ANGALIZO PEKEE: Kwa Viongozi na Wabunge wenye kuikandia JF kiaina

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,461
39,928
Kimya chetu si woga au kuwaonea haya au heshima ya pekee. Kutowajibu kwa namna tunayoweza siyo kwamba mna ujiko wenye kututisha. Kwa wiki kadhaa sasa kuna wabunge na viongozi wa serikali ambao wameanza kurusha mashambulizi ya kiana yenye lengo la kubeza nafasi ya mtandao huu wa JF katika kupambana na mafisadi waliokubuhu na vile vile wakijaribu kutengeneza mazingira ambayo yatafanya mtandao huu ukome kuwa sauti huru zaidi ya Watanzania kuhusu nchi yao.

Ninafahamu baadhi ya viongozi hawa waliapa na kudhamiria kuwa hawawezi kwenda kwenye uchaguzi mkuu ujao wa 2015 na mazingira kama yaliyokuwepo 2010 na hasa kukua na kukomaa kwa mtandao wa JamiiForums. Ninafahamu - kwa uhakika wa kutosha tu - kunatafutwa "zengwe" la kusababisha mtandao huu ufungwe au uongozi wake upatwe na matatizo kiasi cha kushindwa kuendesha. Hofu hii inatokana na ukweli kuwa mtandao huu yawezekana unawafikia watu wengi zaidi kila siku ya wiki kuliko magazeti na una kina zaidi kuliko Televisheni na Radio (vyombo vyote hivyo haviwezi kufikia uwezo wa mtandao wa JF au wa kiintaneti).

Sasa hii hofu yao kuwa JF ilitoa mchango wa kipekee katika kuhamasisha wapinzani na hata kuchochea fikra za mabadiliko hasa kwa watu ndani ya serikali ni hofu inayoeleweka na inaweza kukadiriwa. Sasa badala ya wao kutengeneza madudu yao wanafikiria namna ya kunyamazisha watu wenye kuonesha madudu hayo au hata kuzima sehemu ambapo watu wanaonesha madudu hayo. Wanataka JF ionekane haiwezi kuaminika (not credible). Kuanzia baada ya uchaguzi mkuu wa 2010 baadhi yetu tumeweza kuona jinsi taarifa mbalimbali zenye utata zikipandikizwa kiaiana ili kufanya JF ipoteze credibility na wakati huo huo kutengeneza mazingira ya kisheria ya kuweza kuchukuliwa hatua.

Sasa naomba nitoe angalizo pekee: Tutaendelea kuwa sauti huru zaidi ya Watanzania (nyumbani na nje); tutaendelea kusimamia haki ya msingi ya mawazo na maoni ambayo raia wetu wote wanao na kuendelea kufunua yale ambayo serikali na watendaji wa serikali wasingependa wananchi wajue ili wasije kufunguliwa na kubadilisha mawazo. Tutakaposikia wabunge au viongozi wengine wanaanza kukandia JF au kuchukua hatua za kujaribu kunyamazisha mtandao huu kama walivyojaribu ile Februari 2008 tujawajibu.

Kinachoudhi sana ni kuwa baadhi ya wenye kuendesha na kupanga mambo haya ni wale waitwao "wanasiasa vijana"!

Tutawajibu kwa namna ambayo Wikileaks itaonekana ni cha mtoto.

Watawala fanyeni kazi zenu, viongozi ongozeni na sisi mtuache tuache kufanya ya kwetu - kuwaangalia msije kuuza taifa letu zaidi ya ambavyo tayari mmeliuza. Tayari kuna mtandao mkubwa ambao umekamilika kuweza kuonesha ufisadi uliokubuhu karibu kwenye wizara, idara na vitengo vyote.

DON'T UNDERESTIMATE THE POWER OF A FREE PEOPLE!

Kwa kadiri ya kwamba bado tuko huru tutaendelea kuwakazia macho...
"Those within the hierarchy are ready to support whatever attitudes sustain hierarchy. The functionaries within the hierarchy are not likely to listen to voices that challenge their position or place within the hierarchy.

Whenever the hierarchy is questioned there is a kind of primitive tribal response defending the status quo and attacking the challenges that arise. Yet those who confront the beliefs and practices of the hierarchy are often the ones most needed to correct its hidden distortions and bias. Whistle-blowers offer a corrective for what is not working systematically."


"The higher one goes in hierarchy the more closed one is--not only more blind but more unaware of the blindness. They are not able to hear other voices and yearnings, however legitimate."
– Quoted FROM PASCHAL BAUTE 1995


Jamiiforums is a legitimate voice of the people, our leaders should take comments and information from this forum seriously with intellectual eyes rather than offending it.
 
Sentensi ya kwanza umeiandika kama wewe ndiye mmiliki wa JF. Si uwaache wenye mtandao wao waongee?
 
Sentensi ya kwanza umeiandika kama wewe ndiye mmiliki wa JF. Si uwaache wenye mtandao wao waongee?

wewe dada yangu wa BAVICHA nakuheshimu sana, so hata kama unamachungu yako binafsi basi hapa si mahala pake, kwani MMJ anaeleza maMbo ya busara kabisa lakini wachache kama nyie ambao mmekuwa mkiumbuliwa na JF mnaona bora 2 mpoteze content nzima ya ujumbe huu.

THINK BIG.
 
Vya kunyamazisha viko vingi. Magazeti zalendo na huru, mitandao huru km jf, vyama vya wafanyakz km vya madaktari, radio na tv, vyama vya siasa pinzani kwa sasa cdm, wapinzani ndani ya ccm... orodha ni ndefuu. Hawawezi kuzima mawimbi ya fikra zinazobadilika. It's too late to 'catch the moving train'
 
Haki siku zote husimama! Na batili huanguka japo utapita muda! Let we see the time will tell!! Jf daima!
 
Jamani muacheni radhia wangu! sasa twendeni kwenye hoja, tuwafanye nini hawa viongozi wanao chakachua jf yetu wakidhani nayo inamikataba! ili waanze kujamba songosongo!
 
Nadhani ni wakati wa viongozi wa hii nchi kutambua kuwa tumechoka tunataka nchi yetu. Hatutaki vitisho visivyo na msingi wala tija, sisi sio wagomvi wala wahuni, ni watanzania wazelendo tuliosoma na kukulia Tanzania na wengine tunafanya kazi kwenye sekta mbalimbali za kujenga Taifa hili...Kutunyima uhuru wa kupeana habari hata kama zinawauzi na kuwakera sio haki, mmelifungia gazeti la mwanahalisi kwasababu ya kuficha uharamia na ujangili wenu, leo mnajifanya kutaka kunyemelea JF..tunasema hii sio haki na haikubaliki. Tunasema JF tulianza na MUNGU, tunaendelea na MUNGU, na itamaliza na MUNGU...

Mungu ibariki Tanzania, Mungu Ibariki JF, Mungu ibariki CHADEMA.
 
Wafunge kwanza Radio Imaan na Uhuru fm,GAZETI LA UHURU,ANNUR na Tazama..yanahatarisha usalama wetu.

siungani na wewe! kwa ivyo vyombo vya habari vyenye read! labda waifungie tumaini fm mana inahatarisha usalama wetu!
 
26 Reactions
Reply
Back
Top Bottom