Anna Makinda amponda Sitta kwenye kikao cha siasa Njombe

sheria ya serikali za mitaa ya mwaka 1982 RE 2000 Sec.5(1-5) inatoa mamlaka kwa waziri mwenye dhamana na serikali za mitaa kuanzisha halmashauri ya wilaya. na contents of establishment zinatajwa sec.6(a-c). procedures for establishment sec 7(1-5)
sasa huu uhuru wa mayani kujiamulia wapi yawe makao makuu ya wilaya unatoka wapi? na kama maombi ya awali ya uhitaji wa kuanzishwa kwa halmashauri mpya kwenda kwa waziri mhusika yalitoka kwa wananchi(baraza la madiwani) mihutasari ilikuwa inasema wilaya hiyo mpya iitwe jina gani? na makao makuu yawe wapi? na kama waziri alilizia kuanzishwa kwa wilaya hiyo je, alifanyia marekebisho yoyote kwa vigezo vya awali?

kimsingi sioni sababu ya hili nalo kuwa ishu? na kwa upande wa pili naona hii ndiyo gharama ya democracy kugeuka uhuru wa manyani

Nchi hii imekuwa ikiongozwa kwa ubavu
 
hili ni somo jinsi gani viongozi wetu walivyo wabinafsi..luhanjo anataka makao makuu ya wilaya yawe kwao ili iweje?je kama ni mbinafsi hata kwenye hili,ile kashfa ya kujaza watu wa kwao nafasi za juu kila wizara aliyopita anaikataa vipi?ccm imekufa bado kunuka tu,wasio na macho ndio bado hawajaliona hilo,tunasubiri inuke tuone kama na pua zao nazo hazinusi..
 
Ingekuwa vyema kama tungefahamishwa chanzo cha habari hii, kwa kuwa wasi wasi wangu ni kwamba tunaweza kuwa tunachangia habari ya 'kufikirika'.
Na kama ina ukweli wowote kuhusu chanzo chake, kwangu mimi hakuwezi kuwa na kanuni bila sheria. Kwa wataalamu wa sheria (mie si mmoja wao) wanatuambia kwamba kanuni ni tafsiri ya sheria, yaani (sheria ikisema hivi kanuni ndio inafafanua utekelezaji wa sheria hiyo).

Kwa kuwa lengo ni kusaidiana ikizingatiwa kwamba hatuwezi kusoma fani zote, kama nimekosea hapo juu nitakuwa radhi kurekebishwa kwa faida ya watanzania wenzangu.
 
Suala la makao makuu liamliwe na balaza la madiwani lugha ya kulipeleka kwa kikwete ni kiini macho kwani atakae amua ni Luhanjo. Kwa wale tunaoifaham vizuri wilaya hii mpya IGWACHANYA inastahili kuwa makao makuu kwani kijiografia ni katikati na miundombinu iliyopo inaruhusu. TUMECHOKA KUAMLIWA MAMBO YA NJOMBE WA2ACHE TUAMUE WENYEWE .
 
  • Thanks
Reactions: SG8
Baraza la madiwani liachiwe maamuzi ya kuchagua makao makuu kivuli cha CCM kisi2mike ku2gawa wana Njombe. Ni upuuzi usiokubalika kuweka makao makuu Wanging"mbe kwa ajili ya kumlipa fadhila Luhanjo m2 yeyote aneifahamu wilaya hii atakubaliana nami kuwa IGWACHANYA ni sehemu sahh kijiografia na miundombinu
 
Msipofanya hivi nitahamia Chadema
Msipofanya vile nitahamia Chadema
Mkitekeleza hili nitabakia CCM
Mkitekeleza lile nitabakia CCM
Nikibakia CCM msipotekeleza mliyoahidi nitahamia chadema
Noted with thanx
 
Anna bwana
sasa yeye ni spika wa bunge tena anasema anajua vizuri kanuni
yeye na Kikwete kuna tofauti kubwa? si hawa wote ni viongozi wa kitaifa
tena yeye anaongoza wabunge wenye mahusiano ya moja kwa moja na wananchi
imekuwaje ameshindwa kutatua suhala la wilaya mpaka Kikwete?

ina maana hata pale bungeni yana mshinda na kuomba msaada kwa Kikwete?
huku ni kuudhalilisha uspika bana,
spika anashindwa ushawishi wa wapi yawe makao makuu ya wilaya?

Kwenye kugawa wilaya aliyeplilia moto ni fisadi Luhanjo! yeye kwa ukaribu wake na Ikulu anatumia vibaya nafasi hiyo kuwadanganya wananchi kuwa ana ushawishi mkubwa kwa JK. Jamaa ni noma sana! kampandikiza yule mbunge mbumbumbu Lwenge kwa kulipa fadhila. kamjenga kwa JK hadi kampa unaibu waziri. mambo ya kubebana sijui yanatupeleka wapi?
 
Huyu luhanjo mbona ana ukabila hivi? juzi juzi alishutumiwa kuwajaza wabena wenzake maliasili, leo ameingiza ikulu kuwaamulia wana njombe wilaya iwe wapi.Jamani kama huyu ndo kiranja mkuu wa makatibu wakuu na anafanya kazi ikulu basi tumekwisha! Haya ndo ushikaji wa JK mara luhanjo mara jairo......nimechoka! anogopa nini kumpa Rdhiwani uwaziri
 
Tarehe 8/09/2011 siku ya alhamisi , kamati ya siasa wilaya ya njombe ilikutana ktk ofisi za ccm wilaya kujadili mambo mbalimbali likiwemo suala la hali mbaya ya kisiasa kwa ccm baada ya kuchakachua kura za maoni 2010 na agenda ya makao makuu ya wilya mpya iliyo anzishwa hivi karibuni.

Wajumbe waliweka bayana kuwa kuna mpasuko mkubwa katika jimbo la njombe magharibi uliotokana na kuchakachua kura za maoni ambapo mtu aliyepita kwa kura nyingi ni yono kevela lakini kura zilichakachuliwa kwa ushawishi wa philimoni luhanjo na kumuweka Gerson Lwengwe(Naibu waziri maji) ambaye amemjengea nyumba Luhanjo pamoja na kashifa za kufukuzwa Tanroad kwa ufisadi.

Mhe Lwenge alisikika akilalamika nje ya kikao kuwa , wapiga kura wake wanampigia simu na kumutukana na anawafahamu na kumwambia katibu kuwa ubunge wake upo rehani.
Alimwambia kuwa yeye kwa sasa ni kama jiwe.
Baada ya mjadala mkali wameazimia kwamba wabunge wote wilayani humo wachange pesa na kuanza shughuli za siasa kupambana na chadema.
Wajumbe walisema kwamba ccm haikubaliki na watu wengi wanahamia cdm na wanafungua matawi mapya.

Agenda ya wapi iwe makao makuu ya wilaya mpya yalileta mgogoro mkubwa kiasi cha kutoleana maneno makali.

Mh lwenge amehamisisha madiwani 11 wa eneo la igwachanya(anakotoka lwenge) na kuweka matambiko ya kimila na kuweka msimamo kuwa makao lazima yawe hapo na kama watakataa wanahamia chadema.

Philimon Luhanjo naye ameandika barua kutoka ikulu ikitowa maelekezo ya wilaya mpya huku akielekeza makao makuu yake yatakuwa wanging'ombe anakotoka yeye ili kumpa heshima na wakazi wa huko wanasema wasipo fanya hivyo wanakwenda chadema. Luhanjo anapiga debe eneo hilo kwamba yeye ndiye aliyesababisha wilaya hiyo iundwe kwa kumushawishi kikwete.

Maelekezo ya Kikwete yalikuwa ni kutoa wilaya mpya lakini wapi yawe makao makuu aliwachia wahusika wajadili na endapo watashindwa wamwambie awaamulie.

Sasa mvutano huo ulipamba moto na ndipo anna makinda alipo inuka na kutoa uamuzi kuwa suala hilo limeshindikana na kuandaa taarifa ya kumwachia kikwete awamulie watu wa njombe suala ambalo limewakera wazee wa kimila ambao tayari wamesha tambika.

Wakati anamalizia Anna Makinda alianza kuzungumuzia utendaji wa serikali ,mawaziri na wabunge wa ccm ambapo alianza na kumuponda Mh Samweli Sitta kuwa hajui shughuli za bunge na kwaba Anna Makinda amekaa sana bungeni na ndiye aliyemufundisha Sitta Uspika. Aliwambia wajumbe kuwa Sitta ni tatizo kwenye ccm na serikali kwa kuwa ni mwaasisi wa ccj na kwamba Sitta ndiye aliye kuwa anafanya kampeni za kusema Anna Makinda ni mbumbu wa sheria na hajui shughuli za bunge. Aliwambia wajumbe kuwa shughuli za bunge zinaendeshwa kwa kanunni na sio sheria. Na aliwataka wajumbe wamupuuze Sitta kwa kauli zake kwani zina vuruga ccm.

Maskini Bi Kiroboto. Ameshindwa kujua kwamba hata Kanuni za Bunge nazo ni sheria ambazo zinahitaji legal mind katika kuzitafsiri.
 
hahahahahahhahahahahha makubwa hayo kumbe huyu mama hana adabu kwani kukaa bungeni muda mrefu ndio nini?
 
[h=2]Anna makinda adaiwa kutumia ushirikina kudhibiti upinzani bungeni[/h]
Taarifa za uhakika kutoka njombe , zinaonyesha kuwa , spika anna makinda amefunga kondoo wawili , ambao wamepewa jina la michael na mwingine anaitwa george ambapo kondoo hao wanaishi kwa mganga wa kienyeji anayefahamika kwa jina la babu msomali.

Mganga huyo anaishi njombe mtaa wa mgendela chini ya msikiti mkuu wa wilaya ya njombe kama inavyo onyesha katika picha hizo hapo chini.

Anna makinda alipewa masharti na mganga huyo kupeleka vitu vifuatavyo:
Sare za chama cha mapinduzi,joho la usipika, nguo za kawaida ,kitabu cha wasifu wa makinda ambacho kina nembo ya serikali.
Kwa muujibu wa mganga huyo, joho la usipika lilifanyiwa utaalam na kurejeshewa anna makinda lakini kondoo, sare za ccm na kitabu cha wasifu wake bado vipo hapo kwa mganga.

Kitu cha kushangaza ni kwamba kondoo hao wanaishi kama watu na ukiwaita wanatii wito na wanaachiwa wakilanda landa hapo. Mkakati huo unafahamika vyema na diwani wa viti maalumu njombe mjini aitwaye roi haule ambaye amekuwa akitumwa kwa mganga huyo huku akiwa amuvaa kaniki kwa masharti ya mganga.

Mda mufipi baada ya anna makinda kupata kiti cha usipika arishauliwa na mganga huyo kusikwa kama chiefu wa eneo lote la njombe . Baadhi ya wazee wa mila wa eneo hilo walipinga mkakati huo na kususa sherehe za mwanamke kusimikwa kama chief ambapo walisema ni kinyume na taratibu za mila.

Viongozi wa makanisa ya kiroho walisusa sherehe hizo kwa sababu zilikuwa zina sura ya ushirikina.
Baadhi ya wakazi wa njombe wanasema anna makinda amekuwa akigombea pekee kwa sababu ya watu wengine ndani ya ccm kuhofiwa kufa kishirikina.
Viongozi wa makanisa ya kiroho wameanza kuhamasishana kwa siri kuombea taifa baada ya kushuhudia kondoo hao wakitumika kuongoza bunge na kudhibiti upidhani!!.​
paperclip.png
 
Anna makinda ana mponda sitta kwenye vikao na sitta anamponda anna makinda pia
nchi imeyumba
 
Nyimbo anafungua matawi ya chadema huko Njombe vijijini kama vile hana akili nzuli; hilo ndilo linawapa wasiwasi hao watu wa ccm!!
Good hili ndilo tunalotaka ili 2015 kazi iwe rahisi kama kusukuma mlevi vile peoplezzzzzzz powerrr!
 
Sijaelewa kabisa sasa hao kondoo anawafanya nini ili upinzani usifurukute? Mambo ya ajabu kabisa na ndio maana hatemdelei.
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom