angina (maumivu yatokanayo na ugonjwa wa moyo)

vicent tibaijuka

JF-Expert Member
Mar 22, 2012
268
57
habarini wana JF, ni muda mwingi nimekaa hapa nakusoma maswali mengi humu, mimi leo napenda kuandika au kuelimisha watz wenzangu kidogo kuhushu kiasi fulani moyo na nini cha kufanya kinapokutokea au jirani yako au rafiki ayko na hata katika familia yako.
mara nyingi watu wamekuwa wakipatata wakilalamika kuwa wanapata maumivu makali upande wa kushoto wa kifua na maumivu hayo huenda mapaka shavuni,shingoni, mkonno wa kushoto na hata mpaka mgongoni. mtu aliye na dalili hizo BASI jua ana matatizo ya moyo na ugonjwa huo huitwa angina pectoris. ugonjwa huu husababishwa hasa nakupunguwa kwa ujazo wa mishipa ya moyo na hivyo kuufanya moyo wenyewe usiweze kupata damu ya kutosha na kusababisha hewa ya oksijeni kupungua katika minofu ya moyo (myocard). tatizo hili la mishipa hutokana na kula mafuta mengi hasa ya wanyama (hatari kiti moto), mafuta ya nazi au pamba, kula wanga nyingi (bia) (kwani hubaDILISHWA MWILINI NA KUHIFADHIWA KAMA MAFUTA). kuvuta sigara, kutofanya mazoezi, kuwa na wasiwasi mara kwa mara (stress) au shinikizo la damu (BP).
ugonjwa huu umegawanyika katika sehemu tatu.
1: ni maumivu mtu hayapatayo wakati anafanya kazi ngumu au anatembea zaidi ya mita 100. haya hutokana na moyo kuongezeka kufanya kazi lakini damu yenye okisejen haitoshi
2: maumivu yaokeayo wakati wa kutembea chini ya mita 100 au kufanya kazi kidogo tu, au kupanda ngazi ghorofani .
3: maumivu yatokeayo wakati mtu amekaa au amepumzika tu.
kama ukiwa na na maumivu haya jaribu kuacha shughuli zote unazofanya ka kupumzika. kama uko ndani fungua madirisha ya nyumba ili upate hewa ya kutosha. siku zote tembea na vidonge vya nitroglycerin kwa ajiri ya kuondoa maumivu hayo yanapotokea.
ugonjwa huu huweza tibika kwa kiasi fulani kwa kubadili tabia zetu mfano kuacha kunywa pombe (ingawaje ml50) za pombe kali au glass ya dry wine (mvinyo mkavu) hupunguza tatizo hili, kutokula mafuta mengi au kula wakti unaotakiwa. kuacha kuvuta sigara, kutembea kwa kasi angalau nusu saa hadi saa 1 mara tatu kwa wiki au kila siku inasaidi. kumeza 1/8 (nusu ya robo kidonge) cha aspirin mara moja kila siku baada chakula (angalia kama una vidonda vya tumbo). kutibu BP.
kwa wale wanaopata maumivu wakti wamepumzika hubidi kufanyiwa aina ya pertion iitwayo angiography bahati nzuri itaanza muhimbili mwezi wa december (hufanyika kwa nusu saa tu).
zingatia hayo na linda afya yako.
 
Asante mkuu kwa maelezo mazuri,mi nilienda kucheki moyo muhi2 nikakutwa na tatizo linaitwa MVP,cjui linamahusiano na kitu unachokizungumza?
 
mitral valve prolapse haihusiani na hilo, ila inaweza kusababisha mapigo ya moyo kuwa yanabadilika badilika (arrythymias). na yenyewe imegawanyika katika semu tatu. sehemu ya kwanza hna ya pili haina madhara na sehemu ya tatu ina madhara kwani huweza kufanya moyo kupanuka na kufanya moyo usiweze fanya kazi vizuru (cardiac failure). na dalili zake ni kuchoka haraka wakti wa unafanya kazi
 
mitral valve prolspse haihusiani na hilo, ila inaweza kusababisha mapigo ya moyo kuwa yanabadilika badilika (arrythymias). na yenyewe imegawanyika katika semu tatu. sehemu ya kwanza hna ya pili haina madhara na sehemu ya tatu ina madhara kwani huweza kufanya moyo kupanuka na kufanya moyo usiweze fanya kazi vizuru (cardiac failure). na dalili zake ni kuchoka haraka wakti wa unafanya kazi

oky asante mkuu
 
Mkuu nahisi nina hili tatizo kutokana na dalili ninazopata, sijui wapi nianzie!! Naomba kusaidiwa tafadhali

Back
Top Bottom