Anapodai ushuhuda wa kupendwa........

Labda hajielewi so you need to show are that you care so much by going beyond yale anayojitakia

lemonade nafikiri issue siyo yale anayoniambia bali yale ambayo hawezi kunitamkia ambayo ni kwanini hajiamini kabisa na ndiyo maana hawezi kuniamini hata mie..............
 
Last edited by a moderator:
Ningechangia huu Uzi Ruta lakini niko busy hapa Bongo nafuatilia hukumu ya John Myika tutawasiliana baadae.

Ndallo tuko pamoja kabisa uktioka huko kumbuka kumwaga busara zako humu jamvini nasi tunufaike.........
 
Last edited by a moderator:
Ukipenda, uwepo uwiano baina ya "maneno" na "vitendo"
Ukipenda, ukawa unasema bila kutenda, hupendi.
Ukipenda, ukawa unatenda bila kusema, hutendi.

Nimewasikia wengi wanaolalamika kwa moja au jengine.
Nimewasikia wengi wanaolalamika kwa maneno matamu bila matendo.
Nimewasikia wengi wanaolalamika kwa matendo mema bila maneno ya upendo.

Kupenda bila matendo, kutenda bila maneno
Hufanya neno lisiwe pendo, wala tendo kuwa pendo.

Angalizo: Linapokuja suala la kulinganisha na kupeana ushahidi, neno linachukua nafasi kubwa.
Neno unalolitoa likiwa zuri na ukalitekeleza, tayari umetenda na umependa. Lakini wengi tuchukulia kuwa kupenda ni kusema tu, tena kwa lugha ya kidhungu - I LOVE YOU - kumbe watamkaji "midomo yao" ni michafu haisafishiki hata kwa jiki, limau na jivu. Na ndio maana mababu na mabibi zetu walilishana "nyama za ulimi" na ikawa sababu ya kuishi hadi kutengana kwa vifo, wakati leo "tunalishana denda", na "I love you" nyingiiiiii, lakini mate yakikauka tu na mapenzi yameyayuka.
 
Ukipenda, uwepo uwiano baina ya "maneno" na "vitendo"
Ukipenda, ukawa unasema bila kutenda, hupendi.
Ukipenda, ukawa unatenda bila kusema, hutendi.

Nimewasikia wengi wanaolalamika kwa moja au jengine.
Nimewasikia wengi wanaolalamika kwa maneno matamu bila matendo.
Nimewasikia wengi wanaolalamika kwa matendo mema bila maneno ya upendo.

Kupenda bila matendo, kutenda bila maneno
Hufanya neno lisiwe pendo, wala tendo kuwa pendo.

Umesikika MAMMAMIA lakini yote chanzo si kauli khalafu matendo kufuata.........................kama kauli zina mgongano yawaje basi?
 
Last edited by a moderator:
BADILI TABIA Na kwa vile linaonekana halina uzito na ndiyo maana hata siku hizi hatukumbushani ya kuwa tunapendana..................ukweli wabakia mjue mtu wako kwa undani na usiendekeze majungu khalafu mpime yawezekana anapokutamkia anakupenda mwenzio aongea kilichoko moyoni mwake.............................sasa wewe ukimpuuzilia mbali atafikiri pengine unamdharau na hauna utii kwake...........................naona inabidi turudi kwenye khoja ya utii bila ya kutiana.........lol

lol, hapa pana kaukweli hapa. Kuna wengine akishakupenda siku ya kwanza basi nakupenda hupotea kabisa.
Rutashubanyuma kaka,
matendo hukidhi haja maridhawa kuliko maneno,
Wapo walosema sana, wakabaki na yao maneno
Kwingineko wakabana, wakidhani twashiba neno.
Lol, japo maneno matamu, yakoleze kwa vitendo

kumbe nami malenga mpya, tehe
 
Last edited by a moderator:
Umesikika MAMMAMIA lakini yote chanzo si kauli khalafu matendo kufuata.........................kama kauli zina mgongano yawaje basi?
Ruta Mkuu, labda sikujieleza vizuri, lakini ninachotaka kusema na nasisitiza, ni lazima kuwepo na uwiano na msimamo katika kauli (na matendo). Ninaposema uwiano wa kauli, nakusudia kusiwe na kauli zinazogongana. Sio anasema anataka lakini matendo yake yanadhihirisha kuwa hataki na pengine hajiamini, au anasema hataki kumbe moyoni anaatilika. NWY, "Love process is not cut-to-fit all persons. Every pair is a world of their own. What suits one pair doesn't fit the other".
 
Mie sasa nami namtilia mashaka kwani maangalizo yake yanitisha!
Mie sasa nami namtilia mashaka kwani anishurutisha nifanye makubwa!
Mie sasa nami namtilia mashaka kwani kipimo atakacho kina walakini!
Mie sasa nami namtilia mashaka kwani adai nimtembelee kivilevile, duh!
Anapodai ushuhuda wa kupendwa huku akitoa na maangalizo yake!

Duh!
Fafanua visuri! mbado sijakuelewa bro. Weka mamba hadharani tukusaidie!.
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom