Anayejiita Yesu afyatua risasi Ikulu

MpigaKura

JF-Expert Member
Jan 25, 2007
384
101
Anayejiita Yesu afyatua risasi Ikulu ya Marekani

Mtu aliyeifyatulia risasi ikulu ya White House nchini Marekani amefikishwa mahakamani akikabiliwa na tuhuma la kujaribu kumuua Rais wa nchi hiyo Barack Obama.

Ortega-Hernandez amesema yeye ni 'Yesu' wa zama hizi na kwamba alijaribu kumuua Obama kutokana na kiongozi huyo kutoheshimu mafundisho ya Yesu (Nabii Isa A.S).

Ikulu ya White House imeficha kikamilifu mazingira yanayohusiana na tukio hilo la Novemba 11 ingawa taarifa fupi ya ikulu imesema Rais Obama na mke wake Michelle Obama hawakuwepo Ikulu wakati wa tukio hilo. Chuki dhidi ya Rais Obama zimeongezeka katika miaka ya hivi karibuni kutokana na kiongozi huyo kukengeuka na kukataa kutekeleza ahadi alizotoa wakati wa kampeni zake za uchaguzi za mwaka 2008 alipodai kuwa atairejeshea Marekani heshima na hadhi yake iliyopotea.
 
Back
Top Bottom