Anaswa na kichwa cha albino jijini Dar

I wish kungekua na mawazo kuwa ukipata kichwa cha fisadi wa ccm unakua tajiri nadhani ingesadia sana kuwamaliza kuliko hii ya kuwamaliza ndugu zetu wasiokuwa na kosa
 
Bongo bwana! Kila kitu siasa, Chachaaa! Halafu kwenye uringo wa siasa nawasikia sana hawa Chacha.
 
MFANYABIASHARA wa baa na nyumba ya kulala wageni ya Bongo Star Lodge iliyopo Kawe Ukwamani, James Isame, maarufu kama Mzee Chacha (50), anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni kwa tuhuma ya kukutwa na kichwa cha binadamu anayedhaniwa kuwa ni mlemavu wa ngozi (albino).

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela amethibitisha kushikiliwa kwa mfanyabiashara huyo na kusema kuwa alikamatwa juzi saa 2:45 usiku baada ya wasamaria wema kutoa taarifa kwa jeshi hilo juu ya kuwepo kwa tukio lisilo la kawaida katika nyumba hiyo ya kulala wageni.

Alieleza kuwa, baada ya taarifa hizo, polisi waliizingira nyumba hiyo kisha wakamtafuta mjumbe wa eneo la Kawe kwa ajili ya kuthibitisha upekuzi utakaofanyika na kwamba baada ya taratibu zote, walimtaarifu muhusika ambaye alianza kuonesha upinzani juu ya kufanyiwa upekuzi.

Alisema jitihada za mtuhumiwa kuzuia upekuzi huo zilishindikana, ndipo katika kufanya kazi hiyo maeneo yote ya ndani na nje ya nyumba hiyo pamoja na baa, walifanikiwa kukuta kichwa cha binadamu kikiwa kimewekwa juu ya ukuta wa choo.

"Kilikuwa kimevingirishwa katika mfuko wa rambo na tuliweza kubaini kuwa ni kichwa cha binadamu baada ya kuona nywele na meno, ila bado hatujajua ni wa jinsia gani au kama ni mlemavu wa ngozi," alisema Kenyela.

Akielezea tukio zima, Kamanda Kenyela alisema baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa za kuwepo kitu kisichoeleweka katika eneo la mfanyabiashara huyo, waliweka ulinzi maeneo yote.

Aliongeza kuwa, kichwa hicho kilikuwa na mchanga hali inayoonesha kuwa huenda kilikuwa kimefukiwa kabla ya kufikishwa hapo au wakati wa kukatwa kilikuwa kimewekwa katika mchanga.

Kamanda Kenyela alisema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na baada ya upelelezi kukamilika, watapeleka maoni ya Jeshi la Polisi kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kwa ajili ya hatua zaidi.

Baada ya taarifa hizo kuenea, Tanzania Daima ilifika hadi katika nyumba ya kulala wageni ya Bongo Star Lodge iliyoko Kawe na kuangalia mazingira ya eneo zima na kisha kuzungumza na baadhi ya wafanyakazi na majirani.

Eneo la nyumba hiyo limezungukwa na nyumba nyingine za makazi ya watu, huku eneo la kuuzia vinywaji likiwa limepakana na vyoo vitatu ambavyo ukuta wake ndiyo unaosadikiwa kuwekwa kichwa hicho.

Kuanzia mlango wa kuingilia katika baa hiyo hadi vyumbani, kumesakafiwa na kuwekwa vigae ambavyo si rahisi kwa mtu kuchimba pasipo kujulikana, huku vyooni kukiwa na hali hiyo pia.

Mmoja wa wafanyakazi wa nyumba hiyo aliyeomba jina lake lihifadhiwe alisema kuwa, walishuhudia askari wakifika katika eneo hilo na kwenda moja kwa moja katika upande wa choo, na baada ya muda wakaondoka na mmliliki wa nyumba hiyo.

"Hatukujua ni kitu gani kinaendelea mpaka meneja alipotuambia kuwa mzee ameshikwa na kichwa cha binadamu," alisema mmoja wa wafanyakazi hao.

Majirani waeneo hilo walipoulizwa kama wanafahamu juu ya jirani yao kukamatwa kwa tuhuma za kukutwa na kichwa cha binadamu, walishangaa na kusema ndiyo kwanza wanapata habari hizo kutoka kwa mwandishi.

Kwa upande wake, mjumbe wa nyumba kumi wa eneo hilo aliyefahamika kwa jina moja la Mzee Kilambo, alisema aliitwa na polisi kwa ajili ya kushuhudia upekuzi katika eneo hilo, na kwamba maelezo zaidi ya nini kimetokea yanapaswa kuulizwa polisi.


SOURCE: TANZANIA DAIMA



 
Watu hawamuogopi Mungu! ama kweli Fedha nooooma. huu jama angeweza kumuuza Yesu kwa vipande vya fedha
 
Biashara hii hii ya kuuza pombe inawatia watu kichaa cha kukata vichwa vya watu wengine? What a lose end?
 
Dunia imefika Mwisho maana hata Bwana wetu Yesu alisema kuwa katika Siku za mwisho watu watakuwa wapenda fedha na kujipenda wenyewe
Mwenye macho ambiwi tazama na Mwenye masikio ambiwi sikia.
 
Msitoe hukumu kabla ya kusikia upande wa pili. Inawezekana akahusika na kichwa hicho na pia inawezekana asihusike. Ukisoma vizuri maelezo hapo juu, yana utata. Huenda walim-setup kwa nia mbaya au kwa visasi.
 
Kwa jinsi pollisi walivyofanya kazi hii, kuna dalili zote za kuwa huyu mfanyabiashara kabambikizwa hicho kitu. Haiwezekani mtu aweke kichwa cha binadamu kwenye rambo halafu kwenye ukuta wa choo, ambako kila mtu anaenda. Hapa lazima kawaudhi wakubwa wameamua kumpotezea kwa mtindo huu!
 
kwa maelezo na mazingila ya hapo inaonekana ni hujuma za kibiashara hizo upelelezi ufanyike vizuri itabainika aliyefanya hicho kitu tusitoe hukumu kwa huyo mura chacha wakati upelelezi aujakamilika
 
Watanzania watabadilika kama kiwango cha elimu kitapandishwa. Serikali lazima iwekeze kwenye elimu ya watu wake kuondoa imani potofu. Pia umaskini unachangia, watu wanauzana kuganga njaa. Masikini nch yangu Tanzania.
 
Mimi namjua anaitwa jemsi isame ni mfanya biashara,ila hiyo story niyakubumba tu na nilikuwepo cha kuchekesha waliingia wanatafuta bunduki na walipoingia wakaenda moja kwa moja choo cha nje wakachukua kimfuko ndo kulikua na hicho kichwa ila ni fuvu alafu chakushangaza fuvu linanywele na zile nywele nizakusukia wanawake zimewekwa kama vile gundi,ni mchezo waliufanya maana mpaka askali wengine walikua wanasema hili ni soo watawashutukia.ila anaugomvi na oc cid wa kawe muda
 
Hay ndio matokea ya kuwa na pengo kubwa kati ya matajiri na maskini. Kama utu wa mtu unatambuliwa kwa kiasi cha mali ulichokuwa nacho....kwanini mtu asitumie njia yeyote anayeijua ili aweze kupenya katika pengo hilo???? Tusimlaumu sana kwani ndiyo mfumo wetu uliotupeleka huko.......
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom