Anatamani ajiue, nimshaurije?

KMWONEWA

New Member
Mar 12, 2012
2
0
Mtu mzima, tena mwenye heshima zake,
Alikuwa na rafiki yake wa karibu. Na aliisaidia sana familia hii kutatua matatizo mazito waliyokuwa nayo. Siku moja wakamchukua huyu mtu mpaka kwao. Mke wa mwenye nyumba akamuomba namba huyu jamaa. Siku ya siku mwenye mke kasafiri, huku nyuma siku moja mkewe akakutana na huyu family friend. Usiku wake mke akampigia jamaa saa tano za usiku. wakapiga stori. Alfajiri akampigia kumwamsha. Jioni akampigia tena, alfajiri tena, ........ utani ukaingia. Jamaa akatahadharisha risk ya utani, mama akasema wala haina shida. kesho yake mama huyu akamkopa jamaa hela. siku zikaenda. Jamaa akajikuta amenaswa na mtego wa mke wa mtu. Akaitwa kama mara tatu na huyu mama jamaa roho ikawa inasita akakataa. Kila akiitwa jamaa anakwepa.

Siku moja jamaa akapokea sms kutoka kwa mume wa huyu jamaa kuonyesha kuwa jamaa kagundua mchezo. Jamaa hana hamu tena na anachanganyikiwa kupita maelezo. Dhamiri yake inamtesa kwa sababu hajawahi kukutana na huyu mwanamke japo walichat then akakwepa. Inaonekana kuna msg jamaa kazinotice, sasa kimenuka.
 
Kwa nature ya kazi yake na hali yake ni ngumu kuhama, labda aache kazi. na kupata nyingine itakuwa issue. Mimi ni mtu wake wa karibu nafikiria kumpeleka kwa jamaa wayamalize au kitanuka zaidi
 
Mtu mzima, tena mwenye heshima zake,
Alikuwa na rafiki yake wa karibu. Na aliisaidia sana familia hii kutatua matatizo mazito waliyokuwa nayo. Siku moja wakamchukua huyu mtu mpaka kwao. Mke wa mwenye nyumba akamuomba namba huyu jamaa. Siku ya siku mwenye mke kasafiri, huku nyuma siku moja mkewe akakutana na huyu family friend. Usiku wake mke akampigia jamaa saa tano za usiku. wakapiga stori. Alfajiri akampigia kumwamsha. Jioni akampigia tena, alfajiri tena, ........ utani ukaingia. Jamaa akatahadharisha risk ya utani, mama akasema wala haina shida. kesho yake mama huyu akamkopa jamaa hela. siku zikaenda. Jamaa akajikuta amenaswa na mtego wa mke wa mtu. Akaitwa kama mara tatu na huyu mama jamaa roho ikawa inasita akakataa. Kila akiitwa jamaa anakwepa.

Siku moja jamaa akapokea sms kutoka kwa mume wa huyu jamaa kuonyesha kuwa jamaa kagundua mchezo. Jamaa hana hamu tena na anachanganyikiwa kupita maelezo. Dhamiri yake inamtesa kwa sababu hajawahi kukutana na huyu mwanamke japo walichat then akakwepa. Inaonekana kuna msg jamaa kazinotice, sasa kimenuka.

Mbona sijaona sehemu ya yeye kujiua au kitu cha kumfanya ajiue.anyway mshauri ajiue kwa sababu ipo siku atakufa kama anafikiri utakuwa mwisho wa hayo matatizo
 
Wabongo kwa manjonjo. mbona sijaona wapi anataka kujiua. hapo inategemea nature ya huyo mume wa huyo mwanamke kama ni mwelewa. kama sio mwelewa aendelee tu kua mjinga na kumkwepa.
 
SI amwage tu ! Ukweli siku zote utabaki ukweli lakini hauwezi kuonekana mpaka uelezwe!
 
Hayo mambo ya kucheka na mashemeji zenu, hata kama akijiosha kama hajamega mzigo hakuna atakaesadiki, maana kuna ushahidi wa messages ambazo zinasema vinginevyo.
 
Kama anataka kujiua kweli its ok. But kama anategemea eti watamuwahisha hospitali mwambie madokta wenyewe hawatabiriki hawa.
 
Kujiua si suluhu ya tatizo, dawa ya tatizo ni kukabiliana naye. Naungana na huyo mchangiaji hapo juu kuwa aweke ukweli hadharani vinginevyo, atachukuiwa na huyo ndugu maisha yake yote.
Jamani pia tuwe waangalifu na utani uliopitiliza na wake za watu, matokeo yake ndiyo haya sasa. Fanya utani kwa kiasi, na zoeana kwa kiasi isipitilize, ni risk.
 
Hayo mambo ya kucheka na mashemeji zenu, hata kama akijiosha kama hajamega mzigo hakuna atakaesadiki, maana kuna ushahidi wa messages ambazo zinasema vinginevyo

Madamex Messages Haziwezi kuthibitisha kwa mtu fulani kafanya tendo la ndoa na mtu fulani, Labda kama mmoja kati ya watu hao sio muelewa kabisa

Huyu Bwana Hana sababu ya kuogopa , ni kwenda kukutana na huyo Rafiki yake na kuongea

Na ikiwa Hata eleweka ni kukutanishwa wote watatu ( mume, Mke, Na Mtuhumiwa na kuwekana sawa na sio kukimbia au kujihujumu uhai wake BURE
 
Back
Top Bottom