Anayefahamu hii namba ya simu +4915145132077anijuze

Suip

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
1,314
759
Namba hiyo imenitumia ujumbe(text message) hii:- Your Mobile no.has won you £750,000 pound in Nokia UK PROMO. For claims send your name,address,mobile no. and occupation to Email:- nokiaconnect106@live.co.uk.

Kwa kifupi ni Namba yangu ya simu imeshinda paundi 750,000.katika promosheni ya Nokia ya Uingereza na wanataka niwatumie namba yangu ya simu, anawani yangu na kazi ninayofanya kwenye email hapo juu.

Sasa naomba humu JF kama kuna aliyewahi kupata huu ujumbe kwani katika eneo langu kuna mtu mwingine aliyetumiwa ila tofauti ni iPhone UK PROMO na email ni appleconnect.

Na hiyo code namba ni ya nchi gani? Ninamashaka yawezekana ni matapeli kwani hakuna droo niliyocheza.
 
thats old age online fraud by way of e-mail, they are now using phones instead...delete that message.
 
Kwa kifupi, dunia haiko fair kiasi hicho, hao ni matapeli tu watakuibia hata kile kidogo ulichonacho. Achana nao. Pole.
 
Wezi hao acha kuhangaika nao mkuu, the same sms was sent to me yesterday. I just deleted and forget. How can you won without playing Mkuu.
 
Hapo ukijichanganya umekwisha! Sasa fanya hivi,tuma details za uongo watakwambia lipia kiasi flan ili upate zawad yako.Majib utakayopata tujuze.Lkn hao ni wezi wa mtandaoni.
 
Ya engaland inaanzia +44 hao watakuwa matapeli hata mimi mwezi wa 7 mwaka huu walinitumia katika namba yangu ya hapa oman wakaniambia nimeshinda paundi 450 sikutilia maanani wala sijafatilia,maana sikuwa nimecheza draw yeyote,halafu waliniambia hvyo hivyo ni droo ya nokia,na mimi nlikuwa natumia Samsung,matapeli tu
 
Hao ni matapeli na usijaribu kuwapa taarifa zozote zinazokuhusu.
Nimewahi kupokea e mails kadhaa zenye ujumbe huo.
Tangu lini nokia wakawa na email ya live.co.uk?
Ila jaribu kisha utatwambia hapahapa yatakayokufika.
 
If it were a prize I would give you a piece of an advice to contact them.You can't win if you don't engage to a competation any more.
 
unashindaje bila ya kushindana? halafu promosheni ya nokia uk, taarifa unapata kwenye code ya ujerumani.
 
Namba hiyo imenitumia ujumbe(text message) hii:- Your Mobile no.has won you £750,000 pound in Nokia UK PROMO. For claims send your name,address,mobile no. and occupation to Email:- nokiaconnect106@live.co.uk.

Kwa kifupi ni Namba yangu ya simu imeshinda paundi 750,000.katika promosheni ya Nokia ya Uingereza na wanataka niwatumie namba yangu ya simu, anawani yangu na kazi ninayofanya kwenye email hapo juu.

Sasa naomba humu JF kama kuna aliyewahi kupata huu ujumbe kwani katika eneo langu kuna mtu mwingine aliyetumiwa ila tofauti ni iPhone UK PROMO na email ni appleconnect.

Na hiyo code namba ni ya nchi gani? Ninamashaka yawezekana ni matapeli kwani hakuna droo niliyocheza.

Achana kabisa na upuuzi huo. Mi mwenyewe nishawahi kupokea ujumbe huo. Ni matapeli hao, kwanza tizama figa yenyewe ya kiasi cha paundi hizo. Achana nayo.
 
Kaa chonjo kijana, utaibiwa bureeeeeeeeeeeeeeee!Mjini ni kwa wajanja, washamba kwao ni kijijini.
 
Kimbia sana usigeuke nyuma ndugu yangu. Mama mmoja hapa mwanza ameibiwa milioni kadhaa watu hao. Alipewa Namba ya akaunti Feki ya Natwest Bank akatamani utajiri zaidi. Kila akiingia online anaziona pound zinamngojea. Wakamwambia atume kiasi fulani ili account iwe activated. Kwa kuwa Kiasi kilichotakiwa ilikuwa kubwa na hakuwa nacho aliamua Muuzaji hostel yake hapo malimbe.

Hivi tunavyochat hapa yenye ni semi lunatic
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom