Anaswa na kichwa cha albino jijini Dar

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,006
2,667
Heshima zenu Wakuu,

Taarifa kwa kifupi kuwa bwana mmoja kwa jina la Chacha (sijabahatika kupata jina la pili) ambaye ni mmiliki wa nyumba ya kulala wageni iitwayo 'Bongo Star' iliyopo maeneo ya Kawe jijini Dar kakamatwa na alihojiwa hii leo Polisi - Kawe.

Jitihada za kupata habari hizi toka Polisi zilikaribia kukwama kwani ilionekana kama kuna kitu kilikuwa kinafichwa lakini baadae wakakiri kuwa wamemkamata na amefunguliwa mashtaka.

Updates zitafuata kadiri tunavofuatilia kinachojiri.
 
Ardhi ya tanzania ni kama imelaaniwa kwa kunywa damu isiyo na hatia kila siku, Mungu tunusuru na majanga haya
 
Chacha tena? Mambo ya vichwa vya Albino na Chacha wapi na wapi tena? Mura Chacha umechoka kuswaga ng'ombe umeamua kuswaga vichwa vya watu!
 
ndiyo mambo ya akina john komba na wenzake kichani patupu lakini maalbino wanawangamiza kukalia nafasi za ccm
 
Huyu Chacha ni katibu wa tawi wa ccm au ni nani kumbe?hii thread imekujaje kwenywe siasa?
 
Habari hii haijaandikwa vizuri kukidhi kichwa cha habari. Pamoja na mapungufu hayo ingefaa kupelekwa' Habari na Hoja Mchanganyiko'
 
Njaa ya utajiri bila kufanyakazi kwa bidii, tz wanaamini kila watakachoambiwa kuwa kitamfanya awe tajiri, hapo anamiliki guest house kaja tapeli kamwambia ukipata kichwa cha albino wateja watajaa na baada ya muda utakuwa na hotel kama Hyyat. Halafu tunategemea maendeleo siku za usoni Tanzania. Huyu anauwezo wa kumikili guest house Dar es Salaam, inawezekana hata ni msomi, kama huyu ameshindwa kuelewa kuwa utajiri hauji kwa njia za kawaida, yule mwananchi wa kawaida kule kijiji ataamini nini?

Mungu shusha malaika wako watakatifu kuliokoa taifa lako la Tanzania ambalo linaangamizwa na giza la shetani.
 
Huyu Chacha ni wa chama kipi cha siasa hapa Nchini?

Ama mstaafu wa chama cha mafisadi nini?
 
Chacha tena? Mambo ya vichwa vya Albino na Chacha wapi na wapi tena? Mura Chacha umechoka kuswaga ng'ombe umeamua kuswaga vichwa vya watu!

Mkuu Kimbunga hata mie nimeshangaa hawa jamaa zetu miaka ya nyuma tulikuwa tunawaamini sana kwa ulinzi majumbani...Chacha! Mang'ana kasarikile baba robi..
 
Last edited by a moderator:
hii ndio Tanzania bwana! asilimia kubwa bado wapo kwenye giza wanaamini vitu vya kijinga kweli.ukimuuliza atakwambia anatafuta utajiri. UKITAKA UTAJIRIKE TANGAZA KWAMBA UNAUZA DAWA YA UTAJIRI NA BAHATI WATAKUJA WATANZANI KIBAO KUNUNUA
 
Back
Top Bottom