Anataka kuzaa naye tu mtoto hatamuhusu baba.

manuu

JF-Expert Member
Apr 23, 2009
4,064
10,723
Rafiki yangu mmoja jana tukiwa mahali alinipa kisa kinachohitaji mchango wa mawazo yako.
Kuna mrembo mmoja ambaye jamaa alijuana naye kupitia kaka yake(ie kaka wa huyu mrembo na huyu rafiki yangu walikuwa marafiki mpaka wakawa wanatembeleana nyumbani hapo ndo chanzo cha huyu mrembo kumjua huyu rafiki yangu.)Miaka kama 5 imepita bila yule jamaa kuonana na yule dada wa rafiki yake ambaye yeye alikuwa anamchukulia kama ni mdogo wake pia.
Juzi kati ghafla wakakutana Benk na yule mrembo wakaongea kidogo ikiwa ni pamoja na kubadilishana namba za simu.
Ikapita kama siku 4 mara simu ikaita kucheki ni yule mrembo wakaongea kikubwa yule mrembo akamuomba wakutane week end inayofuata.
Ikafika hiyo siku wakakutana wakaongea mengi sana na yule mrembo akatumia fursa hiyo kumweleza jamaa kwamba alikuwa hayupo nchini alienda Uingereza kuchukua Masters yake na ameshajenga nyumba yupo kwake ana gari 2.
Na ana pato zuri tu kwa mwezi.
Huyo Mrembo ndo ana miaka 29 sasa hivi.
Jamaa akafuraia mafanikio aliyofikia kwa kumpa hongera sana.
Yule binti akamwambia "Si nilichokuitia ila naomba usinifikirie vibaya kwani najua wewe ni rafiki mkubwa wa kaka yangu na ninajua una mke,Ninachoomba kwako ni nahitaji kuzaa na wewe kwani nimekuwa nikikupenda kwa mda mrefu sana ila niliogopa kukuambia mpaka ukaja kuoa ninachoomba kutoka kwako ni unipe mimba then mtoto atakaye zaliwa hasikuhusu kabisa kama una ogopa itakuletea shida kwa mkeo.
Na naomba sana usinifikirie vibaya kwani ni ukweli nakupenda sana na ukinikubalia nakuhaidi nitakupa zawadi nzuri sana"

Jamaa akamwambia nipe mda kidogo nifikirie then nitakupa jibu ndo jamaa kanitafuta jana kanipa kisa hiki.
Anaomba mchango wangu pamoja na wako juu ya hili.
 
Mmh! ngoja wakubwa wa mwagike verses za hekima na busara juu ya hili,
mm nipo nasikiliza.
 
mitego mingine bana... jamaa afanye donation ya mbegu tu binti akajimiminie, shida si ni kupata mtoto tu?
 
Kisa kizuri sana mkuu,lakini ukweli utabakia palepale kuwa babu zetu hawakukosea walipohakikisha kuwa mwanamke hapewi nafasi,sasa kama huyu with masters level ina maana hajaona kina paka mweusi tulivyojaa mpaka akajibane kwa mume wa mtu..??Au ina maana hiyo elimu yake aliyoelimika nyumba na magari yake basi anaona kuwa walio katika level yake ni wachache..?Ushauri tu kwa rafiki yako,mwambie ili kuokoa familia yake avunje kabisa mawasiliano na huyo ibilisi kwani itaanzia kwenye kuambukizana mimba na kitakachofuata baadaye nani anajua..?
 
mitego mingine bana... jamaa afanye donation ya mbegu tu binti akajimiminie, shida si ni kupata mtoto tu?

Ni uhuni tu the real sensible man hawezi kuacha damu yake bila kujua maendeleo ya mtoto hata kama mama atakuwa ni bi.................Kiroboto .wanawake sasa wanataka kutuzalau...
 
Rafiki yangu mmoja jana tukiwa mahali alinipa kisa kinachohitaji mchango wa mawazo yako.
Kuna mrembo mmoja ambaye jamaa alijuana naye kupitia kaka yake(ie kaka wa huyu mrembo na huyu rafiki yangu walikuwa marafiki mpaka wakawa wanatembeleana nyumbani hapo ndo chanzo cha huyu mrembo kumjua huyu rafiki yangu.)Miaka kama 5 imepita bila yule jamaa kuonana na yule dada wa rafiki yake ambaye yeye alikuwa anamchukulia kama ni mdogo wake pia.
Juzi kati ghafla wakakutana Benk na yule mrembo wakaongea kidogo ikiwa ni pamoja na kubadilishana namba za simu.
Ikapita kama siku 4 mara simu ikaita kucheki ni yule mrembo wakaongea kikubwa yule mrembo akamuomba wakutane week end inayofuata.
Ikafika hiyo siku wakakutana wakaongea mengi sana na yule mrembo akatumia fursa hiyo kumweleza jamaa kwamba alikuwa hayupo nchini alienda Uingereza kuchukua Masters yake na ameshajenga nyumba yupo kwake ana gari 2.
Na ana pato zuri tu kwa mwezi.
Huyo Mrembo ndo ana miaka 29 sasa hivi.
Jamaa akafuraia mafanikio aliyofikia kwa kumpa hongera sana.
Yule binti akamwambia "Si nilichokuitia ila naomba usinifikirie vibaya kwani najua wewe ni rafiki mkubwa wa kaka yangu na ninajua una mke,Ninachoomba kwako ni nahitaji kuzaa na wewe kwani nimekuwa nikikupenda kwa mda mrefu sana ila niliogopa kukuambia mpaka ukaja kuoa ninachoomba kutoka kwako ni unipe mimba then mtoto atakaye zaliwa hasikuhusu kabisa kama una ogopa itakuletea shida kwa mkeo.
Na naomba sana usinifikirie vibaya kwani ni ukweli nakupenda sana na ukinikubalia nakuhaidi nitakupa zawadi nzuri sana"

Jamaa akamwambia nipe mda kidogo nifikirie then nitakupa jibu ndo jamaa kanitafuta jana kanipa kisa hiki.
Anaomba mchango wangu pamoja na wako juu ya hili.

Kwa ajili huyo mdada ana uwezo wa kutosha, awe mvumilivu na kuvuta muda, atampata mwanaume atakayempenda na kuweza kuzaa nae.
 
..... Yule binti akamwambia "Si nilichokuitia ila naomba usinifikirie vibaya kwani najua wewe ni rafiki mkubwa wa kaka yangu na ninajua una mke,Ninachoomba kwako ni nahitaji kuzaa na wewe kwani nimekuwa nikikupenda kwa mda mrefu sana ila niliogopa kukuambia mpaka ukaja kuoa ninachoomba kutoka kwako ni unipe mimba then mtoto atakaye zaliwa hasikuhusu kabisa kama una ogopa itakuletea shida kwa mkeo.

Sasa hapa ushauri wa nini tena wakati tayari ana mke?? Kuzaa nje ya ndoa si ndo kumsaliti mkewe? By the way hivi huyo jamaa yeye amegeuka maksai kwa kuombwa kumzalisha mwanamke kirahisi hivyo (maksai-ng'ombe dume anayetumika kuzalishe ng'ombe jike)? Hajioni kama ameshushwa thamani? Haoni kama akikubalia kufanya hivyo pia atakuwa ameshusha utu wake?

Yeye akisikia mkewe kaombwa kufanya hivyo na mwanaume mwingine atajisikiaje? .... Mweeee, labda ufahamu wangu ni mdogo, ngoja niwasikilize wadau wengine nitarudi kumalizia uzi ....!
 
Huyu anatafuta kuwa nyumba ndogo kwa nguvu. Keshasema anampenda alafu ategemee wakishatiana mimba ndio nyege zitaisha??? Si ndio itakuwa tena na tena... mtoto wa pili na wa tatu???

Pili unadhani ni rahisi huyo kijana kuto connect na mtoto atakayezaliwa. Hapo piga ua mkewe atajua tu kwani huwezi ficha damu yako unless uwe hamnazo.

Tatu ataamini vipi kuwa huyo mwanamke hana nia ya kuvuruga ndoa ya yake... kwa maana kuwa ata behave kama other woman au atakuwa anamsumbua the real wife? Mapenzi hayajaribiwi jameni...

Huyo mwanamke ni mwizi tu... kama domo lilikuwa zito kutamka kuwa anampenda jamaa wakati alimjua since akiwa single...leo huo wepesi wa kutamka maneno mazito hayo ameutoa wapi...? Kaona amedoda anahaha... ukute keshaweka mitego kwa wanaume kadhaa... maradhi hayo...

ampe mimba tu sioni tatizo....... ila kwa anavyokupenda anaweza akakung'ang'ania na kukuachisha na mkeo
 
Sasa hapa ushauri wa nini tena wakati tayari ana mke?? Kuzaa nje ya ndoa si ndo kumsaliti mkewe? By the way hivi huyo jamaa yeye amegeuka maksai kwa kuombwa kumzalisha mwanamke kirahisi hivyo (maksai-ng'ombe dume anayetumika kuzalishe ng'ombe jike)? Hajioni kama ameshushwa thamani? Haoni kama akikubalia kufanya hivyo pia atakuwa ameshusha utu wake?

Yeye akisikia mkewe kaombwa kufanya hivyo na mwanaume mwingine atajisikiaje? .... Mweeee, labda ufahamu wangu ni mdogo, ngoja niwasikilize wadau wengine nitarudi kumalizia uzi ....!

Mkuu nashukuru kwa kunena nilichotaka kusema
 
Kiukweli huyu jamaa ametegwa, sio utani dah!! Wewe mwamamume rijali kabisa unaombwa kudonate sperm na mrembo? Ushauri wangu, akimbie!! wala si kutembea ni kukimbia kabisaaa!! Matatizo makubwa yanamyemelea huyu jamaa!! huyu mrembo atasababisha ama apate HIV au ndoa kuvunjika na mateso ya watoto baada ya hapo. Hii ni tamaa tu ya mabint wa kizazi cha leo. miaka 29 bado mdogo kabisa huyu binti kwa hiyo asijitie desperate kihivyo!!
 
Duuh..mwaka huu mpaka wanawake mutumalize..sahivi mntaka kununua mbegu zetu??...duuuh kama mie sitoi mbegu kisa ana masters nyumba na gari 2 na mtoto atamlea...

Then u said she 29yrs old?...hapo ndo utata huja..mama anaona anagonga menopause muda si mrefu n she gotta cheddah anahovia kuolewa...hana lolote anataka kuvunja ndoa ya mshkaji....

Ampe dudu no mimba..finitooo.
 
Mkuu angalia usiingie choo cha kike kwakua una mke achana na huyo dada wa rafiki yako atavuruga ndoa yako!
 
huyo demu ana 29 anaona age inakwenda mwanaume wa kuoa hakuna so ameona bora azae maana hutaki mtu utunze watoto uzeeni..wakae chini waelewane
 
Back
Top Bottom