sikiolakufa
JF-Expert Member
- Feb 1, 2010
- 411
- 54
Napenda kuchukua fursa hii kutoa angalizo wa wananchi wanaoenda ufukwe wa coco beach kwa mapumziko. kuna kundi la askari wa jeshi la polisi ambao wamekuwa wakifanya vitendo vya kiharifu na unyanyasaji kwa wananchi wanaoenda kupunga upepo pale. Taarifa zinasema kwamba mara kwa mara raia wema wamekuwa wakivamiwa na askari hao na kutolewa nje ya magari yao wakituhumiwa kufanya mapenzi ndani ya gari. Askari hao wamekuwa wakiondoka na watu wanaowatuhumu kufanya mapenzi na kuwatishia kwamba watawapeleka mahakamani kama hawatatoa kitu kidogo( rushwa). Watu wengi niliobahatika kuongea nao ni wahanga wa kadhia hii. Askari hao huwa wanashirikiana na vijana wenye pikipiki ambao huvizia wananchi hao na kuwapora pesa. Je hivi kuwa ndani ya gari ni kosa? mimi ninavyofahamu kisheria kuna kosa linaloitwa indecent exposure lakini kama mtu uko faraghani na mwezio hilo ni kosa? Je hao askari polisi ambao hutembea na gari aina ya starlet....ina rangi damu ya mzee na nyeusi kwa nini wanafanya unyanyasaji huo? kwa nini wanaacha kukamata majizi makubwa kama EL na RA na wananyanyasa wananchi maskini? Kova kazi itakushinda sasa