Anayetuhumiwa kumteka DR. Ulimboka azungumza

18.JPG


Askari anayetuhumiwa kumteka Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk. Stephen Ulimboka, Kamishna wa Polisi Msaidizi (ACP), Ahmed Msangi, amehojiwa na kuzungumzia kilichotokea kuhusiana na tuhuma kwamba aliambiwa arejeshe simu ya mkononi na pochi ya Dk. Ulimboka.


Akizungumza na Gazeti la JAMHURI, ACP Msangi alikiri kwenda katika wodi ya wagonjwa mahututi katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) kwa nia ya kumhoji Dk. Ulimboka, ila akaeleza mshangao wake kutokana na habari zilizochapishwa mwishoni mwa wiki, kuwa aliambiwa arejeshe pochi na simu ya Dk Ulimboka kwa maana kuwa alivipora walipomteka.


Vyombo vya habari mwishoni mwa wiki vilichapisha taarifa bila kutaja jina la askari anayetuhumiwa, lakini pia ukawa unasambazwa ujumbe mfupi kupitia simu za mkononi ambao ulisema hivi:


“Kamanda Msangi aliyemkamata na kumtesa Dr. Ulimboka, yuko katika jopo la kuchunguza nini kilimtokea Dk. Ulimboka. Alipofika kumhoji Dk. Ulimboka alimwambia ‘Nirudishie simu na wallet yangu’. Kamanda Msangi taratibu akaondoka wodini kichwa chini. Kama wewe ni mpenda haki na unapinga ujinga na dhuluma, watumie ujumbe huu watu wengi kadri uwezavyo ili wamjue dhalimu aliyeongoza unyama huu,” ulisema ujumbe huo unaosambazwa kupitia simu za mkononi.


Tume ya Jeshi la Polisi iliyoundwa kuchunguza tukio la Dk. Ulimboka kutekwa nyara, kwa mujibu wa Kamanda Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, inaongozwa na Kamanda Msangi.

Kamanda Msangi azungumza

Jamhuri: Afande umetangazwa kuongoza hii Tume ya Polisi kuchunguza suala la Dk. Ulimboka, lakini taarifa zilisosambaa zinaonyesha Ulimboka alikwambia umerejeshee simu na wallet yake. Unalizungumziaje hili?

Kamanda Msangi: Hata mimi nimesikia hizi taarifa, na zimenisikitisha mno. Naamini taarifa hizi zina malengo ya ziada. Si kweli kwamba nilishiriki kumteka Dk. Ulimboka na wala sijawahi kuwa na wazo hilo.

Jamhuri: Ikiwa hukushiriki kumteka iweje wodini akwambie nirudishie simu yangu?


Msangi: Kwanza ifahamike mimi huyu Dk. Ulimboka na mwenzake Dk. Deo nimewafahamu siku nyingi sana. Kwa maana hiyo ni mtu anayenifahamu vizuri tu. Kuna upotoshaji wa makusudi umefanywa ambao mimi nadhani una msukumo wa kisiasa.


Alichosema Dk. Ulimboka nilipozungumza naye, ni kwamba simu moja ilidondoka, nyingine wale watu waliomteka wameichukua pamoja na wallet yake. Hivyo alikuwa ananitajia vitu vilivyopotea. Nilipomuuliza iwapo anakumbuka namba ya simu, aliniambia nikamuulize Dk. Deo. Sasa nashangaa mtu aliyepenyeza uongo huu kwamba alisema mimi ndiye niliyempora hivyo vitu… sielewi ni nani na ana malengo gani.

Jamhuri: Haya unayasema wewe, hivi unadhani jamii itakuamini kwa kauli hizi, haitaonekana unajitetea tu?

Msangi: Wakati anazungumza maneno haya, alikuwapo Profesa Museru ambaye ni Mkurugenzi wa MOI. Sina cha kuficha kamuulize tu, atakwambia alichosema Dk. Ulimboka. Yupo pia Dk. Deo, huyu ananifahamu na Dk. Ulimboka anasema walikuwa wote wakati anatekwa. Dk. Deo ananifahamu, akaulizwe iwapo mimi ndiye niliyemteka Dk. Ulimboka.

Jamhuri: Tuhuma hizi zilianza kusambaa mapema tu Ijumaa. Je, wewe hukuwa na hofu kwenda pale MOI kumhoji Dk. Ulimboka?


Msangi: Ndugu yangu, nchi hii ina askari wengi mno. Hivi mimi kwa akili ya kawaida naweza kushiriki kumteka Dk. Ulimboka kisha nikaenda wodini kumhoji? Hata katika akili ya kawaida ya binadamu hilo haliwezekani.


Jamhuri: Hizi tuhuma zilizoelekezwa kwako ni nzito. Wewe ndiye uliyeteuliwa kuongoza Tume ya Uchunguzi wa tatizo hili. Je, unadhani uchunguzi utakaofanya utaaminiwa na wananchi ukitoa ripoti?

Msangi:
Mimi ninachokuhakikishia sikushiriki kumteka na si kweli kwa kila hali. Mambo kama haya yanakatisha tamaa. Kama tunaanza kuzushiana uongo kwa kiwango hiki, nchi hii sijui inaelekea wapi! Kimsingi imenikatisha tamaa mno. Wapo wanaosema nijiuzulu katika Tume hii lakini mimi nasema wakubwa wangu wamenipa kazi hii na watakaloamua nitalipokea.

Hivi wewe gazeti lako likituhumiwa unaacha kuendelea kutafuta habari? Nitaendelea kufanya kazi hii kama nilivyoapa siku nilipohitimu mafunzo kwamba nitalitumikia taifa kwa uadilifu na uaminifu wa hali ya juu katika kiapo changu cha utii. Na hilo ndilo nitakaloendelea kufanya. Watu wanapenda kuharibiana maisha tu.

Profesa Museru asema alichokisikia


Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru, akizungumza na JAMHURI kuhusiana na sakata kwamba Dk. Ulimboka, alimweleza Kamanda Msangi arejeshe simu na wallet yake.

Jamhuri: Profesa nimezungumza na Kamanda Msangi juu ya tuhuma zinazomkabili kuwa aliambiwa na Dk. Ulimboka amrejeshee simu na wallet yake, na akakutaja wewe kuwa ulikuwapo wakati wa mazungumzo hayo. Wewe nini ulichokisikia kuhusiana na tuhuma hizi.

Profesa Museru: Mimi ndiye niliyempeleka pale wodini. Ni bwana mzuri tu. Nilimu-introduce (nilimtambulisha), akaanza mahojiano. Mimi hilo sikulisikia kwamba ameambiwa arejeshe simu na wallet, hilo sikulisikia.

Jamhuri: Kuna habari kuwa Kamanda Msangi baada ya kuambiwa kauli hiyo alitoweka wodini bila kuaga akikwepa kipigo kama ilivyomtokea askari mwenzake siku mbili kabla. Je, unalizungumziaje hilo profesa?

Profesa Museru: Nini? Kwamba alikimbia? Jamani nchi hii inakwenda pabaya. Mimi nilimsindikiza hadi nje ya wodi akapanda gari lake na kurejea ofisini kwake, sasa hilo la kukimbia limetokea wapi? Jamani ehee, mimi niseme katika hali kama hii sintofahamu zipo nyingi. Ni vyema kuchuja taarifa tunazozipata.

Daktari asisitiza polisi wanahusika

Gazeti la JAMHURI lilichukua jukumu la kumtafuta mmoja wa viongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, ambaye kwa sababu za kiusalama alikataa jina lake lisitajwe gazetini, lakini yeye alisisitiza kuwa polisi wanahusika na utekaji huo kwa asilimia 100.


“Hivi unategemea leo Kamanda Msangi kwa akili ya kawaida ya binadamu anaweza akakiri kuwa alishiriki kumteka? Taarifa tulizonazo ni kwamba polisi ndiyo waliomteka Dk. Ulimboka na kumfanyia unyama huu.

“Ndiyo maana tunasema polisi tayari wanatuhumiwa hivyo hawana haki ya kuchunguza suala hili. Tunataka ateuliwe Jaji, na Tume iwe na wajumbe huru wasiofungamana na chama, taasisi au siasa za nchi hii, wachunguze kwa kina na kutoa taarifa huru,” alisema Daktari huyo.


Alisema mbinu iliyotumika kumtesa Dk. Ulimboka hutumiwa na majasusi wenye mafunzo ya hali ya juu, ambayo hata majambazi wa kawaida hawawezi kuzifahamu.


“Unapomg’oa mtu kucha au jino bila kumpiga ganzi, unashtua mishipa ya fahamu kumfanya anayeteswa afahamu kuwa kinachofuatia dhahiri ni kifo, na hivyo kulazimika kusema ukweli wote anaojua juu ya suala analohojiwa. Mtu akishang’olewa jino au kucha na asiseme chochote, basi unajua fika kuwa hakuna anachokifahamu zaidi ya alichokisema.


“Hii inatokana na nini? Hicho kinatokana na ukweli kwamba baada ya kung’olewa kimojawapo kati ya hivyo, kinachofuata ni kupoteza fahamu. Sekundi chache kabla ya kupoteza fahamu nati za mishipa ya fahamu huwa zinafunguka na kusema kila kilicho cha kweli bila wewe unayeteswa kujua. Ndiyo maana nasema vyombo vya dola ndivyo vilivyohusika. Haya ni mateso ya kitaalamu,” alisema daktari huyo.


Rais wa Chama cha Madaktri Tanzania, Dk. Namala Mkopi, alipopigiwa simu na JAMHURI kueleza chochote anachokifahamu katika sakata hili, alipokea simu akasikiliza kisha akakata bila kujibu na hata alipopigiwa simu tena hakutaka kuipokea tena.

Dk. Ulimboka apelekwa nje kwa matibabu

Madaktari inaelezwa kuwa wameamua kumpeleka Dk. Ulimboka katika matibabu nchini India, ingawa kwa sababu walizosema ni za kiusalama hawakutaka kutaja ni hospitali gani aliyopelekwa.


Jumanne wiki iliyopita, Dk. Ulimboka alitekwa na watu wasiofahamika hadi sasa na kupigwa, akang’olewa meno mawili na kucha mbili, kisha akatupwa katika msikiti wa Mabwepande baada ya kuwa ameteswa kupita kiasi.


Dk. Ulimboka baada ya kuokotwa na wasamaria wema, alikaririwa na Radio Clouds akisema kuwa walipokuwa Kinondoni ndipo alipotekwa usiku wa saa 5:30.


"Mara, katikati ya maongezi tukaona mtu anaongea na simu. Ghafla tukiwa tunasema tuagane, wakaja watu kama watano hivi na bunduki, wakasema wewe na yule bwana mko free (huru), tunakuchukua wewe (Dk. Ulimboka)," alieleza na kuongeza.


"Sijakaa sawa, nikaona nimeshaburutwa nikaanguka kwenye lami, wakaniinua na kuniingiza kwenye gari nyeusi, lakini ilikuwa haina namba."

Wananchi wataka uchunguzi huru

Baadhi ya wananchi waliozungumza na JAMHURI huku wakionyesha hofu ya kutaja majina yao, walilituhumu Jeshi la Polisi kuwa linahusika moja kwa moja na tukio hili hivyo wakuu wa jeshi hilo wawajibike kuhakikisha ukweli unapatikana.


“Ndugu yangu nawahurumia nyie wenye kutafuta habari hizi. Mnafanya kazi ya hatari. Tutazidi kuwaombea tu, muishi milele na Mungu awalinde. Hivi leo kwa mfano unaweza kwenda kumhoji Msangi kuwa unatuhumiwa kumteka Dk. Ulimboka? Ukitoka hapo anatuma vijana wake nao wanakuteka na wewe pia.

“Naamini polisi walihusika kwa kiwango kikubwa na hivyo hawapaswi kushiriki uchunguzi huu. Hawa wanapaswa kupanda kizimbani kujitetea hivyo ni makosa kushiriki uchunguzi wao,” alisema Mkazi wa Dar es Salaam.


Mwananchi mwingine alisema chimbuko la mgogoro wa madaktari liko wazi. “Hawa wanadai mishahara mizuri na marupurupu sawa na wanavyopata wabunge wasiofanya kazi yoyote. Leo unadhani serikali inaona imeshikwa pabaya itawaacha waendelee kutamba tu? Thubutu. Kimsingi polisi wametumiwa. Hao waliowatumia ndiyo tunaotaka uchunguzi huru utueleze ni kina nani na kwa nia ipi,” alisema Mkazi wa Arusha kwa njia ya simu.


Hadi sasa madaktari katika hospitali za umma wamegoma kuendelea na kazi kutokana na mgogoro wa malipo kati yao na serikali, na hivi karibuni mgogoro huo umeshika kasi baada ya Dk. Ulimboka kutekwa na kuumizwa vibaya.

Chanzo: Gazeti la Jamhuri Jumanne, Julai 03, 2012

Sijawahi kuliamini hili gazeti (JAMHURI) na wala haitatokea siku nikaliamini gazeti lolote la magamba.
 
Msangi is a crook but he aren't that dumb
Pamoja na kwamba kiingereza sahihi ni he aint that dumb, naomba nikuulize japo kaswali kadogo tu...since when are crooks never dumb? Gaijin, to make the claim that ACP Msangi aint dumb, you got to be either his boss, his colleague, his mentor, his wife, his doctor(psychiatrist)? or whatever...which are you? FYI hayo majibu yake pekee yanaonesha how dumb he is and if anything, his interview with a third-rate slangy newspaper by the name of Jamhuri, has exposed him for what he really is, a crooked lousy cop.

dumb-crooks-logo.gif
 
Wakati umefika kwa Tanzania kuanza kuwekeza kwenye CCTV katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu, kama Leaders Club, and Stereo kungekuwa na CCTV ingekuwa rahisi kuwatambua waliomteka Dr. Ulimboka, maana CCTv ingeonesha watu aliokutana nao na hivyo yeye kuonyesha ni yupi aliyemteka nyara.

Kwa mazingira ya ‘organise crime of that nature’ CCTV ingeweza kutoa kutoa mwanga kuelekelza upelelezi. Ni muhimu sasa katika ameneo kama Clubs, restaurants, Hotel, hospitali, schools, maduka makubwa na hata ofisi za serikali tukaweka CCTV.

Kabla ya Dr. ulimboka kutekwa nyara taarifa zinaonyesha kuwa mtekaji alikuwa akiwasiliana kwa simu na wenzake, kama tunaweza kujua mahali alipokuwa Dr. Ulimboka ‘Forensics Technology’ inaweza kutumika kujua simu za karibu na aliposimama Dr. Ulimboka, na kwa kuwa sim cards Tanzania zinakuwa registered basi hii inaweza kutoa mwanga kwa kuelekea katika upelelezi, aidha simu ya Dr. Ulimboka imepotea kalini number yake inajulikana, hiyo Operator wa number yake atoe muhutasari wa simu zilizopigwa na kupiga katika simu ya Dr. Ulimbika na kasha kwa kutumia special software inawezekana kufanya forensics analysis kujua namba ya aliyempigia Dr. Ulimboka na kupanga kukutana na hiyo kuitafuta ni simu ya nanai.

Aidha Dr. Ulimboka ahojiwe na facial mapping specialist ambao kwa kutumia taarifa zake to map possible look of the suspects and using special software to generate possible images and circulate to public domain kuwatambuka.

If Tanzania do don’t have this kind of expertise (which I wonder if Mr Mwema hold the expertise as they could be on top of the game of the cybercrime) they can ask for assistance from this side of the world, definitely they will be happy to help and spread the words of what the technology can offer.

Tanzania needs to change and embrace full the advantage of the technology to make life better and easy to everyone including law enforcement agencies. It is the use technology in a forensics will allow government to come clean from conspiracy theory.
 
Duniani sheria itapindindishwa ila mbimguni haki itatimizwa. Tujifuze kuhesabu siku zetu za kuishi.km msangi na hao wengine waliomtesa dr ulimboka munadhani mutaishi milele mumesave
 
Kamanda Msangi fanya kazi yako kwa mujibu wa sheria kama walikataa matibabu ya serikali wakati MOi ni ya serikali unadhani wanaotaka tume huru watasema nini au wataeneza propaganda zipi ili kupotosha ukweli? Polisi wafanye kazi yao kwa mujibu wa sheria maana hata serikali ikiunda tume huru bado haitaaminika anayetaka tume huru aende UN au the Hague. Kwa taarifa ya wanao bwabwaja katika hili hata familia imeanza kujitenga na madaktari wanaotaka umaarufu na wanasiasa na wanaharakaharaka isiyo na baraka wanaotafuta umaarufu na fedha kupitia ndugu yao. Acheni tabia mbaya za uchochezi usiyo na maana.
 
Wakati umefika kwa Tanzania kuanza kuwekeza kwenye CCTV katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu, kama Leaders Club, and Stereo kungekuwa na CCTV ingekuwa rahisi kuwatambua waliomteka Dr. Ulimboka, maana CCTv ingeonesha watu aliokutana nao na hivyo yeye kuonyesha ni yupi aliyemteka nyara.

Kwa mazingira ya ‘organise crime of that nature’ CCTV ingeweza kutoa kutoa mwanga kuelekelza upelelezi. Ni muhimu sasa katika ameneo kama Clubs, restaurants, Hotel, hospitali, schools, maduka makubwa na hata ofisi za serikali tukaweka CCTV.

Kabla ya Dr. ulimboka kutekwa nyara taarifa zinaonyesha kuwa mtekaji alikuwa akiwasiliana kwa simu na wenzake, kama tunaweza kujua mahali alipokuwa Dr. Ulimboka ‘Forensics Technology’ inaweza kutumika kujua simu za karibu na aliposimama Dr. Ulimboka, na kwa kuwa sim cards Tanzania zinakuwa registered basi hii inaweza kutoa mwanga kwa kuelekea katika upelelezi, aidha simu ya Dr. Ulimboka imepotea kalini number yake inajulikana, hiyo Operator wa number yake atoe muhutasari wa simu zilizopigwa na kupiga katika simu ya Dr. Ulimbika na kasha kwa kutumia special software inawezekana kufanya forensics analysis kujua namba ya aliyempigia Dr. Ulimboka na kupanga kukutana na hiyo kuitafuta ni simu ya nanai.

Aidha Dr. Ulimboka ahojiwe na facial mapping specialist ambao kwa kutumia taarifa zake to map possible look of the suspects and using special software to generate possible images and circulate to public domain kuwatambuka.

If Tanzania do don’t have this kind of expertise (which I wonder if Mr Mwema hold the expertise as they could be on top of the game of the cybercrime) they can ask for assistance from this side of the world, definitely they will be happy to help and spread the words of what the technology can offer.

Tanzania needs to change and embrace full the advantage of the technology to make life better and easy to everyone including law enforcement agencies. It is the use technology in a forensics will allow government to come clean from conspiracy theory.

And it is unfortunate that the same suspects are in control of forensic technology!
 
Mitazamo inatofautiana, mimi nilichoelewa ni kwamba Askari wako wengi hivyo angetumwa kiongoz mwingine kuchunguza suala la Dr badala ya Ahmed Msangi. Pia Askari wako wengi hivyo angeteuliwa kiongozi polisi mwingine kwenda kuongea na Dr Uli badala ya Msangi iwapo angekuwa anahusika. Wewe mimi nakufahamu ndo maana nimekujibu hapa. Kwani wewe ulipozzushiwa kuwa ni shoga ukaja kwangu kuniomba ushauri wa jinsi gani ujisafishe ktk jamiii ina maana ilikuwa kweli?
 
HAya ndo mambo ya nchi hii kwa miaka mingi. ubaya tunakumbuka ya jana tu!
 
Back
Top Bottom