ANGALIZO PEKEE: Kwa Viongozi na Wabunge wenye kuikandia JF kiaina

Sentensi ya kwanza umeiandika kama wewe ndiye mmiliki wa JF. Si uwaache wenye mtandao wao waongee?

Jamii Forums ni sauti ya umma na wewe unahusika moja kwa moja ndio maana uko huru katika kuchangia au kuleta uzi wako hapa. JF haingesimama bila yule, wale, wewe na mimi, sisi ndio tunaofanya JF iwepo na ndio malengo ya Mwanzilishi.

Mwanakijiji yuko sahihi kwa alivyoandika.
 
Nahisi mimi nina matatizo kwa kweli.....

yaani kuna 'VIONGOZI ' wenye akli timamu wanaona 'ni bora nchii ikawa na watu wenye mawazo'

kama ya Juma Nkamia...na kuwa serious kabisa na nia ya kuifuta JF....???????


hii nchi iko 'upside down' kwa kweli......

Labda now kilichobaki ni muujiza utokee ili 'upumbavu huu' usipate nafasi.....
 
Umenena vema mzee mwanakijiji, hizo kelele ni za mafisadi zipuuze
wanatamani JF ingekuwa gazeti walifungie kama walivyofanya kwa gazeti la mwanahalisi.
 
mwakyembe alikandia lakini baadae taarifa zikawekwa humu na kuwa alichosema ni uongo

leo membe nae amekandia lakini pia alikuwa wrong maana taarifa ile ilianzia gazeti la the guardian na ipo huko hadi dakika hii

yule afisa afya kule bukoba nae alisema uongo kuwa hakuna mgonjwa wa ebola lakini ukweli ukabaki kuwa wazi kuwa kijana yupo na anaangaliwa na sasa vipimo vimepelekwa dar kwa uchunguzi zaidi

mchungaji lwakatare alioma jf ifungiwe maana inachafua watu kumbe yeye mwenyewe ni mwizi wa umeme mkubwa na kuwa na yote haya yalianikwa humu jf

yule jamaa mzinzi (nkamia Juma) nae aliponda jf juz bungeni na kuuliza nani mmili..lakini waziri alimjibu vizuri tu kuwa mtandao hauwezi kufungiwa


kimsingi hawawezi huu ni moto mwingine wajaribu kufunga waone...naona wanaanza kutafuta sababu taratibu
 
Ngoja nitambae kwani Radhia sweety ananitafutia ubaya nimetoka lockup juzi

Tusipoteze lengo la mada na kumshambulia mtu aliye kosa uustarabu. Lamuhimu wanajamvi tulete mada zenye ukweli ili keundelea kulinda sifa ya JF. Let it always remain the home of Great Thinker
 
Sentensi ya kwanza umeiandika kama wewe ndiye mmiliki wa JF. Si uwaache wenye mtandao wao waongee?

kuna wimbo ametunga msanii 20% unaitwa '' INAUMA'' ule wimbo una mistari ya maana na kuna mahali wimbo unaisifia chadema dhahiri dhairi..wewe katika coment zako ukasemayule jamaa ni marijuana...wengi walikudharau sana...leo tena unakuja na hili

BTW unamfahamu mwanakijiji au unaropoka tu?
 
Mkuu MMM,

Wacha waendelee kutoa tuhuma dhidi ya JF, lakini bila ya wao kujua wanazidi kuipa JF umaarufu zaidi na zaidi.
 
Kwani wewe inakuhusu nini? Kama hujisikii kuwa mmiliki wa JF basi wewe ni miungoni mwa wanaoichukia. Kila mpenda mabadiliko ni mmiliki wa JF. Na kila fisadi anayeichukia JF huyo sio mmiliki, kama wewe.

Yaani Umeongea ukweli 100%.... JF, DAIMA MBELE, WOGA MWIKO..
 
Taifa linahitaji watu kama kumi tu hivi wenye weledi na mihemko ya kimang'amuzi ya kima cha juu kuweza kurikabili kundi mufili lenye watz wasiozidi 50

Na kati ya hao wazalendo kumi Mwanakijiji ni mmoja wao!

Mwanakijiji ni chemchemi ya fikra huru zinazojipambanua ktk ardhi ya Tanzania zenye sura ya Tanzania mpya!

Nakubaliana na wewe kwa asilimia miamoja kabisa!
 
We ulionawapi moto unazimwa na petrol MMM. Don't give up twende zetu kwenye kilele cha ukombozi.
 
......Nimemshangaa sana Mh.MEMBE pale katika uwasilishaji wa hotuba ya bajeti yake eti' jf, wamepotosha umma suala la rada..... Huu ni unafiki wa maGAMBa na govT YAO DhaiFU!!
 
WanaJF, humu ndani kuna watu wengi sana na hata waliopo serikalini baadhi yao ni wanaJF mhimu sana kwani wanatoa taarifa zinazosaidia JF iwe hapa ilipo.

Alichoongea mwanakijiji kama nimemuelewa vizuri ni kuwataka ndugu zetu walioko serilkalini watimize wajibu wao na watumie muda mwingi kuona ni namna gani wanaweza kuboresha huduma zao kwa umma na kufanya nchi yetu isonge mbele. Na pili akawaomba kuwa waendelee na yao na sio kuanza kupoteza muda wa kupanga mbinu za kutaka kuidhuru JF. Hii ni hoja nzuri na sio kitu kigeni sana, amewakumbusha.

2. Ukiangalia uhusiano uliopo sasa miongoni mwa watendaji na watawala wa serikali ya sasa utagundua kuwa kuna uadui mkubwa na hata Mh. Rais kuna mahali alikili hili. Kuwepo kwa uadui miongoni mwao inakula kwetu wananchi maana badala ya kufanya kazi wao wanatumia muda wetu mwingi kufikiria namna ya kumkomoa au kumdhulu fulani. Hii inakuwa ni vita ya fahari tuumia ni sisi wananchi tunaoibiwa sio tu maaliasili bali hata muda wa kutuhudumia.

Naamini ndugu zangu mliopo serikalini mtakaosoma maoni yangu, jaribuni kuzingatia majukumu yenu achaneni na mawazo duni ya kufungia JF na vyombo vingine vya habari maana matatizo na mitazamo tofauti ipo vichwani mwa watu na siyo kwenye vyombo vya habari.

Nawatakia kila la kheri na long live JF
 
mmmh, tuChukue Chetu Mapema hapa jf??

Naombeni chit chat mtanikabidhi.

Hawawezi kuifunga kirahisi hivi.
 
Uzoefu unaonyesha kuwa wanaoiponda Jf wote wanaishia kuadhirika, na kwa bahati mbaya wakisharopoka wadau wanamwaga data hapa na wao wanakosa mahala pa kukanushia, na kila kitu hubaki mtandaoni kuwa aibu yao milele.

Mama Rwakatare alichezwa na wadau hapa na hajarudia tena kubwatuka, na bunge lenyewe likammaliza kwa kuweka hadharani kuwa anaiba umeme wa Tanesco.

Ukiona mtu anaikandia JF kuna mawili;aidha ni fisadi au ni mpumbavu, kwisha.
 
Ukiangalia jitihada zao dhidi ya JF, utagundua kuwa uovu wao umewasababishia upofu wa ajabu. Wanawezaje kujitia ulimbukeni na kujidanganya kuwa wataweza kuwanyamazisha mamilioni ya wabongo ambao wameamka, wako huru na hawadanganyiki kwa namna yoyote ile...?!
 
Mimi huwa nadhani Radhia Sweety ni huyu mama wa UWT ambaye kwasasa yuko kwenye malumbano makali na Anne Kilango Malecela kugombea Uenyekiti wa kundi hilo.

Samahani kama nimewakwaza lakini.
 
Last edited by a moderator:
JF Ni jukwaa huru na yeyote aliye humu na msomaji wa JF ni mmiliki wa JF hata kama hao munao waita wamilini ni viongozi na ni watu wakuufanya huu mtandao uweze kuwepo na kuendelea kuwepo, kama ilivyo TZ ni mali ya watanzania ila kunaviongozi wanaoiona ni mali yao peke yao.

Watafanya jitihada zote za kuifunga hata kawa watafanikiwa nikwamba litaibuka jingine, kadiri unavyombana mwizi unamuongezea akili ya kuvumbua njia nyingine ya kukuibia. Kumpiga chura teke ni kumuongezea speed.
 
Ni lazima ndugu zangu mtambue kuwa siyo wote wanaotumia JamiiForums wanapenda pia iendelee kuwepo. Tawala zote zilizoshindwa duniani hutumia nguvu nyingi sana kukandamiza (suppress) uhuru wa mawazo. Hii ni kwa sababu ni vigumu sana kuwatawala watu vibaya kama watu hao wameamka na wanaweza kufikiri na kubadilishana mawazo. Mchango mkubwa wa JamiiForums - kwa maoni yangu - hauko kwenye kufichua ufisadi au kuwaleta watu wengi pamoja; naamini upo katika kufungua fikra za wananchi wetu na kuwakaribisha kubadilishana mawazo juu ya mambo mbalimbali yanayohusu mustakabali wa taifa letu.

Hakuna kitu kinachowatisha watawala wabovu kama watu wenye kuweza kufikiri na kubadilishana mawazo. Ndio maana hawatocheleaw kupiga marufuku mikutano, maandamano, vitabu, magazeti na wangekuwa na uwezo hata watu kuzungumza wao kwa wao!
 
Back
Top Bottom