la tukio ilikutwa bastola namba GLS 417T2 CAR 83271, mali ya Msuya na vitu vingine, ambavyo ni simu ya Samsung S5, iPhone na koti la mmoja wa watuhumiwa likiwa limetelekezwa mita chache kutoka eneo la tukio.

Polisi waliweza kuwakamata watuhumiwa wa mauaji hayo na kuwafikisha mahakamani mjini Moshi ambako kesi hiyo inaendelea kusikilizwa.

Gazeti Mtanzania

bd44aec3d72989beb86b6a0a490fd708.jpg

View attachment 351239

Hizi ni Picha za Marehemu enzi za Uhai wake
Lala mahala pema dada
 
Dah inasikitisha sana aisee, na wanamoyo kwa kweli hawa watu, na ukizingatia katoto bado ni kadogo maskini kanahitaji malezi kutoka kwa mamaake!

Duh hii kali, umri wenyewe huu wakuishi ni mfupi alaf unatoa roho za watu bila ya kujua na wewe itafika siku yako uta-dead

Very Sad
 
Haiwezekani kifo cha hivi kisitokane na matendo ya marehemu mwenyewe. Tuishi kwa kutenda mema ama sivyo tutaishia kupotezwa kama kuku. Mungu amuweke anakostaili


Mkuu, umechangia nilichotaka kusema.

Mara nyingi mauaji ya namna hii huwa yanahusiana na visasi.

Daaah apumzike kwa amani. Jeshi la police lifanye kazi yake.
 
What does the word ASSUMING mean to you...!!! Where did I confirm kua ndio waliomuua..!!! acha kukurupuka
Hivi nimesema ume-CONFIRM au nimesema usi-CONCLUDE?

Jifunze kukubali kurekebishwa! Najua unajua vitu vingi ..lakini pia ukirekebishwa hata kwenye vingine jifunze kukubali kukosolewa!

Dont major on minor!

After all no one knows everything!
 
MBERE yake nyuma yako na mimi pia, ila kuna kitu sidhani km tumefika pahala pa kuuana bira sosi, wadau hakuna tetesi? alikuwa anafanya kaz wapi? mshahara wake, mali zake, company zake, tabia zake, muumini wa dhehebu gani? tuanzie apo kutafta ukweli, pia vyombo vyan usalama anzieni nilipo dodosa.
 
Halafu utawasikia wale wanaojiita wanaharakati Wa haki za binaadamu kuwatetea wauwaji Wa namna hii wasiuwawe na wao.... R.I.p Dada ila naunga mkono adhabu ya kifo itekelezwe...

Haiwezekani watu wanachinjwa kinyama namna hii halafu mwisho Wa siku wauwaji wakula kodi zetu gerezani...
 
Dunia hii ina visa acha kabisa.Kama ni mumewe alifariki(kama mdau mmoja alivosema hapa) unaweza kuta ni mambo ya mirathi.

Yaani siku hizi hatari ya kifo ipo mlangoni kabisa,mara majambazi mara visa,mara magonjwa...yote kuyakwepa kwa wakati mmoja basi inabidi usijichanganye sana.
sio mumewe ni kaka yake
 
May ur soul rest in peace ..pia kisasi sio kitu kizuri kifo chake kinahusiana na muendelezo wa kesi ya kaka ake the far as i can see kuna kitu behind ukizingatia matajiri wa mirerani mhuu..i know most of then na system zao za kibabe na kuosheana sanaa include marehem erasto kaka mtu
 
H

Hivi mbona watu wa arusha wanapenda sana uongo. Sh 2 B unatembea nazo Vipi kwenye gari. Na gari anina gani. Au alikuwa anatembea na hiace au bus.

Bora umesaidia kushangaa, bilioni mbili ndani ya gari si mchezo.!
 
nyumba bado mpya,gari ya kutembelea,pengine angeweka watchman ingesaidia kidogo,ama atleast alarm system yakumtahadharisha kama kuna intruder

Mkuu mtu anaekuja kukua hakurupuki siku moja tu, ni maandalizi ya muda mrefu wakati mwingine na wewe unashirikishwa kwenye mpango bila kujua.
 
Kuna wakati huwa nawaza nafika mbali mno. Matumbo yetu wanawake yanabeba viumbe vyenye tabia za kila aina. Laiti Mungu angetupa neema ya kujua hatima ya mtoto aliyeko tumboni kabla hajazaliwa. Tungekua tunajua kuwa mimba uliyobeba utakuja kuzaa muuaji au jambazi la kuisumbua dunia nadhani wanawake wengi wangezitoa hizo mimba. Tunawaza mpaka tunaweza tukakufuru

Inawezekana wewe Ni mkatili kuliko hawa waliofanya haya mauaji kwa kuwaza kuua kiumbe asiye na hatia wala uwezo WA kujitetea., potelea mbali na mawazo yako maovu.
Leo hii wazazi Wako wangefanya unavyowaza ungelikuwepo??
Mimi nasema wanawake wengine makatili WA kiwango cha juu kabisa
 
Back
Top Bottom