OSOKONI
JF-Expert Member
- Oct 20, 2011
- 10,965
- 5,336
Katika hali ya kawaida na ustaarabu huyu Msangi maadamu ameshatajwa kuhusika na habari zimesambaa sana na zimekaa kwenye mioyo ya watu basi angejiondoa kwenye hii tume ili tume iwe huru! maana kwa sasa ripoti ambayo itakubalika na jamii ambayo Msangi ataitoa ni kama akisema polisi walihusika lakini akisema hawakuhusika hakuna mtu ataamini hata kama kweli hawakuhusika! Serikali nayo kwa upande wake kama kweli haikuhusika na inataka kujisafisha iundwe tume huru isihusishe polisi wawepo majaji madaktari na wanancchi wengine wanaoaminiwa na jamii! Lakini hii jeshi la polisi na serikali kung,angania kuchunguza wakati wao ni watuhumiwa nambari moja ni sawa na kuoga na matope !!!