Anna Kilango achafua hali ya hewa kamati ya Miundombinu

Makupa

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
5,024
2,553
Kamati ya Miundo mbinu jana ilikumbwa na tafrani baada ya wajumbe wake kudaiwa kumshambulia kwa maneno makamu mwenyekiti wa kamati hiyo Anne Kilango wakidai amewasiliti.

Kwa mujibu wa taarifa ni kwamaba anna kilango alipeleka majungu kwa waandishi wa habari wa magazeti mawili kuwa serukamba ameagiza wasuse bajeti na kibaya zaidi alimpigia simu waziri mkuu saa 5 usiku akisema serukamaba mi mtu mbaya sana.

Alisema serukamba anatumiwa na Lowasa amezuiya tusipitishe bajaeti.

Taarifa zinabainisha zaidi kuwa wajumbe hao hawakufurahishwa na kitendo cha kilanago na kuanza kumshutumu kuwa mchochezi .

Chanzo: Habari leo tarehe 5/6/12
 
Hivi hizi kamati kweli zitzfanya kazi mwaka huu? Hiyo ya LAAC ndio hivyo mwenzao kakamatwa akiwachukulia advance ili wapitishe mahesabu ya Mkuranga, Miundo mbinu nao wameanza kufanyiana majungu
wananchi tutegemee lolote kwa kwa aina hiyo ya wabunge?
 
Wote wameshanichosha,hawana jipya...
Wanaongea sana likija swala la kusign, wote wanaingia mitini......
Ufike tu wakati tupate fursa ya kukung'uta carpet na kuchagua upya....
 
Nipo kwenye jimbo lake naona wanajitahidi kurejesha barabara iliyoharibiwa na mafuriko ila wanajenga makalavati kwa teknolijia ya 1947.
 
Huyu mama cjui kwa nini hakuna cku aliyowai kuongea nikamwamini! Ila alinikera sana kwenye kuchangia rasimu ya katiba anaongea utafikri anauchungu na nchi hii kumbe anapigia debe tumbo lake na la malecela! Mama nuksi huyu. Kipembele mbele tu hana chochote. Mbona hakusaini kitabu cha kutokua na iman na PM kama kweli ni mpiganaji?
 
Alishasema PATACHIMBIKA!!!!

anne-kilango-nae-akichamgia-suala-la-mafuta.jpg
 
Mama Kilango si mtu wa maana sana linapokuja swala la uongozi bora, lakini kwa hakika Serukamba ana matatizo makubwa. Hadi sasa sijaelewa wenyeviti wa hizi kamati za bunge wanapatikana kwa kutumia vigezo gani? Serukamba ndiye alikuwa mpiga debe mkubwa kwa TPA ili wale watoa rushwa wa kimataifa CCCC wapewe kazi ya kujenga gati kwa 'usanii' wa mkopo nafuu toka EXIM BANK- China.

Pia Serukamba kama mwenyekiti wa kamati ya miundo mbinu ambayo inahusika pia na sekta ya mawasiliano sijamsikia akisema chochote kuhusu Vodacom ukwepaji wa kodi. Na hapa ndipo madai ya Mama Kilango yanaweza kutupa hisia kuwa Serukamba anasimamia maslahi ya watu fulani fulani.

Lakini kubwa kwangu ninaloona ni kuyumba kwa maadili kwa hizi kamati za bunge. Mbunge wa Bahi (CCM) ana kesi mahakamani, yuko mwenyekiti mwingine amepelekwa Japan na TBS ili awasafishe wakubwa wa TBS! Na week hii tunaambiwa ndugu Chenge kapata uenyekiti wa kamati ya fedha! Chenge alilazimika kujiuzulu kwa sababu wakubwa wake na wananchi pia walikosa 'confidence' kwamba ni mtu safi. Sasa waliomchagua wanapingana na wananchi?

Kwa kifupi, CCM wameonesha ujasiri wa hali ya juu wa kuziba masikio na kufumba macho. Wanakwenda kinyume na matakwa ya wananchi ambao ndio wenye mamlaka ya mwisho nchi hii. CCM wamepata wapi hiki kiburi?
 
Maadili ya familia yoyote hujengwa na wazazi.

Kwa asilimia kubwa tabia za watoto huwakilisha tabia za wazazi...........Tafakali.

Pinda mwenyewe mlimsikia vurugu za arusha, kadanganya bunge na watanzania kwaujumla, Lema anatoa ushahidi kuthibisha uwongo wa Pinda, Speaker Anna makinda anakalia maelezo kwa ahadi za uwongo atazitoa kesho, kesho, hadi leo.... (Bunge)

Mheshimiwa sana Rais wa jamhuri J. M Kikwete, ahadi nyingi na orodha ni ndefu.......Meli Z. tanganyika...Meli Z. Victroria....Meli Z Nyasa... Mabarabara .... viwanja na kubwa kabisa sijui ataitekelezaje ni ya maisha bora kwa kila mtanzani..........(Serikali mhhhh)

Kwahiyo mama Ana kilango is just a reflection about the axis of the reflection (Government & parliament) haaihitaji kuumiza akili sana kushangaa anavovujisha siri na kukiumiza chama chake CCM na kamati anayoitumikia ya miundombinu.

Viongozi ndani ya mfumo wa serikari yetu wameparaganyika, hawana muundo, control wala maadili.

NIJANGA LA KITAIFA. Hamuoni? wanafanya kazi kwa kujali maslahi binafsi.
 
Mama Kilango si mtu wa maana sana linapokuja swala la uongozi bora, lakini kwa hakika Serukamba ana matatizo makubwa. Hadi sasa sijaelewa wenyeviti wa hizi kamati za bunge wanapatikana kwa kutumia vigezo gani? Serukamba ndiye alikuwa mpiga debe mkubwa kwa TPA ili wale watoa rushwa wa kimataifa CCCC wapewe kazi ya kujenga gati kwa 'usanii' wa mkopo nafuu toka EXIM BANK- China.

Pia Serukamba kama mwenyekiti wa kamati ya miundo mbinu ambayo inahusika pia na sekta ya mawasiliano sijamsikia akisema chochote kuhusu Vodacom ukwepaji wa kodi. Na hapa ndipo madai ya Mama Kilango yanaweza kutupa hisia kuwa Serukamba anasimamia maslahi ya watu fulani fulani.

Lakini kubwa kwangu ninaloona ni kuyumba kwa maadili kwa hizi kamati za bunge. Mbunge wa Bahi (CCM) ana kesi mahakamani, yuko mwenyekiti mwingine amepelekwa Japan na TBS ili awasafishe wakubwa wa TBS! Na week hii tunaambiwa ndugu Chenge kapata uenyekiti wa kamati ya fedha! Chenge alilazimika kujiuzulu kwa sababu wakubwa wake na wananchi pia walikosa 'confidence' kwamba ni mtu safi. Sasa waliomchagua wanapingana na wananchi?

Kwa kifupi, CCM wameonesha ujasiri wa hali ya juu wa kuziba masikio na kufumba macho. Wanakwenda kinyume na matakwa ya wananchi ambao ndio wenye mamlaka ya mwisho nchi hii. CCM wamepata wapi hiki kiburi?

Ni kweli Mkuu na pongezi za dhati ziende ka JJ Mnyika kwa kutuokoa katika hilo!
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Nadhani M4C imemchanganya!
Apewe msaada wa kisaikolojia!
Alichofanya si ishara ya uongozi bora hata kidogo.
Hatimaye, tunapima viongozi wetu si kwa sauti zao,si kwa makelele yao.
Tunawapima kwa matendo yao.
 
Hivi hizi kamati kweli zitzfanya kazi mwaka huu? Hiyo ya LAAC ndio hivyo mwenzao kakamatwa akiwachukulia advance ili wapitishe mahesabu ya Mkuranga, Miundo mbinu nao wameanza kufanyiana majungu
wananchi tutegemee lolote kwa kwa aina hiyo ya wabunge?

hazifanyi kaz na hazitafanya,,,,sababu kuu ni kwamba zinaundwa na wabunge haohao tunaowalaumu ambao kazi yao kuzomeana,,,,TUTAYASIKIA MENGI SANA WADAU
 
Back
Top Bottom