Angalizo kwa wana JF - Lugha ya matumizi ya nguvu haina nafasi

Status
Not open for further replies.
NAUNGA MKONO HOJA MWANAKIJIJI -BUT ili mabadiliko yafanyike hisia kali na ukweli lazima ziruhusiwe, ccm ndio mchezo wao wamezoea kuchakachua walianza siku nyingi -lazima tuwaambie ukweli kupitia JF. Tunataka Tume huru ya Uchaguzi na siyo Tume ya CCM, tunataka tume inayojali maslahi ya watanzania wengi, kwani mbona Ivory Cost wanatume bomba inashindikana vipi TZ, ni kwa kusema ukweli na kuandamana ndio watajua hiki ni kizazi kipya, TUME IVUNJWE HATUITAKI IMESHINDINDWA KAZI ILIYOPEWA KIKATIBA.
 
Every war has its casualities, hakuna mapinduzi ya kweli yanayoletwa kwa propaganda za maneno (kama unavyoita nguvu ya hoja) tukubali tuu, tutaendelea kukaa hapa mbele ya monitors miaka na miaka mambo yatakuwa yale yale Mwanakijiji, mifano michache ya nchi zilizokombolewa kutoka unyonyaji ni Marekani (kutoka England), Kenya (now they have a new constitution), Iran ( King Shah) and so many, na zote hizi nguvu za hoja hazikuleta mabadiliko mpaka watu walipoingia mitaani. Watanzania hatujawa tayari, tutakapokuwa tayari matumizi ya nguvu ( physical confrotation) hataepukika Mzee, trust me.
 
Kweli kaka...ki ubinadamu haya yaliyojitokeza kwenye uchaguzi yametia vidonda katika mioyo ya wengi...ila nakubalina nawe kuwa kuna haja kutafuta namna ya kuzizinga hasira zisizae chuki...nina imani kuwa kwa kutumia hekima, busara na nguvu ya hoja mtanzania atakombelewa tu...
 
Wewe nakuelewa lakini mwanakijiji kuna mahali hatutakubaliana na nakubali kutokubaliana na mwanakijiji. Bila kutumia nguvu hatutavuka. Ni nguvu za kiasi gani hapo ndipo kuna hoja. Lakini mazungumzo ya kwenye keyboard hayatatuvusha tusidanganyane!
 
Mkuu I support you 100%.

Kuna wakati nimekuwa nikijiuliza hivi kweli JF ni HOME OF GREAT THINKERS au la. Kuna mambo kadhaa ambayo yameanza ku-dilute nguvu ya hii forum ntatoa machache.

1. Kutokubali mawazo m-badala.
Kuna tabia inayokuwa ya wachangaiaji wengi kuamini yoyote mwenye mawazo tofauti na yako basi yuko katika njia potofu. kwangu hili ni kosa maana lengo moja la forum hii ni watu kutoa mawazo yao kwa uwazi (pasi kuvunja sheria). Hivyo basi ili uweze kujipima usahihi wa mawazo yako mawazo tofauti na yako ni muhimu ili kuona kama kuna eneo ambalo umelisahau katika kujenga hoja ambalo linaweza kukupa mwelekeo mzuri zaidi.

2. Kushambulia watu zaidi kuliko hoja

Mara kadhaa tunasahau hoja na kumchambua mtoa hoja. Hii pia inapunguza umaarufu wa forum.

3. Kauli za jazba, vitisho na hata matusi
Busara za mtu huanza kupimwa kwa kauli zake maana matendo hujitokeza baadae baada ya kumjua mtu husika. Mtu mwenye natusi huonyesha upungufu wa busara.

My opinion:

JF inapaswa iwe chungu cha kupika hoja ambazo zinaweza kutumiwa na mtu yoyote ikiwemo wawakilishi na viongozi wetu katika kusukuma mbele Taifa letu.

Mgongano wa mawazo ni sharti la kwanza katika kujenga jamii imara. Lazima tujenge utamaduni wa kusikilizana. jamii lenye mawazo yanayofanana ni jamii mgando.

Naomba kuwakilisha

Well said mkuu!
 
Kuanzisha forum hiyo inawezekana kila siku, lakini kuwa na forum ambayo ni jicho la jamii si kitu rahisi. Hatuhitaji mtu aipende JF lakini pia si vema watu kuvuka mipaka. Kumbuka uhuru wa mtu huishia pale wa mwenzake unapoanzia.
Nguruvi3, Umenijibu baadhi ya hoja mkuu lakini kwa hili unasemaje? "Kuna post nimeuliza swali kwamba ikiwa hamjaona hatari iliyonayo JF kwa kuweka wazi nyaraka za siri za serikali! hatari nyingine kubwa itakuwa ni ipi?" Maana tusiishie tu kusema uhuru wako unaishia pale wa serikali unapoanzia wakati umechakachua uhuru wa mwenzio kwa kuingilia siri zake na kuziweka public.SAWA?
 
Swali la msingi KAA LA MOTO.

Msimamo wangu ni kwamba, Hoja ya Nguvu, ni jambo la lazima na lisiloepukika, kwa sababu ni upande wa pili wa Nguvu ya hoja.
Kuwaandaa Watanzania kukataa Amri zisizo za kisheria ni moja kati ya mambo ya Awali kabisa yenye kujenga Msingi wa Hoja ya Nguvu.
Nguvu ya hoja itangulie ikisindikizwa na Hoja ya Nguvu. Hiyo ndiyo lugha sahihi ambayo CCM wataielewa hakuna Polisi, FFU.UWT na hata JWTZ wawwezao kupingana na Hoja ya Nguvu ya wananchi.
Kiongozi na mwasisi wa South Afrika NELSON MANDELA alianzisha Military wing ya ANC ambayo hatimaye ilimpeleka Jela na kuwapa taabu sana Makaburu. Sisi hapa tunadeal na Makaburu Weusi ambao tumesha penetrate ngome yao kwa sana. Tutatumia Nguvu ya Hoja lakini wakae wakijua kwamba Hoja ya Nguvu haichezi mbali.

Ndiyo maana somo la Siasa ya CCM High Schoo nilipata F lakini nikiwa chuo niliandika Misonge ya nguvu sana.
 
Mkuu MKJJ,

Toka kuanza na kufa kwa CCJ, harakati zote zilizopita, hadi hivi leo!! Bado sijawahi kukuelewa!!!:doh:
 
Every war has its casualities, hakuna mapinduzi ya kweli yanayoletwa kwa propaganda za maneno (kama unavyoita nguvu ya hoja) tukubali tuu, tutaendelea kukaa hapa mbele ya monitors miaka na miaka mambo yatakuwa yale yale Mwanakijiji, mifano michache ya nchi zilizokombolewa kutoka unyonyaji ni Marekani (kutoka England), Kenya (now they have a new constitution), Iran ( King Shah) and so many, na zote hizi nguvu za hoja hazikuleta mabadiliko mpaka watu walipoingia mitaani. Watanzania hatujawa tayari, tutakapokuwa tayari matumizi ya nguvu ( physical confrotation) hataepukika Mzee, trust me.
Na usisahau kwamba kwingi ambako nguvu za kuondoa serikali zimetumika hakujafanikiwa mf. Somalia, Sudan, Uganda, Chad, Chechnya n.k. huku vilevile ukikumbuka mgogoro mkubwa wa Angola ulikwisha kwa maongezi tu. MATUMIZI YA NGUVU SI SULUHISHO LA KUDUMU NA KAMA INGELIKUWA NDIVYO BASI IVORY COAST NA NIGERIA MPAKA LEO KUNGEKUWA HAKUKALIKI, KAMA ILIVYO KWA IRAQ NA AFGHANISTAN.:smile-big:
 
Kweli kaka...ki ubinadamu haya yaliyojitokeza kwenye uchaguzi yametia vidonda katika mioyo ya wengi...ila nakubalina nawe kuwa kuna haja kutafuta namna ya kuzizinga hasira zisizae chuki...nina imani kuwa kwa kutumia hekima, busara na nguvu ya hoja mtanzania atakombelewa tu...
apo chacha!:tape:
 
Swali la msingi KAA LA MOTO.

Msimamo wangu ni kwamba, Hoja ya Nguvu, ni jambo la lazima na lisiloepukika, kwa sababu ni upande wa pili wa Nguvu ya hoja.
Kuwaandaa Watanzania kukataa Amri zisizo za kisheria ni moja kati ya mambo ya Awali kabisa yenye kujenga Msingi wa Hoja ya Nguvu.
Nguvu ya hoja itangulie ikisindikizwa na Hoja ya Nguvu. Hiyo ndiyo lugha sahihi ambayo CCM wataielewa hakuna Polisi, FFU.UWT na hata JWTZ wawwezao kupingana na Hoja ya Nguvu ya wananchi.
Kiongozi na mwasisi wa South Afrika NELSON MANDELA alianzisha Military wing ya ANC ambayo hatimaye ilimpeleka Jela na kuwapa taabu sana Makaburu. Sisi hapa tunadeal na Makaburu Weusi ambao tumesha penetrate ngome yao kwa sana. Tutatumia Nguvu ya Hoja lakini wakae wakijua kwamba Hoja ya Nguvu haichezi mbali.

Ndiyo maana somo la Siasa ya CCM High Schoo nilipata F lakini nikiwa chuo niliandika Misonge ya nguvu sana.
Ndugu yangu Madela Wa- Madilu,
Leo asubuhi nilikuwa kwa shoe polisher mmoja na palikuwa vijana pale. Mmoja wa vijana wale wakaniuliza swali. "Mzee kaa la moto, je mbona Dr Slaa hasemi kitu?"
Niliwajibu bado yuko katika tathimini na atakuja tu kutokea na hoja iliyo na uhakika na iliyosheheni ushahidi ambao hata ccm hawataweza kujitetea. Nikawambia ninavyomjua Dr Slaa si mtu wa kuja na bla bla za kulalamika kama walivyokuwa wanalalamika wakina Seif. Nikawambia lazima atakuja na evidence.
Baadae kati ya wale vijana mmoja akaniuliza "Mzee kaa la moto, je kama hii njia ndiyo inatumika kuchagua viongozi wa nchi hii kwa nini tunapoteza muda wetu kupiga kura?" yeye akasema anaona si vema kupiga kura badala yake hawa viongozi tuwaache wawe viongozi wa maisha kuliko kupoteza muda wao na pesa ya serikali kwa ajili ya uchaguzi. Nilisikitishwa na kauli yake kwamba "Sintapiga tena kura katika nchi hii"
Neno hilo lilinisikitisha sana kiasi kwamba nilianza kumshawishi kwamba hilo wazo lake ndilo haswa ccm wanachotaka. Maana kwa kutopiga kwake kura ccm wao hawatajali bali baadhi ya viongozi na familia zao watapiga kura na kurudisha maharamia hawa hawa na maisha yataendelea kama yalivyo.
Mara akadakia mwenzie kwa kusema "mimi naona suruhu ni kuchapana tu wengine wafe na wengine watunze heshima ya wengine." Ghafla ikanirudisha kwenye mazungumzo yetu yanayoendelea hapa. Maana niliona wote wanaanza kukubaliana na hoja hiyo na nikaona mara kuwa kuna hatari kubwa mbele yetu. Nikajaribu kuwatuliza kwa kuwambia hapana zipo njia nyingi mbadala kama anavyotutuliza mwanakijiji hapa, lakini niliendelea kupata pressure toka kwa vijana hao kuwa hakuna njia mbadala ila tutumie nguvu kupata haki zetu. Niseme ukweli niliamua kuondoka kimya kimya nikiacha mzozo ukiendelea ili nisijikute nabanwa kwa maswali magumu zaidi. This is a true story na imetokea asubuhi ya leo.
Sasa basi hoja yako Madela Wa- Madilu inanirudisha kule kule nilikokuwa asubuhi. Tutafute namna ya kupeleka nguvu ya hoja kwa watawala wetu hawa wakina Kikwete lakini ikishindikana the other option ni kutumia hoja ya nguvu kwa watawala hawa hawa.
 
Great thinkers, JF kuna rules zinazoonyesha bayana do's and dont's. Kwa ubendera hadi upepo mzee ahubiri moral conducts, tuvume naye upande huo.

Siku mwanakijiji atayohamia ccm......
 
Nimeona dilema ilipo!

Ni kwenye mantiki nzima ya namna ya kutumia nguvu kwenye kujenga na kustawisha jamii.

Kimsingi tutambue kuwa kuna nguvu kuu mbili ambazo lazima zitumike kwenye kufanikisha ustawi wa maisha yetu kila siku. Ni lazima kutumia nguvu moja kati ya hizi mbili.

Chuki, hasira, woga, kinyogo, kisasi, ukatili, unyama.. Ni nguvu

Upendo , heshima , haki, ubinaadamu, ujasiri, ukweli, busara na Utu..pia ni Nguvu.

Moja ni nguvu iliyo asili ya ustawi wa mwanadamu, ni nguvu ya kustawisha Utu na maendeleo ya mwanadamu…Ni lazima kuitumia tena kwa kiwango kikubwa ikibidi.

Lazima kutumia nguvu sahihi ninapodai ustawi sahihi kwenye jamii yangu… hili halina mjadala. Nguvu ya Utu, Upendo, Heshima, Busara..na Ubinaadamu lazima itumike…hata ikibidi nguvu hii kubebeshwa silaha ya aina yeyote.

Nguvu ya Utu na matawi yote inaweza kutumika kuistawisha na kuijenga jamii inapobebwa na ..silaha, elimu , mawazo, kauli, matendo nk. Ni nguvu inayovipa vitu vingine vyote thamani yake. Bila nguvu sahihi fikra, kauli , matendo havina maana yeyote..

Nguvu ya utu lazima itumike kumhoji Rais, Serkali, yeyote anayehusiaka na NEC mienendo yote ya uchaguzi ilivyokwenda…sitatumia nguvu ya kuupinga utu wangu wala wa Rais wala watu wote wanaohusika, wala wa Watanzania lakini nitatumia nguvu sahihi Kutaka kujua ukweli wa kura yangu niliyopiga.

Nitatumia nguvu sahihi ya Utu..kumhoji Rais..Lazima kufanya hivyo kwa nguvu sahihi tena kwa ubora wote. Sitatumia..chuki, hasira, kinyongo, ukatili na hali ya unyama katika kutekeleza adhma yangu. Nitatumia nguvu tena kwa kiwango sahihi kulingana na namna hoja itakavyokuwa inajiendesha..lakini kwa nguvu sahihi, ya Upendo, Heshima, Haki..na kuenzi Utu na Ubinnadamu.

Ni lazima kufanya hivyo kwani Kibox cha kura kipo kuilinda na kuienzi nguvu sahihi katika kustawisha Serekali, wizara zake, taasisi mabalimbali…na Kiongozi mkuu yupo kulinda na kusimamia kuwa nguvu sahihi inatumika katika miongozo yote ya Tiafa, kwa hiyo nguvu sahihi lazima itumike tena kwa kiwango stahili kulingana na nyakati na mahitaji.

Kushindwa kutumia nguvu stahili kuilinda na kuistwaisha jamii..ni aibu na ni kusaliti, Utu na ubinaadamu wa ulimwengu huu. Na iko wapi maana ya maisha kama hilo limetushinda? Taifa la Tanzania linahitaji nguvu na sio umaamuma katia kufikia ngazi inayofuta katika maendeleo yake.. Lakini Nguvu sahihi.. ile yenye inayoweza kuharibu silaha zote duniani..Nguvu ya UTU!

Demokrasia itakuwa ni kama kasha tupu kama haikubeba moja kati ya nguvu hizi.

Ikibeba nguvu ambayo sio sahihi …itakuwa ni demokrasia inayofaa wanyama wa mwituni na mafisadi walioikumbatia Tanzania kwa sasa huku ukitumia ujanja na mbinu tata kuifunga midomo na fikra zetu..huku wao waki advansi kwa kasi kufikia malengo yao.

Demokrasia sahihi inayosimamia maendeleo ya kweli ..imejengwa na kubeba nguvu sahihi. Inajua shina la ustawi wa mwanadamu na kulienzi kwenye kila nyanja…na haioni tatizo nguvu kutumika kwani nguvu sahihi si adui wa mwanadamu kamili na chochote ila hili litapingwa na wapinga Utu na ubinaadamu. Na sisi hatutawaelewa kabisa…

Kwenye demokrasia ya nguvu sahihi ya utu na ubinaadamu ni sahihi kutumia nguvu sahihi na kuibebesha silaha, mabomu, vifaru, majeshi…ili kuilinda jamii ya binaadamu timamu waliostaarabika. Na ninaongea hivi kwa ujasiri mkubwa usio na ujeuri, chuki, woga, ila kwa upendo na heshima kuu kwa watu wote.

Lakini kwenye demokrasia pinzani kwa utu na ubinaadamu, nilichosema kitakuwa ni tatizo lakini wao watataka kutumia silaha za kivita, majeshi, na nguvu zote za dola ili kilinda nguvu isiyo sahihi ya ufisadi. Hili halikubaliki kamwe!!!

Kwa hiyo tusiwe wajinga; Vita, mabomu ya nuklia, silaha mbalimbali, majeshi, usalama wa taifa na nyenzo kama hizo zenyewe sio tatizo. SHIDA NI NGUVU GANI VITABEBESHWA VYOMBO HIVYO! ..Kisu cha mkate ..kinaweza kutumika kwa ubaya au kwa uzuri..hilo lieleweke…hii ni pamoja na dhana ya kumwaga damu... Damu kumwagiga si tatizo inategemea unafanya hivyo kwa ajili ya nguvu ipi!!! Mwaka 1978 Tanazania kwa kutumia nguvu sahihi ilimwga damu kule kagera na hatimaye uganda! ...Hoja ni Nguvu gani inabeba hiyo vita na malengo yake...nk lakini tusiogopeshani juu ya kumwaga damu. Jambazi akavamia nyumba yangu usiku wa manane na kuanz akusogelea chumba cha mabinti ..wangu..ohh Nitamwaga damu!! Ili kulinda heshma na ubinnadamu na ustaarabu wa familia na dunia yote!!

Chadema, CCM, TLP, nk…ni vyombo vya kuilinda na kuitetea nguvu stahili katika kujenga na kustawisha jamii. Kama chama chochote kitakiuka misiningi hiyo ..nguvu sahihihi itatumika kukihoji tena bila woga , hasira, chuki, na aina yeyote ya nguvu isiyo sahihi…ikibidi hata kutumia chochote, ..ili mradi chochote hicho kibebe nguvu sahihi. Chama hicho kisitegemee tutakuwa magoigoi na wanyonge..kukikabili la hasha tutakihoji. Lazima hili nilieleze kwa upendo, ujasiri na kuuheshimu utu wangu na watanzania wote kuwa..Lazima kitafuatwa kwa nguvu ..tena nguvu kabisa..na kitahojiwa ..vipi hakilindi uasili na ustawi wa mwanadam. Haitawezekana tena kututishia vita, kupoteza amani nk. Kama amani ikipotea kwa ajili ya nguvu sahihi ..hakuna tatizo lolote... kwani kusema kweli amani na utulivu huo havikuwepo!

JF..inahaki kutumia nguvu sahihi kuhoji na kulinda utu na ubinaadamu wa jamii inayojikuta. Hili ni sahihi kwa blog na mitandao yote nchini. Technologia na watu wake sio tatizo..tatizo ni inabebeshwa nini….

Utu na ubinaadamu sio mali ya mtu au chama chochote useme itafungiwa na kuangamizwa. Kuangamiza nguvu sahihi kwenye jamii..ina maana kuangamiza watu wote kwnye jamii hiyo na hilo haliwezekani. Hakuna anayeweza kuangamiza nguvu sahihi. Mtu asije kudanganywa na kudanganyika….

Kama JF na wanachama wake ni watii wa Utu na ubinaadamu wao ..na wametumia nguvu sahihi katika kauli, fikra na matendo yao na JF ikafungiwa ..sawa… Ni kwa kuwa ujumbe na lengo la JF litakuwa limefika..na hakuna atakaye jinsikia mkosaji.

Kama JF italazimika kutumia nguvu isiyo sahihi kama woga, wasiwasi, kuupinga na kuusaliti utu wa jamii yake nk ili isifungiwe ..hiyo sio sawa..bora ifungiwe kuliko itumike kustawisha nguvu isiyo sahihi kwenye jamii.

Si kweli kuwa kuna mamlaka ya kibinaadamu inayoweza kufumgia nguvu ya utu inayotegeneza nguvu ya umma iliyosheheni nguvu sahihi..nguvu ya umma. Hamuoni ..viti 22 mjengoni…Hamuoni..toka 80% mwaka 2005 hadi 61% mwaka 2010..Ni bilioni ngapi zilitumika kuhonga na kuyumbisha matokeo..? Hakuna!! Ni mwanzo wa nguvu sahihi kuiteka na kuirudisha Tanzania ile ya waasisi wake!! Peoples power.

Mamlaka yenye ufinyu wa kufikiri kuwa nguvu sahihi ya umma unafungika au kuangamizwa..malaka hiyo itakuwa imepofuka na ni dhaifu ..itaangamia.

Tuamke tutumie nguvu sahihi..kulijenga Taifa letu! Ikibidi hata kulifia kwenye misingi sahihi kwani huo ndio uzalendo..na utanzania wenyewe..

Na tunamuomba Mungu atubariki katika ujenzi wa Taifa hili!!
 
Dawa ya moto ni moto ingawa kuna wakati mwingine dawa ya moto ni maji. Kwa sasa nakubaliana na wewe kuwa tutumie maji kama dawa ya moto, lakini ikiwa upande mwingine hautakuwa tayari kuelewa kuwa maji ndiyo dawa, basi dawa mbadala itatumika.
Hata Yesu kuna wakati aliingia kanisani akakuta watu wanaitumia nyumba hiyo tofauti na makusudio - alitengeneza mjeledi wa kamba na kuzipindua meza zao.
Mwanakijiji nakuelewa unachozungumzia, lakini nahisi ccm hawako tayari kwa mazungumzo. Si umeona pemba? - baada ya bakora sasa muafaka - shwariiiii!. Tuwape muda lakini wajue pia kuwa uvumilivu una mwisho na hili gunia la amani wanalotumia kufichia maovu yao iko siku litatoboka maana limekwishazeeka
 
Msemo maarufu hapa JF ni '' let us call a spade the spade not a big spoon''. Tafadhali rejea mada ya MMKJ na hasa aya za mwisho. Ukweli unabaki pale pale watu waseme kwa lugha yenye hoja. Tunaposema lugha za vitisho ni kama zilizotumika ''sniper'' n.k. Watu wanataka kujenga hoja zenye nguvu,hoja zilizotufikisha mahali ambapo Chama tawala kimehofia matokeo, hoja zitakazotufikisha mahali tunapata 2/3 majority, hoja zitakazotuwezesha kuwa na mabaraza ya madiwani kama karatu. Tunahitaji hoja zitakazojibu matatizo ya wananchi. kusema nitampiga au kumdhuru fulani si hoja zenye mashiko, matatizo yetu ni mengi kiasi kwamba tunahitaji umma utuelewe na uelewe.
Kutisha mtu ni silaha iliyotumiwa na CCM kuwadhalilisha wapinzani, hatuhitaji kuwatisha watu, tuwaambie wa morogoro wamechagua nini na wategemee nini, tujenge hoja itakayowasukuma waelewe hatima ya nchi yao kimaendeleo kama walivyoelewa kigoma,mwanza, Tanga, Lindi, Kilimanjaro, mbeya, Arusha, Singida,n.k.
Kuanzisha forum hiyo inawezekana kila siku, lakini kuwa na forum ambayo ni jicho la jamii si kitu rahisi. Hatuhitaji mtu aipende JF lakini pia si vema watu kuvuka mipaka. Kumbuka uhuru wa mtu huishia pale wa mwenzake unapoanzia.
Nitaita spade the spade na si big spoon hata kama kufanya hivyo kutakuwa na mtazamo tofauti. Bado naunga hoja ya MMKJ.
Kabla hujaendelea na kushabikia anayosema MMKj, muulize aliita CCJ spade au big spoon?
Huyu ni bingwa wa spinning, atabakia kuwa hivyo mpaka pale atakapotueleza aliingizwa chaka on CCJ issue au la. Watu wanaomwamini kama wewe na wengine ninauhakika wangehama vyama vyao vilivokuwa na dira na kuhamia kwenye hoax - CCJ. Ushindi uliopatikana sasa hivi kwa kupitia vyama vya upinzani ungepatikana?

THINK.
 
Kweli kaka...ki ubinadamu haya yaliyojitokeza kwenye uchaguzi yametia vidonda katika mioyo ya wengi...ila nakubalina nawe kuwa kuna haja kutafuta namna ya kuzizinga hasira zisizae chuki...nina imani kuwa kwa kutumia hekima, busara na nguvu ya hoja mtanzania atakombelewa tu...

apo chacha!:tape:

Ndio... soma post namba 97
 
Nimeona dilema ilipo!

Ni kwenye mantiki nzima ya namna ya kutumia nguvu kwenye kujenga na kustawisha jamii.

Kimsingi tutambue kuwa kuna nguvu kuu mbili ambazo lazima zitumike kwenye kufanikisha ustawi wa maisha yetu kila siku. Ni lazima kutumia nguvu moja kati ya hizi mbili.

Chuki, hasira, woga, kinyogo, kisasi, ukatili, unyama.. Ni nguvu

Upendo , heshima , haki, ubinaadamu, ujasiri, ukweli, busara na Utu..pia ni Nguvu.

Moja ni nguvu iliyo asili ya ustawi wa mwanadamu, ni nguvu ya kustawisha Utu na maendeleo ya mwanadamu…Ni lazima kuitumia tena kwa kiwango kikubwa ikibidi.

Lazima kutumia nguvu sahihi ninapodai ustawi sahihi kwenye jamii yangu… hili halina mjadala. Nguvu ya Utu, Upendo, Heshima, Busara..na Ubinaadamu lazima itumike…hata ikibidi nguvu hii kubebeshwa silaha ya aina yeyote.

Nguvu ya Utu na matawi yote inaweza kutumika kuistawisha na kuijenga jamii inapobebwa na ..silaha, elimu , mawazo, kauli, matendo nk. Ni nguvu inayovipa vitu vingine vyote thamani yake. Bila nguvu sahihi fikra, kauli , matendo havina maana yeyote..

Nguvu ya utu lazima itumike kumhoji Rais, Serkali, yeyote anayehusiaka na NEC mienendo yote ya uchaguzi ilivyokwenda…sitatumia nguvu ya kuupinga utu wangu wala wa Rais wala watu wote wanaohusika, wala wa Watanzania lakini nitatumia nguvu sahihi Kutaka kujua ukweli wa kura yangu niliyopiga.

Nitatumia nguvu sahihi ya Utu..kumhoji Rais..Lazima kufanya hivyo kwa nguvu sahihi tena kwa ubora wote. Sitatumia..chuki, hasira, kinyongo, ukatili na hali ya unyama katika kutekeleza adhma yangu. Nitatumia nguvu tena kwa kiwango sahihi kulingana na namna hoja itakavyokuwa inajiendesha..lakini kwa nguvu sahihi, ya Upendo, Heshima, Haki..na kuenzi Utu na Ubinnadamu.

Ni lazima kufanya hivyo kwani Kibox cha kura kipo kuilinda na kuienzi nguvu sahihi katika kustawisha Serekali, wizara zake, taasisi mabalimbali…na Kiongozi mkuu yupo kulinda na kusimamia kuwa nguvu sahihi inatumika katika miongozo yote ya Tiafa, kwa hiyo nguvu sahihi lazima itumike tena kwa kiwango stahili kulingana na nyakati na mahitaji.

Kushindwa kutumia nguvu stahili kuilinda na kuistwaisha jamii..ni aibu na ni kusaliti, Utu na ubinaadamu wa ulimwengu huu. Na iko wapi maana ya maisha kama hilo limetushinda? Taifa la Tanzania linahitaji nguvu na sio umaamuma katia kufikia ngazi inayofuta katika maendeleo yake.. Lakini Nguvu sahihi.. ile yenye inayoweza kuharibu silaha zote duniani..Nguvu ya UTU!

Demokrasia itakuwa ni kama kasha tupu kama haikubeba moja kati ya nguvu hizi.

Ikibeba nguvu ambayo sio sahihi …itakuwa ni demokrasia inayofaa wanyama wa mwituni na mafisadi walioikumbatia Tanzania kwa sasa huku ukitumia ujanja na mbinu tata kuifunga midomo na fikra zetu..huku wao waki advansi kwa kasi kufikia malengo yao.

Demokrasia sahihi inayosimamia maendeleo ya kweli ..imejengwa na kubeba nguvu sahihi. Inajua shina la ustawi wa mwanadamu na kulienzi kwenye kila nyanja…na haioni tatizo nguvu kutumika kwani nguvu sahihi si adui wa mwanadamu kamili na chochote ila hili litapingwa na wapinga Utu na ubinaadamu. Na sisi hatutawaelewa kabisa…

Kwenye demokrasia ya nguvu sahihi ya utu na ubinaadamu ni sahihi kutumia nguvu sahihi na kuibebesha silaha, mabomu, vifaru, majeshi…ili kuilinda jamii ya binaadamu timamu waliostaarabika. Na ninaongea hivi kwa ujasiri mkubwa usio na ujeuri, chuki, woga, ila kwa upendo na heshima kuu kwa watu wote.

Lakini kwenye demokrasia pinzani kwa utu na ubinaadamu, nilichosema kitakuwa ni tatizo lakini wao watataka kutumia silaha za kivita, majeshi, na nguvu zote za dola ili kilinda nguvu isiyo sahihi ya ufisadi. Hili halikubaliki kamwe!!!

Kwa hiyo tusiwe wajinga; Vita, mabomu ya nuklia, silaha mbalimbali, majeshi, usalama wa taifa na nyenzo kama hizo zenyewe sio tatizo. SHIDA NI NGUVU GANI VITABEBESHWA VYOMBO HIVYO! ..Kisu cha mkate ..kinaweza kutumika kwa ubaya au kwa uzuri..hilo lieleweke…hii ni pamoja na dhana ya kumwaga damu... Damu kumwagiga si tatizo inategemea unafanya hivyo kwa ajili ya nguvu ipi!!! Mwaka 1978 Tanazania kwa kutumia nguvu sahihi ilimwga damu kule kagera na hatimaye uganda! ...Hoja ni Nguvu gani inabeba hiyo vita na malengo yake...nk lakini tusiogopeshani juu ya kumwaga damu. Jambazi akavamia nyumba yangu usiku wa manane na kuanz akusogelea chumba cha mabinti ..wangu..ohh Nitamwaga damu!! Ili kulinda heshma na ubinnadamu na ustaarabu wa familia na dunia yote!!

Chadema, CCM, TLP, nk…ni vyombo vya kuilinda na kuitetea nguvu stahili katika kujenga na kustawisha jamii. Kama chama chochote kitakiuka misiningi hiyo ..nguvu sahihihi itatumika kukihoji tena bila woga , hasira, chuki, na aina yeyote ya nguvu isiyo sahihi…ikibidi hata kutumia chochote, ..ili mradi chochote hicho kibebe nguvu sahihi. Chama hicho kisitegemee tutakuwa magoigoi na wanyonge..kukikabili la hasha tutakihoji. Lazima hili nilieleze kwa upendo, ujasiri na kuuheshimu utu wangu na watanzania wote kuwa..Lazima kitafuatwa kwa nguvu ..tena nguvu kabisa..na kitahojiwa ..vipi hakilindi uasili na ustawi wa mwanadam. Haitawezekana tena kututishia vita, kupoteza amani nk. Kama amani ikipotea kwa ajili ya nguvu sahihi ..hakuna tatizo lolote... kwani kusema kweli amani na utulivu huo havikuwepo!

JF..inahaki kutumia nguvu sahihi kuhoji na kulinda utu na ubinaadamu wa jamii inayojikuta. Hili ni sahihi kwa blog na mitandao yote nchini. Technologia na watu wake sio tatizo..tatizo ni inabebeshwa nini….

Utu na ubinaadamu sio mali ya mtu au chama chochote useme itafungiwa na kuangamizwa. Kuangamiza nguvu sahihi kwenye jamii..ina maana kuangamiza watu wote kwnye jamii hiyo na hilo haliwezekani. Hakuna anayeweza kuangamiza nguvu sahihi. Mtu asije kudanganywa na kudanganyika….

Kama JF na wanachama wake ni watii wa Utu na ubinaadamu wao ..na wametumia nguvu sahihi katika kauli, fikra na matendo yao na JF ikafungiwa ..sawa… Ni kwa kuwa ujumbe na lengo la JF litakuwa limefika..na hakuna atakaye jinsikia mkosaji.

Kama JF italazimika kutumia nguvu isiyo sahihi kama woga, wasiwasi, kuupinga na kuusaliti utu wa jamii yake nk ili isifungiwe ..hiyo sio sawa..bora ifungiwe kuliko itumike kustawisha nguvu isiyo sahihi kwenye jamii.

Si kweli kuwa kuna mamlaka ya kibinaadamu inayoweza kufumgia nguvu ya utu inayotegeneza nguvu ya umma iliyosheheni nguvu sahihi..nguvu ya umma. Hamuoni ..viti 22 mjengoni…Hamuoni..toka 80% mwaka 2005 hadi 61% mwaka 2010..Ni bilioni ngapi zilitumika kuhonga na kuyumbisha matokeo..? Hakuna!! Ni mwanzo wa nguvu sahihi kuiteka na kuirudisha Tanzania ile ya waasisi wake!! Peoples power.

Mamlaka yenye ufinyu wa kufikiri kuwa nguvu sahihi ya umma unafungika au kuangamizwa..malaka hiyo itakuwa imepofuka na ni dhaifu ..itaangamia.

Tuamke tutumie nguvu sahihi..kulijenga Taifa letu! Ikibidi hata kulifia kwenye misingi sahihi kwani huo ndio uzalendo..na utanzania wenyewe..

Na tunamuomba Mungu atubariki katika ujenzi wa Taifa hili!!
Nimekukubali mkuu wangu. Thanks again.
 
...Kwa kufanya hivyo, tunaweka mtandao wetu tuupendao hatarini kwani kikiwa ni chombo kilichoandikishwa na licha ya watu kutumia majina mbadala endapo jambo fulani linatokea mtandao huu una wajibu wa kushirikiana na vyombo vya kiusalama kutekeleza amri halali ya mahakama kuweza kuwapata wahusika. Sasa tusichukulie kimzaha tunapotoa kauli zenye mfanano wa vitisho, kauli hizo hazilindwi na "uhuru wa maoni" kwani ni kama ilivyosema "kupiga kelele moto, kwenye ukumbi uliojaa" ....

Ni kweli kabisa, japo mi ni member mgeni wa kujiunga ila nimekuwa nikiitembelea hii forum muda mrefu, nimeona watu wengi wanapoona wanatumia majina mbadala wanatumia hoja za nguvu na kauli ambazo kwa mtazamo wangu ni hatarishi na zinawaweka ma mods pabaya.

Hivyo nina shukuru Mkuu kwa kutujuza na kutukumbusha wanaJF kwa ujumla kuwa tuwe makini kwenye kutoa hoja tukijua kuwa uhuru wa kuoa maoni si uhuru wa kuvunja sheria, na kwa technolojia ya sasa we can easily be traced no matter tunatumia majina mbadala.

Tusikubali JF iharibiwe na wasio itakia mema, kwani JF ime na ina endelea kutusaidia wengi, walio nchini na wasio nchini.

Umesikika na kueleweka!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom