Elections 2010 Anayetaka kumwaga damu akamatwe mara moja

QUALITY

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
853
115
ANAYETAKA KUMWAGA DAMU AKAMATWE MARA MOJA
Hii ni kauli iliyotolewa juma moja lililopita baadaa ya Mnajimu wa JWTZ kujitokeza na kusema kuwa kuna wanasiasa wanataaka damu imwagike ili mradi waingie madarakani.

Dr. Slaa alitoa kauli kali kuwa yule anayetaka kumwaga damu, akamatwe mara moja na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria. Kimya… Kimya… Mpaka tunavyongea leo hakuna mtu hata mmoja ambaye amekamatwa kwa kujihusisha na suala la damu kumwagika. Maana yake ni nini?

  1. Hakuna aliyesema au aliyeonesha hisia za kumwaga damu
  2. ulikuwa ni uzushi kuwatisha wapiga kura
  3. Sera zimeisha na hivyo imebaki kutapatapa.

Lakini kwanini kutapatapa namna hii? Kama watanzania wameamua kufanya mabadiliko, na hawaungi mkono CCM, suala siyo kupaniki bali ni kutulia na kuendelea na kampeni mpaka situ ya uchaguzi. Kama CCM ikishindwa, ikubali na wasikate tamaa maana hii ni nchi ya watanzania wala siyo ya CCM wala CUF wala CHADEMA. Watanzania wanaipenda Tanzania ila wamemchoka Kikwete na CCM yake. Apumzike, yumkini akija kugombea tena yeye au mwingine kupitia CCM, ataweza kushinda.

Hiyo ndiyo itendeleza amani na utulivu.

Siku njema :rain:
 
Kwa uzoefu wangu kwa wanaojua kampeni zilizokwishapita walikuwa wanaweka video za mchafuko yaliyotokea huko nchi jirani hivyo hizi nazo naziita mbinu chafu kwa mtu mwenye kuitakia amani tanzanzania you can't wish bloodshed in your own country!:mad:
 
mwaka huu mashambulizi makali beki hazikabi ndomaana wamepaniki
 
Ukiwa unapigana na mtu halafu gafla unamuona mwenzako anakimbilia mawe ujue kazidiwa..!
 
kazi kwelikweli, watu wanajua kuwa vyama vya upinzani si vita. tafuteni na fikirini njia nyingine ya kumchafua Slaa na Lipumba!
 
kama kweli yupo, mbona hakamatwi? au wanamwogopa kama wanavyowaogopa mafisadi?
 
Back
Top Bottom