Anayejiita "mbunge" Iramba Magharibi ahamia CHADEMA!

manutddevil

Member
Apr 22, 2012
5
0
Habari kutoka chanzo cha kuaminika zinasema kuwa, mzee mmmoja anayejulikana kwa jina la Nzuankende Kitundu almaarufu kwa jina la MBUNGE wa Kijiji cha misigiri wilayani Iramba mkoani Singida amehama chama chake cha CCM na kuhamia CHADEMA.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Mbunge huyo zinasema kuwa amehamia CHADEMA kutokana na tohuma mbalimbali za ufisadi zinazoelekezwa CCM ambazo yeye aliziita ni za kweli.

Aidha Mbunge huyo aliendelea kusema kuwa wakati umefika sasa wa Ukombozi wa Taifa la Tanzania na hivyo kutoa wito kwa watanzania wote wenye mapenzi ya dhati na Taifa hili kuhamia CHADEMA kwani wameonesha wana nia ya Dhati ya ukombozi wa Watanzania.
 
Hizi post zenu nyingi na vichwa vya habari haziendani kabisa, uwe unakula mchana kabla hujaposti kitu chochote ili akili zako zikae sawa na ujue unachokiandika sio unakimbilia kupost kama Pasco
 
Na yule chizi anayejulikana kwa jina maarufu kama Raisi wa Tanzania sijui lini atahamia Chadema
 
Habari kutoka chanzo cha kuaminika zinasema kuwa, mzee mmmoja anayejulikana kwa jina la Nzuankende Kitundu almaarufu kwa jina la MBUNGE wa Kijiji cha misigiri wilayani Iramba mkoani Singida amehama chama chake cha CCM na kuhamia CHADEMA.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Mbunge huyo zinasema kuwa amehamia CHADEMA kutokana na tohuma mbalimbali za ufisadi zinazoelekezwa CCM ambazo yeye aliziita ni za kweli.

Aidha Mbunge huyo aliendelea kusema kuwa wakati umefika sasa wa Ukombozi wa Taifa la Tanzania na hivyo kutoa wito kwa watanzania wote wenye mapenzi ya dhati na Taifa hili kuhamia CHADEMA kwani wameonesha wana nia ya Dhati ya ukombozi wa Watanzania.
Mkuu ahsante kwa taarifa hii kwani inazidi kunipa uhakika kuwa sasa Wanyiramba na Wanyisanzu wanataka ukombozi wa kweli. Pia mpe hizi salam fataki Mwigulu na Salome.
 
I see! Wewe umesoma chuo cha uandishi wa habari cha shigongo nini? Mbona watu mnatulazimisha tusome habari zenu hata kama hazina mvuto? Yaani nimeingia mbio nikijua Mwigulu ndiyo kahamia CHADEMA!
 
Hongera Mbunge moto ulio washwa wa ukombozi hauzimwi kwa kupulizwa
 
Frankly naomba ku-declare kuwa, SIZIPENDI THREAD ZA NAMNA HII! hivi karibuni kuna mwingine alianzisha NAPE ahamia chadema... kwanini usiwe direct katika unachotaka kukisema badala ya ku-play na mind za watu?

I wish mods wasiruhusu thread za namna hii

hebu pata picha mtu kasoma heading halafu salio likakata kabla ya kusoma habari yenyewe! si unataka aka-preach nini mtaani?

please be matured
 
Mkuu ahsante kwa taarifa hii kwani inazidi kunipa uhakika kuwa sasa Wanyiramba na Wanyisanzu wanataka ukombozi wa kweli. Pia mpe hizi salam fataki Mwigulu na Salome.

Hii kabila kumbe linajulikana mie nilifikiri halijulikani kabisa, maana ukimwambia mtu mie Mnyisanzu anabaki kushangaa.

Frankly naomba ku-declare kuwa, SIZIPENDI THREAD ZA NAMNA HII! hivi karibuni kuna mwingine alianzisha NAPE ahamia chadema... kwanini usiwe direct katika unachotaka kukisema badala ya ku-play na mind za watu?

I wish mods wasiruhusu thread za namna hii

hebu pata picha mtu kasoma heading halafu salio likakata kabla ya kusoma habari yenyewe! si unataka aka-preach nini mtaani?

please be matured

teh teh teh ..... usipende kukimbilia thread ... fungua thread ukitegemea lolote lile ...
 
Frankly naomba ku-declare kuwa, SIZIPENDI THREAD ZA NAMNA HII! hivi karibuni kuna mwingine alianzisha NAPE ahamia chadema... kwanini usiwe direct katika unachotaka kukisema badala ya ku-play na mind za watu?

I wish mods wasiruhusu thread za namna hii

hebu pata picha mtu kasoma heading halafu salio likakata kabla ya kusoma habari yenyewe! si unataka aka-preach nini mtaani?

please be matured

Du! Inasikitisha kufanya jukwaa hili linaloheshimika kuwa kichaka cha heading za UDAKU! Mleta mada anatakiwa ajue kuwa huku ni sehemu ya facts tu si sehemu ya kuleta upuuzi bwn. Alivyotengeneza heading haijapendeza kabisa.
 
Back
Top Bottom