Anataka kutoa mimba kisa Anaogopa Compulsory HIV testing

Janja PORI

JF-Expert Member
Jul 31, 2011
825
246
wadau Tunapoelekea Yani lazima Kila mtu ajue afya yake labda Usipende kupata mtoto Maana Huu mtindo Mtu akipata Mimba lazima apimwe mh Hapa na Czn wangu anataka kutoa mimba kisa anaogopa du wadau afanyaje

Ni lazima apime..hiyo itamsaidia kulinda afya ya mtoto asiambukizwe akiwa tumboni au akiwa anajifungua. Kama atakutwa nao kuna dawa watampa ya kumsaidia mtoto asiambukizwe tumboni. Mimi ninafahamu ni sheria na kuna sehemu ya kadi ya klinic inatakiwa ijazwe matokeo ya HIV. jamani tutumie akili zetu. Kwa nini muue kiumbe ambacho hakina hatia? Haya matangazo ya 'imagine the posibility of free HIV generation, it began with u' hamyasikilizi? Kupima ngoma ni jambo zuri sio kungoja mpaka apate mimba. Lets fight against ABORTION. :(

Mjamzito lzm apimwe. my wife is 7 month preg. alipoanza clinic akaambiwa ni lazima apime ili ijulikane km anao apewe dawa za kumkinga mtoto na maabukizi. hii ni ya preg ya pili so tunauzoefu wa kutosha tu. So tukapima tukapa majibu tunayafurahia maisha huku tuki expect a healthier baby!!

Kutoa mimba ni kuuwa na umevunja amri ya Mungu so dada zetu pls kama hampo tayar kulea achana na ngono au tumia kinga ili uepukane na balaa la kujakutoa mimba na nihatari kwa maisha yako na hata kwa baadae ukijataka mtoto unaeza usipate kutokana na kutoa mimba awali

ni lazima tena wote 2, msipopima no huduma hasa maeneo ya mkoa wa iringa
kweli kabisa ni lazima wapime. Tatizo watu hawajui umuhimu wa kupima! :(

Kupima siku hizi ni lazima,mshauri aende tu kupima ili ajue HIV status yake.

Kupima ni lazima ila kuchukua majibu ni hiari. Mfano kama ukikataa kupima watakupima bila ridhaa yako kwani wakati wa clinic lazima utatolewa damu tu. Wao watajaza kadi yako ya clinic na kuonyesha status yako. Hii inasaidia hata wakunga watakao kuhudumia wakati unajifungua kujikinga usiwaambukize. Ukiwa makini unaweza soma kadi ukajua status ya mtu hawaandiki HIV wanatumia technical language(nimeisahau) lakini kama umeenda shule utajua.

Nimekumbuka rafiki yangu mumewe hajatulia fulani (yani wanaume wengi utulivu zero ila yeye hafichi anajulikana ni macho juu) sasa alipokuwa mja mzito mume wake eti anamwambia marufuku kupima HIV hawawezi kukulazimisha. Wanaume bwana. Lakini alipima bila kumshirikisha.

Ila haya mambo nakumbuka nilikwenda clinic siku moja nikaona mdada analia na mimba yake yani nikajisemea kaambiwa +ve nini. Tena hizi private hospital hakuna cha counselling wala nini.

Tatizo watu wengi hatucheki afya zetu na tunazaa bila mpangilio. Kama una good planning ya uzazi unapima kwanza kabla ya ku conceive.

Hii mada imenifanya niwahurumie manesi. Unajua wako kwenye risk ya kuambukizwa HIV kazini. Nilijenga urafiki na manesi walikuwa wananambia wamemuachia Mungu maana kuna kujidunga sindano wakati wa kushona wazazi. Acha tu.

ni lazima tena wote 2, msipopima no huduma hasa maeneo ya mkoa wa iringa

SIKUHIZI WALA HITAJUA KAMA UMEPIMWA UKIMWI YAANI NI KAMA MALRIA VILEE,AF KUPIMA RAHA SANA HATA KAMA UNAKWEPA HUKO MBELE UNAPOANZA KUUMWA MAGONJWA YASIYOISHA INABIDI UPIME,NI HERI KUPIMA UJUE MOJA INAOGOPESHA LAKINI INASAIDIA SANA

Ni lazima apime..hiyo itamsaidia kulinda afya ya mtoto asiambukizwe akiwa tumboni au akiwa anajifungua. Kama atakutwa nao kuna dawa watampa ya kumsaidia mtoto asiambukizwe tumboni. Mimi ninafahamu ni sheria na kuna sehemu ya kadi ya klinic inatakiwa ijazwe matokeo ya HIV.
unaweza kueleza ni sheria ipi inayoelekeza mama mjamzito apime HIV?ninavyofahamu kupima HIV ni hiari na hufanywa baada ya mhusika kupewa ushauri nasaha na kama akikubali kupimwa anapewa ushauri unaoendana na matokeo yake.kwa kifupi kinamama wanashauriwa na sio kulazimishwa kupima HIV.

Ni hiari lakini in most cases muhusika anakuwa hana choice na jinsi wakunga/madaktari wanavyointroduce issue ya kupima kwa mja mzito ina sound as if ni lazima. That is why asilimia kubwa ya wanao attend clinic wanapimwa HIV. Na kwa hospital za private hakuna cha counselling wala nini labda kwa wanaokutwa positive lakini to my experience unaambiwa tu inabidi upime HIV.
Sasa kama counselling itafuata majibu yakiwa mabaya I don't know lakini kabla ya kupima wanakwambia kavu kavu hakuna cha ushauri.
unaweza kueleza ni sheria ipi inayoelekeza mama mjamzito apime HIV?ninavyofahamu kupima HIV ni hiari na hufanywa baada ya mhusika kupewa ushauri nasaha na kama akikubali kupimwa anapewa ushauri unaoendana na matokeo yake.kwa kifupi kinamama wanashauriwa na sio kulazimishwa kupima HIV.

Kupima ni lazima ila kuchukua majibu ni hiari. Mfano kama ukikataa kupima watakupima bila ridhaa yako kwani wakati wa clinic lazima utatolewa damu tu. Wao watajaza kadi yako ya clinic na kuonyesha status yako. Hii inasaidia hata wakunga watakao kuhudumia wakati unajifungua kujikinga usiwaambukize. Ukiwa makini unaweza soma kadi ukajua status ya mtu hawaandiki HIV wanatumia technical language(nimeisahau) lakini kama umeenda shule utajua.
Nimekumbuka rafiki yangu mumewe hajatulia fulani (yani wanaume wengi utulivu zero ila yeye hafichi anajulikana ni macho juu) sasa alipokuwa mja mzito mume wake eti anamwambia marufuku kupima HIV hawawezi kukulazimisha. Wanaume bwana. Lakini alipima bila kumshirikisha.
Ila haya mambo nakumbuka nilikwenda clinic siku moja nikaona mdada analia na mimba yake yani nikajisemea kaambiwa +ve nini. Tena hizi private hospital hakuna cha counselling wala nini.
Tatizo watu wengi hatucheki afya zetu na tunazaa bila mpangilio. Kama una good planning ya uzazi unapima kwanza kabla ya ku conceive.
kupima sio lazima na kama umelazimishwa ni kinyume na maadili ya udaktari.hizo technical terminologies zinaelezea makundi yote aliyepima na kuwa +,aliyepima na kuwa negative,aliyepima lakini majibu hajulikani na asiyepima kabisa.kuhusu kuepusha maambukizi kwa wahudumu wa afya;hii haina logic kwa sababu sio ukimwi pekee unambukiza.isitoshe muhudumu wa afya amefundishwa kuzuia maambukizi kwake au kwa mgongwa(infection prevention techniques)
nasisitiza kabla mgonjwa hajafanyiwa chochote(pamoja na kupima) lazima atoe informed conset.tusihalalishe makosa yanayofanywa na baadhi ya wahudumu wa afya kuwa ni sheria.

Sasa hapo ni kazi. Je utatofautisha vipi hiari na lazima; kwani unatakiwa usaini kabla ya kupimwa. Hata ukisema ushitaki una evidence gani kuwa ulilazimishwa au ilikuwa hiari wakati hakuna sehemu unayotakiwa kusaini kuonyesha umekubali au la? Nachojua operesheni ndio watu wanasaini makaratasi kuonyesha wamekubali. Lakini hata ukipimwa ki lazima huwezi shitaki kwa kuwa huna ushaidi kuwa umelazimishwa.

kutoa mimba ni laana kubwa sana..tatizo watu tunaogopa matokeo yaan tunafikiria baada ya kutenda..akapime tuuu ili alinde kiumbe kilichopo tumboni na ajifunze pia kuplay safe kama anaogopa ukimwi kiasi hicho cha kutaka kutoa mimba..kupima siku hizi kwa mama mjamzito ni lazima.

Sasa hapo ni kazi. Je utatofautisha vipi hiari na lazima; kwani unatakiwa usaini kabla ya kupimwa. Hata ukisema ushitaki una evidence gani kuwa ulilazimishwa au ilikuwa hiari wakati hakuna sehemu unayotakiwa kusaini kuonyesha umekubali au la? Nachojua operesheni ndio watu wanasaini makaratasi kuonyesha wamekubali. Lakini hata ukipimwa ki lazima huwezi shitaki kwa kuwa huna ushaidi kuwa umelazimishwa.
ki maadili huwezi kutolewa damu ya vipimo bila ridhaa yako.kumbuka unapompima mama kwa lazima hutaweza kumlazimisha anywe dawa au afuate masharti ya kuishi na virusi hivyo unachohitaji ni kumnasihi ili akubali na kuelewa.ulazima hautakiwi kuwepo kwa sababu hausaidii.

unaweza kueleza ni sheria ipi inayoelekeza mama mjamzito apime HIV?ninavyofahamu kupima HIV ni hiari na hufanywa baada ya mhusika kupewa ushauri nasaha na kama akikubali kupimwa anapewa ushauri unaoendana na matokeo yake.kwa kifupi kinamama wanashauriwa na sio kulazimishwa kupima HIV.

Mama yeyote mjamzito anapohudhuria clinic katika kadi ya clinic kuna aina mbalimbali za vipimo unavyotakiwa kufanyiwa kama vile BP, Kisukari, UTI, VDL, HIV.

Sasa katika hivyo vipimo hakuna suala la hiari kwa sababu limelenga katika uzazi salama. Mfano, ni lazima ijulikane kama umeambukizwa magonjwa yoyote ya zinaa STDs (Kaswende, gonorrhea, warps, n.k) ili kama uko +ve kwa hayo magonjwa utibiwe ili usije mwambukiza mtoto au usije jifungua mtoto mwenye ulemavu wa macho n.k. Kwa HIV ni lazima kwa sababu kwanza inaweka kumbukumbu ili wakati wa kujifungua ijulikanae kama wewe ni +ve utaratibu maalumu utaandaliwa kwa ajili yako. Lakini vilevile, kwa kuwa uzazi wa sasa hivi unakuwa na matatizo na wakati mwingine kujifungua kwa operation, tahadhari kwa madaktari lazima ichukuliwe katika hali yoyote ile kulingana na hali ya kiafya ya mjamzito.

Kwa hiyo hakuna suala la hiari kwa mjamzito. Kama hutaki kupima basi usibebe mimba. Ninasema hivyo kwa uzoefu kwa kuwa nimekuwa nikihudhuria nikimsindikiza "mywife" wangu, so i know everything. Na kimsingi kuna faida zaidi kwa mjamzito kujua hali yake ya HIV kuliko kutokujua. Hii pia ni kwa upande wa madaktari, wakunga na wauguzi wanaowahudumia hao akima mama wajawazito.

Hakuna sheria iliyotungwa na bunge ya kulazimisha hili suala, ila ni mwongozo wa wizara ya afya wa namna ya kuwahudumia wajawazito kuhakikisha uzazi salama kwa mama na mtoto anayezaliwa.

Back
Top Bottom