ANGALISHO:Watumiaji wa VODACOM

ThinkPad

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
1,844
232
Jamani watumiaji wa vodacom ikifika saa 11 jioni gharama ni zilezile msijisahau nasikitika kwanini voda hawakutangaza kuwa mwisho ni saa 11 jioni hii imenikuta mimi baada yakuongea najua naongea kwa sh 60 kwa dk kumbe naongea kwa 4** kwa dk nikajikuta nimemaliza pesa yangu yoote kwenye simu.
 
Pole ThinkPad. Nadhani hii ni mbaya sana kwenye biashara. Ilitakiwa kwenye matangazo yao yote (hata ya Tv na radio) hili waliweke wazi kwa wateja wao. Kusema tu 'Terms and Conditions' apply, haitoshi.
 
Kwa nini wafanye siri siri hizo terms. Walishanogewa kutuibia sasa wanashindwa kuacha wizi. ENYI VODACOM, njooni mseme wazi sera zenu tuzielewe ili tuamue kuendelea nanyi au tupa mbali.
 
Hahahahaha dah wajinga ndo waliwao sisi tulisha stuka mtandao wa kifisadi huo.
 
Thanks Ndugu:

Lakini kilichofanyika ni maksudi maana kwenye Radio wanasema 24hr 1per sec sasa jamani hii ni halali kweli wanafanya au wameshagundua udhaifu wetu kuwa bora liende then wana take advantage tena hao unakuta ni waswahili wenzetu wenye asili ya kiasia au Wenye asili ya kiafrika kama mimi na wewe.....

Jamani tuwe makini PESA ni ngumu kuliko kawaida sisi tulioko huku duniani tunaonja joto la jiwe..naomba tuurumiane.
 
Janja ya nyani kula mahindi mbichi wanatuyeyusha hawa kwanini wasiseme wazi hii hai-apply kuanzia saa 5pm-9pm na kwa sasa wanatumia nguvu nyingi mno kujitangaza kama hii picha hapa...

attachment.php
 
Attachments

  • vodashilingimoja.jpg
    vodashilingimoja.jpg
    61.2 KB · Views: 195
Kwa nini wafanye siri siri hizo terms. Walishanogewa kutuibia sasa wanashindwa kuacha wizi. ENYI VODACOM, njooni mseme wazi sera zenu tuzielewe ili tuamue kuendelea nanyi au tupa mbali.
niliamiaga TIGO sikunyingi BAADA YA KUGUNDUA VODA WIZI MTUPU.
 
Pole ThinkPad. Nadhani hii ni mbaya sana kwenye biashara. Ilitakiwa kwenye matangazo yao yote (hata ya Tv na radio) hili waliweke wazi kwa wateja wao. Kusema tu 'Terms and Conditions' apply, haitoshi.

Poleni sana. Ila matangazo yao yapo wakati wa kuangalia salio. Ukiangalia salio hata sasa hivi. unapata meseji kama hii hapa
Salio lako ni Tsh. ***. Habari Ndio hii, Tsh1 kwa sekunde, Voda kwa Voda siku nzima, Kila siku (isipokuwa saa 11 jioni hadi 3 usiku)
Halafu hawa Voda walivyo wabahiri sijui kwa nini. Kwa nini isiwe siku nzima mfululizo kama TIGO?
 
Dah pole mzarendo
Huu mtandao bana kuna watu wamefunga nao nadhiri.

Na mimi nikiwa mmojawapo. toka 2001 niko Voda. Lakini na mitandao mingine ninayo pia. Ila Voda iko hewani 24hrs
 
sasa hapa ndio namuona mafuru na mwamvita kama katuni....kwanini watangaze kwenye TV kuwa ni 24hrs kumbe uzushi....tutaendelea kujiexpress kama kawa
 
Jamani watumiaji wa vodacom ikifika saa 11 jioni gharama ni zilezile msijisahau nasikitika kwanini voda hawakutangaza kuwa mwisho ni saa 11 jioni hii imenikuta mimi baada yakuongea najua naongea kwa sh 60 kwa dk kumbe naongea kwa 4** kwa dk nikajikuta nimemaliza pesa yangu yoote kwenye simu.

Mimi sio MTEJA WA VODA lakini hilo nalijua na nimeliona kwenye matangazo, lakini POLE SANA.
 
Inabidi tuwe makini sana na hizi wanazoziita promosheni, mara nyingi zimekaa kiwiziwizi.
 
Jamani watumiaji wa vodacom ikifika saa 11 jioni gharama ni zilezile msijisahau nasikitika kwanini voda hawakutangaza kuwa mwisho ni saa 11 jioni hii imenikuta mimi baada yakuongea najua naongea kwa sh 60 kwa dk kumbe naongea kwa 4** kwa dk nikajikuta nimemaliza pesa yangu yoote kwenye simu.
so sad! unasikitika nini? unaona uchungu gani kutumia hela bana? tatizo husomi habari, ndugu na wala usiwalaumu voda. usipende sana vya chee ndugu. mia nn4 kitu gani?
 
Mwamvita na Mafuru huku mishipa ya shingo imewakakamaa mbele ya kamera za tbc1 wakisema "hii si promosheni....tunamaanisha kwamba unaruka kwa Tshs.1 kwa saa 24...habari ndo hii" ( non verbatim") : Kama wateja wanaibiwa kiaina hii sishangai kwani URT siku hizi ni kama shamba la bibi. Enyi wateja wa VTL pelekeni mashtaka yenu pale TCRA au baraza la walaji kwamba VTL wamewatapeli.
 
Back
Top Bottom