Anguko la CHADEMA sasa ni dhahiri

Makupa

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
4,995
2,527
Nilifuatilia kwa makini kabisa bunge lililopita, nilichogundua ni kwamba wabunge wa cdm walioanzisha swala la kuiwajibisha serikali ni halima mdee na Tindu Lissu.

Kwa mshangao wa wengi mbunge Zitto Kabwe aliteka mawazo ya hao wabunge wawili na kunukuliwa akisema swala la kuiwajibisha serikali lilikuwa ni la kwake, kwa lugha nyepesi tu utagundua ya kwamba cdm hawako pamoja kama chama ila ni mkusanyiko wa wanaharakati wenye malengo binafsi.
 
kwa mshangao wa wengi mbunge Zitto Kabwe aliteka mawazo ya hao wabunge wawili na kunukuliwa akisema swala la kuiwajibisha serikali lilikuwa ni la kwake...

Haya ndio mambo yanayofanya mtukanwe hapa jamvini. Utumbo bila uthibitisho, alinukuliwa wapi na lini akisema hivyo? Nukuu zote zilizoziona anasema hili ni jambo la kitaifa na ni zaidi ya chama. Haya yako ameyasema lini na wapi?
 
Ndugu yangu Makupa hivyo visenti unavyopata kutoka kwa wakina Nape kusambaratisha Chama kubwa zitakutokea puani kila mtu ana njaa lakini ya kwako imekithiri kweli nimeamini wewe ni mangi meza
 
Nilifuatilia kwa makini kabisa bunge lililopita ,nilichogundua ni kwamba wabunge wa cdm walioanzisha swala la kuiwajibisha serikali ni halima mdee na Tindu Lissu, kwa mshangao wa wengi mbunge Zitto Kabwe aliteka mawazo ya hao wabunge wawili na kunukuliwa akisema swala la kuiwajibisha serikali lilikuwa ni la kwake, kwa lugha nyepesi tu utagundua ya kwamba cdm hawako pamoja kama chama ila ni mkusanyiko wa wanaharakati wenye malengo binafsi.

Nakubaliana na wewe, hapa mtaani kwetu mwenyekiti wa tawi la CDM na Katibu wake usiku wa jana wameshikana mashati; kweli hiki chama ni uvunjaji wa amani tu
 
SITHANI KAMA ULIYOTE HII MADA UNAAKILI TIMAMU, NA HAKUNA THAMBI KUBWA KAMA KUWA UPANDE WA WATENDA MAOVU...kwa kupotosha haki,kuwaibia walala hoi NK...
 
kwa hiyo anguko hapa liko wapi? Cha msingi ni kwa hoja imefanikiwa na viongozi watawajibishwa hivi karibuni.
 
Kumbe ni kweli common sense is not always common. CDM leardership is not a homogeneous lot, ni watu wenye common vision na mission; lakini kila mmoja anafikiri independently and that synergy of independent thought process ndiyo inayozaa Kimbunga unachokiona kinaipeperusha MAGAMBA mpaka hawaelewi what is hitting them.

wewe unataka CDM ifanye kazi kama JK anayeshindwa kutumia executive authority yake kama Rais kuwawajibisha mawaziri na watendaji wahuni wachache mpaka aitishe CC ya magamba, uko wapi wewe? faculties zako umezimpeleka sabbatical leave?!
 
Ndugu yangu Makupa hivyo visenti unavyopata kutoka kwa wakina Nape kusambaratisha Chama kubwa zitakutokea puani kila mtu ana njaa lakini ya kwako imekithiri kweli nimeamini wewe ni mangi meza

Mkuu siku zote ukweli unauma, mkuu sio siri hata huyo Nape hanijui sijatumwa na mtu yoyote yule bali nimeamua kuwasilisha ninachoona ni dhahiri.
 
Shida kubwa ya Watanzania ni kukosa uzalendo tu. Unawezaje kushangilia kuanguka kwa CDM wakati wanakusaidia mambo yako yaende vizuri?
 
Pamoja na huu upuuzi wako hapa anguko liko wapi sasa au kuna kuwashwa na jinsi cdm kinavyopiga siasa zake?
 
Kuna watu wanalalamika kwamba sisi tunawatusi, em sema na wewe kwa uzi kama huu unategemea michango gani toka kwangu, Ni wapi Zitto aliposema kwamba hii ni hoja yake binafsi, siku zote amesema hii ni zaidi ya hoja ya CHADEMA, ni hoja ya kitaifa kwa ajili ya wanyonge.

Leo mtu anakuja kupotosha kiasi kama hiki! Af et kwa hili tu ndiyo iwe proof ya anguko la CHADEMA, Yaani udini, ukanda ulishindwa leo ije hili la sahihi 70
 
Sina hakika kama thread hii ni ya kipumbavu au mtoaji mwenyewe!
 
nakubaliana na wewe, hapa mtaani kwetu mwenyekiti wa tawi la cdm na katibu wake usiku wa jana wameshikana mashati; kweli hiki chama ni uvunjaji wa amani tu
mafilili kwa hili unaarisha kwa kutumia mdomo jamani, waongelea katibu wa tawi wa cdm kushikana mashati, hujui kuwa waziri omar nundu na naibu wake wameshikana mashati tena hadharani? Hujui kuwa jk na fisadi lowasa hawaelewani? Hujui kuwa samwel sita na el hawaelewani? Duh fahamu mafisadi hawabebeki
 
Back
Top Bottom