Ande'ngenye akiri kuwa maandamano yaliruhusiwa arusha

Mfamaji

JF-Expert Member
Nov 6, 2007
6,631
1,926
Katika mahojiano yaliyofanyika leo na Magic Fm, Kamanda wa polisi arusha amekiri kuwa maanadamo yaliruhusiwa na walikaa kikao na viongozi wa CDM kupanga njia yatakayopitia.

Anasema kasoro ni viongozi wa CDM hawakurudi kukonfirm njia walizopendekeza polisi akiamini kuwa hizo njia zingefanya mji usimame. Eti walipata taarifa za Kiinteligensia kuwa vurugu ingetokea kwa hiyo wakasitisha maandamano kwa njia ya vyombo vya habari.

Anakiri taarifa ya maandamano ilitolewa mapema na ilikubaliwa na jeshi lake .

MY TAKE.
Wakuu hebu angalieni hii kauli na kitendo walichofanya Polisi cha kuuwa watu na kuwapeleka viongozi wa CDM mahakamni kwa kosa la kuandamana kinyume cha sheria . Haiingii kichwani kabisa , na hata mwenyewe alikuwa anajikanyaga kuelezea hali ilivyokuwa hadi akatoa amri ya kutumia nguvu na risasi kuuwa watu.

Kweli inasikitisha Kamanda mzima hajui wajibu wa jeshi la Polisi. Kama walipata taarifa za kiinteligensia mbona hawakuongeza polisi ili kuhakikisha hazitokei badala yake wakawakamata viongozi na kupiga mabomu mji mzima hovyo hovyo?

HE must face ICC.
 
mkuu... hawa jamaa tusihangaike ICC mbona kuna Sangoma technology...... muda mfupi tu utamkuta anaosha magari pale billicanas
 
mkuu... hawa jamaa tusihangaike ICC mbona kuna Sangoma technology...... muda mfupi tu utamkuta anaosha magari pale billicanas


Umenikumbusha yaliyompata Ditopile.
 
Mimi ningewashangaa watu wa serikalini na polisi kama wangekuwa bayana kujikosoa kwamba wao ndio chanzo cha vurugu na mauaji Arusha. in Jungle laws, inajulikana kwamba kuna sheria kuu mbili zinazotawala:
  1. Mkubwa hakosei ng'o!
  2. Na kama utagundua kuwa mkubwa kakosea ujue maana yake ni moja tu, yaani rejea sheria ya kwanza: Mkubwa HAKOSEI.
 
Ndio madhara ya u-puppet haya.

Sasa aeleze kwanini sheria isichukue mkondo wake dhidi yake.
 
Andengenye!

Jiuzulu kazi!...damu ya waliopoteza maisha inakulilia wewe na mabosi waliokutuma!
 
Back
Top Bottom