Ananipenda ananitamani??

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,138
Fikiria wewe ni binti mwenye sifa zote za kuolewa (excellent marriage material) na umri wako ni sahihi kuolewa, umempata kijana wa kiume mwenye sifa zote za kuoana na wewe.
Anakujali kwa kila kitu na unaona mambo yanaenda vizuri, baada ya muda mrefu unaamua kumuuliza akupe majibu lini mnaweza kuoana, yeye anakuruka na kusema muda bado na unapoendelea kumuuliza akupe majibu sahihi anagoma na kukuacha huku hujui kama kweli yupo committed.

Unajiuliza na kujihoji kama kweli anakupenda na ana upendo wa kweli kwako na je upendo wake kwako una maana yoyote kama hataki kujitoa na kuamua kuoana?

Unajiuliza kwa ukaribu (intimate) uliopo je kuna tatizo gani kwake kushindwa kukubali lini tuoane na kuamua kuishi kama mke na mume?
Kila siku inayoenda unajikuta una maswali mengi kuliko majibu.

Swali kuu ni kwa nini huyu mwanaume anakugeuka tu pale unapotaja suala la kwenda madhabahuni kufunga ndoa ili kuthibitisha kwamba anakujali, anakupenda na kwamba wewe ndiyo chaguo lake duniani kama anavyotamka mkiwa pamoja.

Je, ungekuwa wewe ni huyu mwanamke ungefanyeje?

Ukweli ni kwamba kuna wanaume ambao ni ovyo, hujiingiza katika mahusiano bila lengo la kuoana bali “just for fun”

Pia ieleweke kwamba hakuna mwanamke anaweza kulazimisha mwanaume kumuoa kama mwanaume mwenyewe hayupo tayari au hataki.
Ukweli ni kwamba unavyozidi kumlazimisha ndivyo anatakavyokuwa mgumu zaidi kukubali.

Jambo la msingi ni kumuuliza huyo mwanaume mapema kabisa kabla uhusiano haujafika mbali akueleze wazi maana ya uhusiano mnaoanza ili asikupotezee muda wako wa thamani na kuchezea hisia zao na kukupa matumaini makubwa wakati hana mpango wowote bali kujifurahisha.

Pia wapo wanaume ambao kwao kuoa ni kupoteza uhuru, kuongezewa majukumu, wanaamini ukishaoa unapoteza uhuru na zaidi “kwa nini ununue ng’ombe kama unaweza kupata maziwa bure”

Haina haja kuwa katika mahusiano ambayo mmoja hakubaliani na aina ya mahusiano unahitaji
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom