Anguko la taifa laja

Mtoto akililia wembe mpe, mwacheni yatakayomkuta atakuja simulia vijukuu vyake kama atatoka jela akiwa hai
 
Ndugu zangu wanawaJF na wasiyo kuwa wanawaJF ambao huwa wanapita humu kwakuperuziiii na kudadisi ASALAAM ALYKHUMUU.

Nimeamua kutoa mtazamo wangu juu ya anguko la TAIFA hili kwa kile ninachokiona kinavyoendelea kwasasa. nimesikitishwa sana na kauli zinazoendelea huku mitaani na maofisini juu ya nani awekiongozi wataifa hili na watu wengi *wa maofisi wamipongeza forum hii kuwa inauwezo wa kumpanga Rais wataifa hili kuliko taasisi yeyote ile ukilinganisha na wnzetu waliyoendelea huwa na taasisi maalum ya kumchagua Rais hata kama wananchi hamumtaki mtamchagua tu kwambinu wanazozitumia kwa ushawishi mkubwa wa hali ya juu.

Hapa kwetu Tanzania hamna mpango huwo ndiyo maana unasikia kila siku tunatengeneza kizazi cha kifisadi, kizazi cha kulipana kisasi na kizazi cha majigambo hili nianguko la taifa kwasasa. ila niendembali zaidi nipale ninapoendelea kusikia watu makini au forum makini kama hii pamoja na uhuru wa maoni au mawazo watu wanao takiwa kutoa eti na kufikiri kwetu kote TUNAWAZISHWA HUMU LOWASSA aje atawale taifa hili, kiukweli tunaanza kumjengea LOWASSA njia ya URAIS bila sisi kujijua kuwa ni watu muhimu sana katika kupanga na kupangua viongozi bora na wasiyo bora.

Naamini kauli hii wengi watanipinga na wengi wataniunga mkono: turudi nyuma uchaguzi uliyopita JF ilichangia kwakiasi kikubwa mno kumpata mgombea URAIS wa CDM na tuliona tulivyochangia kumpata mgombea makini mwenye uwezo mkubwa kuliko aliyeshinda sasa na hata huku AFRICA KUSINI tulipo forum hii inasifika sana kwa hilo. sasa iweje leo hii tuanze kupoteza malengo yetu kwakutaka kuwarudishia madaraka wezi wakuu wataifa hili? kama sikutaka kuliangamiza taifa kwa ushabiki usiyo na tija yeyote ile kwa mwananchi wa kijijini asiyejua kinachoendelea kwasasa ?

Hofu *hii nimeipata leo kupitia humu humu JF nasikia LOWASSA leo alikuwa anachangia hutuba ya waziri mkuu wengi mmemsifu badala ya kuendelea kumkataa kwa maovu yake aliyoyafanyia taifa mmeanza kusahau na wengine kumuonea hata na huruma. hili niaanguko la taifa na JF mtahusika na hukumu hii pamoja na mimi kwa kuwa ni member humu.

HITIMISHO
Tuanndaeni viongozi makini kwa faida ya dada zetu mama zetu watoto wetu waliyopo vijijini ambao nawao siku moja wanatamani kuliongoza taifa hili na anaweza kuwa viongozi bora kuliko kizazi chtu cha sasa. haya ni maoni yangu na wewe unaweza fikri zaidi yangu kwa kulisaidia taifa. MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI JF......

Ninashangaa watu wanasumbua vichwa vyao kwa ajili ya Lowasa wakati wake umesha pita. Akasome historia ya mussolini wa Italia, Italia ilipomshinda walimfanya nini, walimkimbiza kama paka na kumkabidhi kwa watu wake wanaomtaka awawakilishe huko. Ninadhani humu Jf wanaompijia debe ni watoto wake wanasumbua vichwa vya watu wakati watu wanalala njaa, hakuna umeme, wao wanasikia raha wanaposikia baba yao kaenda kazi akirudi mfuko imejaa, lakini sisi tukienda tunashinda kijiweni mpaka jioni tunasubiri umeme ndio watoto watu waweze kusema pole baba. Haina haja ya kujibu thread zake zivunde mpaka ziondoke zenyewe. Wataandika kama watu hawatachangia hawataandika tena kwa sababu wataona wanapoteza muda.
 
Bora EL arudi tu! Kuliko kuwa na administration hopeless kama hii ya JK ambayo haina maamuzi hauijui kipi inasimamia...tuna PM kama hatuma ... ali mradi kila mtu ana sauti.
 
Back
Top Bottom