Anna Kilango achafua hali ya hewa kamati ya Miundombinu

Nadhani M4C imemchanganya!
Apewe msaada wa kisaikolojia!
Alichofanya si ishara ya uongozi bora hata kidogo.
Hatimaye, tunapima viongozi wetu si kwa sauti zao,si kwa makelele yao.
Tunawapima kwa matendo yao.

kwenye Blue nampa A+
 
hamjui kuwa huyu mama ana matatizo ya kiakili?

Ile familia yao imeingia kirusi cha nyuklia kinawakula.

Baba anaumwa kaugonjwa kanakoitwa PRESIDENTIMANIA
mama yeye kapata FIRSTLADYMANIA
Mtoto yeye aliukwaa u EALAMANIA

Tuendelee kuwaombea
 
Sijawahi kumuamini hata siku moja kwa kila anachoongea huyu maza, sijui kwanini. Naona anafaa kuwa muigizaji zaidi kuliko mbunge.
 
Hizi zote ni SERA za CCM katika muendelezo wake wa kuvua magamba watu a.k.a kusafisha oil chafu .... CCM msirudi nyuma !
 
Hivi hizi kamati kweli zitzfanya kazi mwaka huu? Hiyo ya LAAC ndio hivyo mwenzao kakamatwa akiwachukulia advance ili wapitishe mahesabu ya Mkuranga, Miundo mbinu nao wameanza kufanyiana majungu
wananchi tutegemee lolote kwa kwa aina hiyo ya wabunge?
miundo mbinu inaongozwa na Mwakiembe na serukamba ni kambi ya El,El na mwakiembe ni kama ujuavyo nadhani umeiona picha mkuu wangu.hiyo ndo ccm
 
Mama Kilango si mtu wa maana sana linapokuja swala la uongozi bora, lakini kwa hakika Serukamba ana matatizo makubwa. Hadi sasa sijaelewa wenyeviti wa hizi kamati za bunge wanapatikana kwa kutumia vigezo gani? Serukamba ndiye alikuwa mpiga debe mkubwa kwa TPA ili wale watoa rushwa wa kimataifa CCCC wapewe kazi ya kujenga gati kwa 'usanii' wa mkopo nafuu toka EXIM BANK- China.

Pia Serukamba kama mwenyekiti wa kamati ya miundo mbinu ambayo inahusika pia na sekta ya mawasiliano sijamsikia akisema chochote kuhusu Vodacom ukwepaji wa kodi. Na hapa ndipo madai ya Mama Kilango yanaweza kutupa hisia kuwa Serukamba anasimamia maslahi ya watu fulani fulani.

Lakini kubwa kwangu ninaloona ni kuyumba kwa maadili kwa hizi kamati za bunge. Mbunge wa Bahi (CCM) ana kesi mahakamani, yuko mwenyekiti mwingine amepelekwa Japan na TBS ili awasafishe wakubwa wa TBS! Na week hii tunaambiwa ndugu Chenge kapata uenyekiti wa kamati ya fedha! Chenge alilazimika kujiuzulu kwa sababu wakubwa wake na wananchi pia walikosa 'confidence' kwamba ni mtu safi. Sasa waliomchagua wanapingana na wananchi?

Kwa kifupi, CCM wameonesha ujasiri wa hali ya juu wa kuziba masikio na kufumba macho. Wanakwenda kinyume na matakwa ya wananchi ambao ndio wenye mamlaka ya mwisho nchi hii. CCM wamepata wapi hiki kiburi?

RED: kwenye kura tulizowapa 2010. ndo mkome kuwachagua tena
 
  • Thanks
Reactions: FJM
these chaps are joking with us!! Wanacheza na kodi zetu, wanaenda kukaa dodoma miezi 3 wakilipana mamilioni wakirudi business as usual!Ifike mahali sisi wananchi tuamke tubane serikali na bunge tuhoji utendaji wao sio wanatuletea upuuzi kila siku tunawasikiliza tuu!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom