Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Huwezi kusema tunataka nchi ya viwanda. Kuna maswali lazima ujiulize.
Mosi,viwanda vipi? Processing(usindikaji) au vya aina gani?.
Pili,unatumia rasimali fedha,watu nk ( resources) zipi,kiasi gani za aina gani?
Tatu,kuna nishati ya umeme ya uhakika? Kama haipo,una mikakati gani?.
Nne,mtawanyiko wa viwanda utakuwa wa kisoko,ki-malighafi au kijiografia?.
Tano,nchi zilizoendelea,zimeendelea kwa sababu ya viwanda au zina viwanda kwa sababu zimeendelea? Swali la msingi.
Mtoa mada asipuuzwe,wanaopingna na mtoa mada waninjibu maswali haya kwa umakini,kama huna majibu ni dhahiri kuwa taifa halina dira wala kiongozi hana maono. Msitukane mtoa hoja
Tatizo tu nazungumzia viwanda wakati tunategemea Mchina ndiyo aje na hivyo viwanda!!
 
Mwl Nyerere aliwahi kusema "hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya rais au waziri mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida. Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.
Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je? anajua jinsi ya kututoa? Anajua anakotupeleka? Nimejitahidi kuangalia bunge ili nione labda mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi. Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
Tatizo umeshachelewa vichwa vyacwatu vimejaa kauli za magufuli
 
Tatizo tu nazungumzia viwanda wakati tunategemea Mchina ndiyo aje na hivyo viwanda!!
Mkuu ccm imeua elimu yetu na pia akili za watanzania walio wengi. Watanzania tumebakia kushabikia wasemayo wanasiasa,walioko madarakani na wasio madaraka,hatuwezi kufikiria tena, kiukweli inauma sana.Mtu anakaririshwa Tanzania ya Magufuli itakuwa ya viwanda ,then watu wasomi kwa wasio soma kama Mimi tukajitoa ufahamu kushabikia bila hata kujiuliza hivyo viwanda atajenga nani na vile tulivyokuwa navyo vilienda wapi, watu hatuwezi fikiri tena,na hata tukifikiri uwezo wetu unaishia Leo,we can't think about tomorrow na ccm kwa uroho wa madaraka wanaendelea kutudanganya misukule yao, elimu yetu wameua sasa sijui kwa akili zao nani atajenga kiwanda kama si mtanzania? Nani atazalisha malighafi za hicho kiwanda kama si mtanzania, Nani atafanyakazi kwenye hicho kiwanda kama si mtanzania? Je huyu mtanzania anaelimu ya kufanya hayo? Sasa masikini wadanganyika hasa wanaccm wakabaki kukaririshwa tu.I hate ccm
 
Tatizo tu nazungumzia viwanda wakati tunategemea Mchina ndiyo aje na hivyo viwanda!!
Kipaumbele cha Elimu,Elimu,Elimu nilikuwa sahihi sana maana elimu ndiyo huzaa viwanda,malighafi,umeme na mambo mengine ila wadanganyika waliozoea kudanganywa,wadanganyika hawa wasiofikiria kesho yao wala ya watoto wao wakaishia kuimba hapa kazi tu huku wakiwa hawana kazi,Tanzania ya viwanda huku wakiwa hawana elimu hata ya kuwawezesha kupata kazi ya ukarani,Tanzania ya viwanda huku wakiendelea kuvuna kilo 100 hadi 200 kwa ekali moja ya pamba,mahindi nk.Wakati mwingine unaweza ukaona aibu kujitambulisha kuwa ni mtanzania
 
Binafsi nadhani ana nia nzuri.

Lakini sidhani anajua anakoelekea.....

Yupo yupo.

Kudhani ni kudhani tu hakuna mantiki kisayansi kwa sababu unaweza kuwa unasukumwa na kutojua au itakadi mgando au hisia tu, kuache kudhani kubaki kudhani tu. Mwenye kazi yake anajua anakoelekea. Go go JPM. tulia tuli!
 
Napita tu ila tusiwe na tabia kama mashabiki Wa mpira , timu ikisajili mchezaji mpya wanataka aanze kufunga magoli asipofanya hivyo bac utasikia mchezaji gani huyu hafai, ni vyema kwa apewe muda kabla ya kumuona hafai, nilichotaka kusema mapinduzi ya kweli huwa hayaji kiurahisi na huwa hayatoi matokeo on sport.
 
wewendio hujui unaelekea wapi hii nchi iligeuka kichaka cha wezi na mafisadi ndio maana watu watu walifikiri wanaweza kununua nchi kwa pesa zao za ufisadi jiulize hao watu wangechukua nchi wangetupeleka wapi
Mkuu inaonekana unawaamini sana viongozi wako wa ccm?siku ukipata ufahamu jiulize hivi,kama kweli ccm wanaipenda nchi hii hayo majipu tunayoambiwa yanatumbuliwa na magufuli yalitokana na nini? Kwa nini hawataki bunge live,je gharama za kuonesha bunge live ni kubwa kuliko kununua v8 na kulihudumia for one year? Je gharama ya kuonesha bunge live ni kubwa kuliko kufuta kinga ya kutokushitakiwa ya marais wasitaafu?
 
Napita tu ila tusiwe na tabia kama mashabiki Wa mpira , timu ikisajili mchezaji mpya wanataka aanze kufunga magoli asipofanya hivyo bac utasikia mchezaji gani huyu hafai, ni vyema kwa apewe muda kabla ya kumuona hafai, nilichotaka kusema mapinduzi ya kweli huwa hayaji kiurahisi na huwa hayatoi matokeo on sport.
Hatukusema tunataka matokeo on the spot ila mwelekeo. Ili tuyafikie hayo matokeo tunahitaji kuona njia ya kutufikisha huko, ndo maana tunasema tumepotea
 
Kudhani ni kudhani tu hakuna mantiki kisayansi kwa sababu unaweza kuwa unasukumwa na kutojua au itakadi mgando au hisia tu, kuache kudhani kubaki kudhani tu. Mwenye kazi yake anajua anakoelekea. Go go JPM. tulia tuli!

Kudhani ni haki yangu na nitaendelea kudhani na hakuna yeyote awezaye kufanya lolote juu ya hilo.
 
Mbona swali la mleta mada liko linaeleweka ila wachangiaji wengi wamekuja wanatokwa na mapovu wakati ukweli ni kuwa jitihada zote zinazofanywa na mheshimiwa rais lakini hatuoni maboresho yoyote katika hali ya uchumi wa wa Tanzania walio wengi wa hali ya kawaida.
Tuache ushabiki tuongee ukweli.
 
Mkuu shida si wanasiasa,shida ni wadanganyika can you believe watu walewale,chama kile kile ,Sera zile zile wametudanganya for 54 years na bado hatujitanbui.nakuhakikishia Tanzania ya viwanda haiwezekani kama vile maisha bora kwa kila mdanganyika yalivyoshindikana
Ukiwaambia namna hii wanakasilika sana wanaishia kutaja Majina ya watu....unafanya jambo lile miaka yote then unategemea Jipya kama sio upumbavu nini
 
Binafsi uchumi naona unakuwa kwa asilimia 7.1 na tuna wazidi hata wa kenya hivyo basi tukianza kufanya export kwa wingi na import kwa uchache itapelekea hata thamani ya hela kupanda, japo hata sasa ivi hela imepanda, inflation imepungua mpaka asilimia 5.3 mm naona tunaelekea kuzuri, .. kwa sera ya hapa kazi tu.
 
Binafsi uchumi naona unakuwa kwa asilimia 7.1 na tuna wazidi hata wa kenya hivyo basi tukianza kufanya export kwa wingi na import kwa uchache itapelekea hata thamani ya hela kupanda, japo hata sasa ivi hela imepanda, inflation imepungua mpaka asilimia 5.3 mm naona tunaelekea kuzuri, .. kwa sera ya hapa kazi tu.
Uchumi kuanza kukua kwa kasi ni wimbo aliyoanza kuimba Mkapa, JK hadi sasa, nini kimebadilika? Maisha ya watanzania yamebadilikaje kuenda na kukua kwa uchumi?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom