Angalia kwa makini vijana hawa.....

Mkuu Anyisile hauko sahihi sana kwa ulichoandika. baada ya kuangalia hiyo picha ilikupasa urudishe kumbukumbu zako nyuma na kujiuliza; Picha hiyo ilipigwa lini? Ilipigwa chuo gani? Nini lilikuwa suala la msingi mpaka hao wakaandamana? Maana ya ujumbe uliopo hapo ndani ya mabango? Nini yalikuwa matokeo ya ujumbe wa bango hilo na maandamano/mgomo wao?

Usikurupuke tu kudharau wakati unaonyesha ni bingwa wa kusahau( unamatatizo makubwa). Nani kakwambia kuwa walikaririshwa wafanye hivyo? Rudia kuyasoma mabango yote mawili, halafu tumia akili yako kuyatafsiri maudhui yake

Labda kukukumbusha wewe nawale wengine wanaotafsiri vibaya ni kuwa picha hiyo ilipigwa pale UDSM-Main campus wanachuo walikuwa wakilalamikia kutopewa pesa zao toka Bodi ya Mikopo.

Hawa wasomi walitumia fikra zao kiusahihi katika kutafuta chanzo cha matatizo waliyonayo. Japo kwa nje tatizo laonekana ni Bodi ya Mikopo, lakini kiuhalisia tatizo la msingi lilikuwa serikali ambayo watendaji wake walichaguliwa ama kupewa vyeo kwakuwa ni marafiki wa Jakaya Kikwete au walimsaidia kuingia madarakani (connect na yule mama aliyekuwa anahusika na kashfa za EPA akapelekwa kwenye Bodi hiyo).

Japo walisalitiwa na yule Raisi wa TAHLISO (ambaye ni kada CCM) na kisha kufukuzwa, ukweli umebaki vilevile hadi leo ya kwamba "TANZANIA TUMEPATA MATATIZO MAKUBWA SANA KATIKA AWAMU HII YA NNE HATA WENGINE KUSHINDWA KUWAJIBISHWA JAPO NI WEZI, KWASABABU TU NI WASHIKAJI (MARAFIKI,VIBARAKA,etc) wa KIKWETE".

Need I say more?

Naomba tujiulize wanafunzi hao walikuwa waongo?

Nimekukubali kiongozi we ni thinker wa kweli!!
 
Walimaanisha hayo yanayosomeka tatizo ni la leo kulaani na kesho kupongeza ni ukweli kuwa wanaolaani siku ya kupongeza hawajitokezi kwani mara nyingi huwa ni mamluki wa magamba
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom