Andrew Nyerere on Mwalimu humble children!

I think he knows. I just hope he is successful unlike his try in politics.

Afu na wewe mshikaji wake sijuhi unampa ushauri gani. Jina la baba yao kama trade mark ya Coca-cola. Yaani sijuhi wanashindwa nini kutumia ile brand.
 
Zakumi,

Hapa kuna a classic dilemma kwenye familia ya Nyerere.

Upande mmoja mnawaona hawako competitive -kwa lugha rahisi wamezubaa-

Upande mwingine wangechangamka na ku push ma BMW kama mtoto wa muungwana watu wangewaita mafisadi.

What's a president's son to do? Mie ndiyo maana nimekataa kumuita mtoto wa muungwana fisadi just because ana push BMW
.

acha kumtetea ni fisadi, anafanya kazi IMMA na cheo chake ni legal officer amepata wapi hela ya kunua hiyo BMW.
usione watu hawana akili humu ndani, you dont have to be a rocket scientiest .......
 
acha kumtetea ni fisadi, anafanya kazi IMMA na cheo chake ni legal officer amepata wapi hela ya kunua hiyo BMW.
usione watu hawana akili humu ndani, you dont have to be a rocket scientiest .......

Mnataka atembelee nini ??? bajaji ???. Misafara anayofanya rais na marupurupu anayopata yanatosha kwa familia ya rais kuwa na BMWs.

Swali lije kwenye performance. Je rais kutokana na marupurupu anayopata anafanyakazi tunayotaka ???
 
acha kumtetea ni fisadi, anafanya kazi IMMA na cheo chake ni legal officer amepata wapi hela ya kunua hiyo BMW.
usione watu hawana akili humu ndani, you dont have to be a rocket scientiest .......

You are missing the point.

Hii habari ya "amepata wapi hela ya kununua BMW" ndiyo kusaka wakomunisti alikokufanya Eugene McCarthy.

Principles za deal ni kwamba watu wengi tukijua deal thamani ya deal inapungua, kwa hiyo kumsema mtu "amepata wapi hela wakati mshahara wake tunaujua" ni kusema kwamba huyu bwana anategemea mshahara tu, unajuaje kama babu yake aliokota sarafu za Mjerumani Bagamoyo?

Point ninayoisema hapa ni kwamba, ukitaka kukmuita mtu fisadi muite, lakinio njoo na data, jamaa anafanya IMMA IMMA mafisadi hivi na vile, yeye alivyopatiwa kazi kifisadi hivi, kuna mfanyabiashara fulani fisadi ndiye kamnunulia lile BMW, hapo tutaelewa.

Vinginevyo ukija na "amepata wapi hela mshahara wake tunaujua" unakuwa unaishi maisha ya kizamani ya Kinyerere, ya kutegemea mshahara.

Si ndiyo hayo tunayowasema watoto wa Nyerere hawako competitive?

You just proved my point.

Kama unataka kumsema mtoto wa muungwana fisadi onyesha ufisadi unatokea wapi, hata wewe tukija kukupigia hesabu vitu vyako na mshahara wako vinaweza visioane.

Ufisadi hata mie naupinga, na Kikwete sim mind tangu day one, lakini kuna hii bitterness nai sense hapa ya kwamba kila mtu anayepush BMW fisadi.Hata kama mtu fisadi kweli, justify case yako kwa kutoa a concrete narration kwa nini unasema fisadi.Hizi habari za kumaka tu "fisadi fisadi" kesho keshokutwa utawa group watu wote wenye hela kwenye ufisadi.

Bongo si masikini? Wametoa wapi hela?

Furaha yako wote tuwe masikini?
 
It all depend na unavyo-define maisha ya kawaida, uliyem-quote hajatia chumvi kusema wana wa Mwl JKN waliishi maisha ya kawaida......Yes ni watoto wa Mwl na hawakuomba kuzaliwa na Mwl JKN....however ktk level ya mtu kuwa Rais kuna opportunity nyingi ambazo watoto wangeweza nufaika nazo.......lakini baba yao hakuendekeza hizo na badala yake aliwapa nafasi ya kuwa kama watanzania wengine wa kawaida.........narudia kuishi kwao Ikulu au kwenye Nyumba ya Rais ambaye alikuwa Baba yao....hawakuomba iwe hivyo............

huhitaji kuwa mtaalamu wa kutathmini kujua kuwa wana wa Mwl JKN waliishi maisha ya kawaida.............

unapolinganisha opportunities zetu tuliomo humu JF na kwamba sisi sio wa kawaida....unakosea.......kwa sababu wengine humu tumetokea from kijijini tukiwa na nothing na we went through mpaka tulipofikia hapa.........

Mkuu Ogah. Kuna tofauti kati ya mtanzania wa kawaida na mtu wa kawaida. Tunapozungumzia ( kama unavyofanya wewe) mtu wa kawaida tunapanua wigo. Hapo tunazungumzia "average person" na humo wewe na mimi tunakuwemo. Lakini tunapozungumzia mtanzania wa kawaida ( kama alivyofanya PM) yaani average Tanzanian, wewe na mimi hatumo humo. Katika nchi ambamo asilimia 10 ya wananchi wake wana umeme, sisi tunaopeta kila siku kwenye mtandao hatuwezi kujihesabu kuwa average. Sisi ni privileged. Tusijilinganishe na middle class kwa wenzetu. Kwetu middle class ni wenye neema na wengi wanashindana na umasikini uliokithiri. Watoto wa Mwalimu hawajawahi kuwa na maisha ya average Tanzanian.

Sijawalaumu watoto wa Nyerere kwa kuishi Ikulu n.k. Ninachokataa ni kudai kuwa hawa hawakupata upendeleo wowote kutokana na wao kuwa watoto wa rais. Hawa hawakupata hata tatizo basic la watanzania wengi yaani kupata makazi ya heshima. Wote walipatiwa makazi na si kutokana na juhudi zao bali kutokana na uzawa wao. Hivi kweli tunaamini kuwa hizo nafasi za ubunge n.k. wangepata kama wasingekuwa watoto wa Mwalimu?

Naam, nakubali kuwa hakuna tuhuma dhidi yao ya kile tunachokiita ufisadi siku hizi kama ambavyo ilivyo kwa watoto wa viongozi wengi nchini mwenu. Hata mtoto wa Katibu kata wa siku hizi inawezekana akajisikia kuliko wanavyofanya hao. Lakini hii haiondoi ukweli kuwa kipimo cha mtu si ufisadi peke yake. Katika nyanja nyingine za maisha, wao kama tulivyo sote, walikuwa na mapungufu yao. Wapimwe, wasifiwe na wahukumiwe kwa kile ambacho wame-achieve wenyewe na si kwa sababu walizaliwa na Mwalimu.

Amandla...........
 
Mkuu:

Pamoja na mimi kutumia mtandao, bado nipo-aveleji.
 
nyerere amelitumikia taifa na akastaafu akawa anakula pension yake, watoto wake nao wanatakiwa watafute za kwao na si za baba yao.
kama watoto wa nyerere hawana hela ni kwa ajili wao wenyewe hawakutaka kujishuhulisha kwa ajili baba yao aliwapa elimu na akampa kila mtz elimu......
kutokuwa na hela kwa watoto wa nyerere hakuusiani na nyerere bali juhudi za watoto wake.
watoto wengi wa viongozi sasa hivi hawana juhudi na hela zao ni moja kwa moja ufisadi wa baba zao na ndio maana wanamuona nyerere mpumbavu, angetaka kuiba kama baba zenu watoto wake wangekuwa matajiri kulikoni nyinyi watoto wa viongozi sasa hivi na madhara yake hapa JF wangekuwa watu wa chache kwa ajili wengi wamesoma bure humu JF.
hizo hela ambazo baba zenu wanaiba kuwapa nyinyi zinatosha kusomesha watu kibao ambao wanagoma kila siku pale mlimani kwa ajili hawajapata posho.
lakini hiyo akili ya voingozi kuiba mpaka vijukuu vyao sio ukali na sio ujanja bali ujinga...
lakini hiyo akili ya watoto wa viongozi kupora mali za watanzania sio ujanja, watu watachukua hatua mikononi ipo siku tuu.
 
Mkuu:

Pamoja na mimi kutumia mtandao, bado nipo-aveleji.

Unajidanganya, Mkuu. Si katika Tanzania ya sasa. Wewe ni mmoja wa wachache sna waliobahatika. Average Tanzanian hata umeme haujui itakuwa huo mtandao? Average tanzanian hatembei kuokoa hela ya daladala. Average tanzanian anatembea kwa sababu hana jinsi. Average Tanzanian hajui hata rangi ya passport. Average Tanzanian anaishi kwenye sub-standard housing. Anaishi kwenye nyumba aliyojenga mwenyewe kwa mikono yake au kupanga chumba kwenye nyumba isiyo na siling, umeme, maji, madirisha na haijapakwa rangi!
 
You are missing the point.

Vinginevyo ukija na "amepata wapi hela mshahara wake tunaujua" unakuwa unaishi maisha ya kizamani ya Kinyerere, ya kutegemea mshahara.

Si ndiyo hayo tunayowasema watoto wa Nyerere hawako competitive?

You just proved my point.
kama hauishi kwa kutegemea mshahara ndio tunarudi kulekule kwamba wewe ni fisadi kama huwezi kujustfy hela yako umepataje....
tunavyojuwa watoto wa viongozi sio competitive wengi wao wanamilikisha mfano kiwira, ubungo ......

kama wewe ni enterprising weka biashara unayofanya... kuiweka JF hamna tofauti na kuitangaza na kama biashara yako haitangazwi(marketing) basi sio biashara bali nyoka
kutegemea mshahara sio maisha ya kizamani ndio maisha ya ukweli na ndio maisha ya asilimia kubwa dunia kote....

naona umejaribu kutumia maneno kama competitive, kizamani, kinyerere, kutegemea mshahara ili kutaka ku justfy maelezo yako, jaribu njia nyingine......
 
Afu leo Ni Bethidei ya Mwalimu. Tungekuwa North Korea, tungeenda kuweka maua kwenye kaburi la kiongozi mkuu na mpendwa.
 
Familia ya Nyerere ni nani kabaki? Madaraka ndie spokesman sasa hivi ambae nae amesha anza kupoteza gololi.

Madaraka anasema Baba yake ni mpenda amani ambaye angekuwepo angeshamsamehe Amini. Baba yake si mtu wa kusamehe maadui, hakwenda hata kwenye msiba wa Kambona, mpaka Makongoro akaona aibu akaenda.

Madaraka anatoa misahama kwa waanzilishi wa vita vya Kagera eti kwa vile ni mambo yalitokea zamani. Anadhani vile ni vita kati ya baba yake na Amin. Watu wamekufa kwa ajili ya kutetea nchi, na kwa kuheshimu siasa na matakwa ya Amiri Jeshi Mkuu. Havikuwa visa vya wanaume wawili kugombea kimada vile.

Lakini sitegemei Madaraka awe amerithi na kujifunza mengi kutoka kwa baba. Ameiambia BBC kwamba Nyerere alikuwa anawafunga midomo kujadili maswala ya kazi yake na siasa wakiwa kwenye meza ya chakula. Madingi wetu wa Kibongo tena, mambo ya kazi ni mambo ya kikubwa. Watoto hakuna kuuliza uliza mambo ya kikubwa.

Makongoro nae alishaanza kupoteza gololi kwenye pombe, akarudi CCM. John anaumwa, kafungiwa ndani maisha yake yote. Magige mwanakijiji Butiama ambako hata radio signals hazifiki, hayuko in touch na nini kinaendelea duniani. Rosemary na Mama Maria wanawasikiliza Madaraka na Makongoro, mfumo dume.

Anaefuatia, ambae bado hajapoteza goroli pale, ni Butiku. Lakini Butiku nae hawezi kujifanya kama ni mtoto wa Nyerere, inabidi aende ende na kina Makongoro wanavyotaka, japo siku zote kina Makongoro walikuwa hela yao ya kula anaishika Butiku, Kambarage hakuwa na muda na watoto. Sasa kwa Butiku, Makongoro hawezi kuwa mtu huru, alishahongwa hongwa fadhilia na Mkapa, mlezi wa familia. Mkapa ana bifu la damu na Butiku, maana Nyerere alipokufa Mkapa akawaweka pembeni watu wa Nyerere, Butiku hakupenda, akaona huyu afisa wa mambo ya nje asiye na jina tumempandisha kwenye magari ya wazi kumuuza Tanzania nzima leo hanisikilizi? Akamwita Mkapa fisadi hadharani. Kumbe Mkapa aliwahi kumnunua mmoja wa familia akijua atamhitaji mbeleni. Mgawanyiko. Makongoro na Mkapa na Butiku na Madaraka. Mkorogo wa uongozi pale Butiama.

Duh! Ebana eeeh...that is some serious name-dropping....
 
Last edited by a moderator:
Afu na wewe mshikaji wake sijuhi unampa ushauri gani. Jina la baba yao kama trade mark ya Coca-cola. Yaani sijuhi wanashindwa nini kutumia hile brandy.
Zakumi,
Unfortunately mimi siko nyumbani. Kwa hiyo ushauri wangu unakuwa kama fimbo ya mbali haiui nyoka. But I wish him well, I want him to succeed and I believe this time he has his head in the right endeavour.
 
Mtoa mada nakushukuru umetukumbusha vitu ambavyo wengi tunasahau. Misingi ya uongozi ayolifuata Nyerere haikuwa ya kifisadi ndiyo maana ukifuatilia watoto wake karibu wote wanaishi maisha ya kuhangaika tu. Sitegemei watoto wa AL au RA watakuja kuishi maisha hayo kwani baba zao wameshawakusanyia za kifisadi za kutosha.

Kwa hilo napa TANO Mwalimu.

Cha kusikitika hapa nimekutana na Andrew Two Months ago, nilivyotambulishwa kwa kweli nilisikia uchungu sana, amekua akiishi Maisha ya Taabu sana pale msasani, ukipita anakuomba Tshs na akishapata hiyo kidogo basi anapotelea kwenye gongo ili kujifariji na kupunguza mawazo.

Hiyo hali imempelekea hadi anakuwa kama kichaa akishakunywa. Na ameteseka kwa muda mrefu bila msaada. Hivi sasa angalau Serikali imemkumbuka wameamua kumchukua na kumpeleka pale Kijitonyama kwenye Hospital ya Usalama ndimo anaishi na kula na kulala. Ukienda utamkuta pale anazunguka zunguka na ni humble kuliko unavyofikiri.

Swali je ule mfuko sijui Foundation ya Mwal. Nyerere inamsaidia nani? Watoto wake hawausiki??????
 
... watoto wake karibu wote wanaishi maisha ya kuhangaika tu.

Kwa hilo napa TANO Mwalimu.

... ukipita anakuomba Tshs na akishapata hiyo kidogo basi anapotelea kwenye gongo ili kujifariji na kupunguza mawazo.

... ni humble kuliko unavyofikiri.

Unataka kumsafisha Andrew kwa kusema eti anakunywa kupunguza mawazo. Mlevi ni mlevi tu.

Na huwezi "kumpa tano" Mwalimu kwa kulea watoto walevi wasio mwelekeo ambao yeye ndie amechangia.

Moja ya sababu ya kwa nini baadhi ya watoto wa Mwalimu wametokea walivyo ni kwa sababu Mwalimu hakuwa na muda na watoto. Hata mahitaji yao walikuwa wanaenda kumwona Butiku. Hela ya shule unaenda kuchukua kwa Butiku. Mzee mwenyewe alikuwa too busy na nchi. Sasa kawaida unapopeleka mahitaji yako ya shule kwa mzazi pengine huo ni wakati mzuri wa kuongea nae kuhusu maendeleo yako na kadharika. Hawa Butiku hakuwa Baba yao, wasingeweza kumueleza yaliyo moyoni, yanayowasibu.

Ndio maana walipungukiwa upendo wa Baba hawa watu, wakaghafirika, wakawa frustrated kabisa.

Sasa tusimpe tano Nyerere, wala tusisafishe walevi, eti walikuwa wanapunguza mawazo.

Tanzania utapata waandishi feki watakwambia Andrew wa Nyerere ni mtoto mnyenyekevu. Lakini hakuna atakae andika kwamba ni mlevi wa kuokotwa na kutunzwa Kijitonyama na Usalama wa Taifa
 
Afu leo Ni Bethidei ya Mwalimu. Tungekuwa North Korea, tungeenda kuweka maua kwenye kaburi la kiongozi mkuu na mpendwa.

Mjamaa Mpotevu kwenye hii sikukuu yake ya kuzaliwa sisi tupo Nkrumah Hall tunamuenzi kwa maua ya fikra yakinifu na tafakuri jadidi, pata dondoo za nini kinachojiri hapa: MICHUZI
 
kama hauishi kwa kutegemea mshahara ndio tunarudi kulekule kwamba wewe ni fisadi kama huwezi kujustfy hela yako umepataje....
tunavyojuwa watoto wa viongozi sio competitive wengi wao wanamilikisha mfano kiwira, ubungo ......

kama wewe ni enterprising weka biashara unayofanya... kuiweka JF hamna tofauti na kuitangaza na kama biashara yako haitangazwi(marketing) basi sio biashara bali nyoka
kutegemea mshahara sio maisha ya kizamani ndio maisha ya ukweli na ndio maisha ya asilimia kubwa dunia kote....

naona umejaribu kutumia maneno kama competitive, kizamani, kinyerere, kutegemea mshahara ili kutaka ku justfy maelezo yako, jaribu njia nyingine......

Ni hivi, ulimwengu wa sasa unaenda na investment, kuna mambo ya stock market, kuna real estate, kuna biashara kibao.Simtetei mtu, lakini ukiuliza swali la kipindi cha mikingamo ambalo lilikuwa valid 1984 wakati kila mtu channel zake zote zilikuwa zinajulikana na kila mtu, kuuliza hili swali la amepata wapi kama msingi wa kumshuku mtu ufisadi inakuwa ni kijiba cha roho tu.

Sema kama unajua fisadi, peleka isue mahakamani au kwenye tume ya maadili, au hata hapa JF andika unachojua kuhusu ufisadi wa mtu.

Kusema mtu fisadi kwa sababu anaendesha BMW next mtu mbeba box atakuja nyumbani na sneaker zake za $200 ataambiwa anauza bwimbwi.Nakataa kumsema mtu fisadi just because ana hela, nakataa kumuuliza mtu umepataje hela (nje ya settings nilizotaja hapo juu, mahakamani, kwenye tume ya maadili etc).

Fisadi hana wajibu wa kujionyesha kwamba yeye si fisadi, wewe unayemsema kwamba huyu ni fisadi ndiye una burden of proof ya kuonyesha kwamba huyu ni fisadi.

Ndiyo maana mnawapa misemo senile bulldogs kama kina Makamba, hili neno fisadi linakuwa cheapened into a cliche siku hizi.

Kumkoma nyani giladi, no data no right to speak.
 
I thank god for this exceptional mtumishi julius k.nyerere, from now onwards nitasali na kumsifu mungu kwa ajili ya kutuonyesha bin- adamu julius k.nyerere.

Inawezekana , tutimize wajibu wetu kwa jamii na mungu kwa uaminifu. Amen
 
Unataka kumsafisha Andrew kwa kusema eti anakunywa kupunguza mawazo. Mlevi ni mlevi tu.

Na huwezi "kumpa tano" Mwalimu kwa kulea watoto walevi wasio mwelekeo ambao yeye ndie amechangia.

Moja ya sababu ya kwa nini baadhi ya watoto wa Mwalimu wametokea walivyo ni kwa sababu Mwalimu hakuwa na muda na watoto. Hata mahitaji yao walikuwa wanaenda kumwona Butiku. Hela ya shule unaenda kuchukua kwa Butiku. Mzee mwenyewe alikuwa too busy na nchi. Sasa kawaida unapopeleka mahitaji yako ya shule kwa mzazi pengine huo ni wakati mzuri wa kuongea nae kuhusu maendeleo yako na kadharika. Hawa Butiku hakuwa Baba yao, wasingeweza kumueleza yaliyo moyoni, yanayowasibu.

Ndio maana walipungukiwa upendo wa Baba hawa watu, wakaghafirika, wakawa frustrated kabisa.

Sasa tusimpe tano Nyerere, wala tusisafishe walevi, eti walikuwa wanapunguza mawazo.

Tanzania utapata waandishi feki watakwambia Andrew wa Nyerere ni mtoto mnyenyekevu. Lakini hakuna atakae andika kwamba ni mlevi wa kuokotwa na kutunzwa Kijitonyama na Usalama wa Taifa

Dillunga, again....Sio kwamba kila ulichosema ni sahihi,lakini ukweli ni kwamba,kwenye upande wa familia mwalimu alichemsha na ni watu wengi sana waliiga mifano yake na ndio maana Taifa liko hivi lilivyo,alitaka watanzania ndio wawe familia yake...Sasa unadhani watu kama kina Andrew wako wangapi bongo? Ama kwasababu tu ni mtoto wa Nyerere? Hakuna cha ajabu sana hapo,mbona ni maisha ya watu wengi tu yako hivyo? Mwalimu tutampa credits zake pale inapostahili na pale pa ku criticize tutafanya the same...Kwenye upande tunaozungumzia hapa alichemsha na matokeo yake ni sisi kama Taifa na si tu familia yake.
 
Last edited:
capt.john ambaye wanasema hapa amefungiwa msasani au kijitonyama [UT] ..pia ni jet fighter pilot.........
 
Back
Top Bottom