Anaomba msaada kuokoa ndoa yake

Dogo1

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
1,361
576
Rafiki yangu alienda nje kusoma akabahatika kupata rafiki wa kike ambae walishirikiana katika nyanja zote za mapenzi. Baada ya kumaliza masomo rafiki yangu akarudi TZ peke yake. TZ akapata rafiki mpya wa kike ambaye kila mmoja hakumficha mwenzake juu ya maisha aliyopitia.

Bahati huyu msichana kabla ya kukutana na rafiki yangu alikuwa bado hajawahi kufanya tendo la ndoa, so alianza na huyu rafiki yangu. Hatimaye rafiki yangu alitangaza uchumba kwa rafiki yake na wakakubaliana kufunga ndoa.

Baada ya kutoa mahari na wanasubiri kufunga ndoa, mchumba wa rafiki yangu akapata mwanaume ambaye alikua anashirikiana nae katika mapenzi including ngono, takriban kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita. Lengo la kufanya hivyo ni kulipa yale ambayo mchumba wake aliyafanya kabla hawajafahamiana wakati akiwa masomoni.

Rafiki yangu hakugundua kuwa mchumba wake anamahusiano na jamaa mwingine. Mda ukafika wakafunga ndoa. Mke wa rafiki yangu akaachana ya yule jamaa mwingine.

Hata hivyo rafiki yangu sometimes alikua anafanya ngono na wanawake ingawa ni kwa mtindo wa "hit n run". Ni hadithi ndefu. Lakini ktk hali ya ajabu rafiki yangu na mke wake kila mmoja aliconfess kwa mwenzake matendo aliyoyafanya kabla na baada ya ndoa.

Ni mwaka mmoja sasa maelewano yamekuwa yanalegalega, haipita wiki moja lazima watalumbana for hours kila mmoja akimlaumu na kumlaani mwenzake kwamba hakuwa mwaminifu.

Ushauri wenu unahitajika kuinusuru ndoa hii
 
hao nao mfala kweli! Eti mtu unaconfece kwa mke/mume wako eti nimecheat juzi.mhh! Uzungu ukizidi nayo balaa.we kama umeamua ku cheat,ponda raha kimya kimya,yakija sanaku ndio utajua ubaya wa ku cheat.
 
Watahadhalishe kuwa wafanyacho ni ujinga kwani wanahatarisha maisha yao na kuharibu uzuri na utamu wa ndoa yao ambao hawataweza kuurudisha bali itabaki majuto na kulaumiana. Wakae chini na kujadiliana upya nini lengo la kuoana kwao.

Hakuna atakayeweza kuwajengea maisha bora ya ndoa ila wao wenyewe. Waanze upya kwa kusahau na kusamehe yaliyopita.
 
hao nao mfala kweli! Eti mtu unaconfece kwa mke/mume wako eti nimecheat juzi.mhh! Uzungu ukizidi nayo balaa.we kama umeamua ku cheat,ponda raha kimya kimya,yakija sanaku ndio utajua ubaya wa ku cheat.

comment ya akili sana hii.
 
Wote ni wachafu, waende wakaombewe pepo la ngono liwatoke wamrudie Mungu watubu dhambi zao na kuziacha kabisa namaanisha waokoke na wamuombe Mungu awajaze Roho Mtakatifu ili awe msaidizi wao katika kuzishinda dhambi na majaribu yote. Na wasiache kwenda kuabudu kamwe. Vinginevyo hakuna suluhisho kwenye hiyo ndoa. Wasisahau kupima afya zao kama wameshapata maambukizi ya Ukimwi.
 
Zinaa ni dhambi, zinaa ni deni, zinaa inaongeza umasikini, zinaa inaleta madhara kwa jamii nzima, zinaa ni uchafu.
ACHENI ZINAA
 
Kwa hali hii, wapeana divorce paper!! Hakuna ndoa hapo. Hivi unapoamua kuao au kuolewa si unatakiwa kuacha makandokando yote? Hapa wote ni malaya tu hakuna wa kumsuta mwenzake, no uaminifu, no ndoa
 
eeeti mwanamke umemkuta bikra analipia uliyoyafanya wakati hukua naye! duu hv haya mambo yapo kweli!
MUNGU aepushe nisilipiziwe duu!
 
hao wamekutana wenye akili sawa.watajua jinsi ya kwenda sawa tu

Siyo rahisi kukifuta hicho kitu. Walitakiwa kuconfess kwa Mung Baba kivayao vyao na kusonga mbele na maisha. Inaonekana wanaendeshwa sana na hisia hao watu. Ukipingwa wimbo mzuri watacheza hata nguo zitaanguka, wakiletewa msimba watalia mpaka ardhi itapasuka. Ndio maana wanakumbusahana yaliyopita.
 
hao nao mfala kweli! Eti mtu unaconfece kwa mke/mume wako eti nimecheat juzi.mhh! Uzungu ukizidi nayo balaa.we kama umeamua ku cheat,ponda raha kimya kimya,yakija sanaku ndio utajua ubaya wa ku cheat.
He he he..leo nilikuwa sijacheka kabisa...te te te you made my day!.
 
Back
Top Bottom