Ananilea Nkya apata Mrithi TAMWA. Ni Mwandishi wa RTD zamani...

[h=2][/h]JUMAMOSI, SEPTEMBA 29, 2012 08:49 NA ELIZABETH MJATTA


ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Ananilea Nkya, jana alikabidhi madaraka kwa Mkurugenzi mpya wa chama hicho, Valerie Msoka.

Amesema chama hicho kitaendelea kutetea haki za wanawake na watoto na kwamba, hakitaogopa kufanya hivyo.

Hafla hiyo fupi iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwamo wanachama wake, ilifanyika katika ofisi za chama hicho zilizopo Sinza Mori, Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo, Nkya alisema chama chake kitaendelea kutetea haki za wanawake na watoto na kwamba hakitaogopa kufanya hivyo.

Nkya alisema, TAMWA ni moja ya chombo cha kuwatetea wanawake wanyonge, watoto na Watanzania kwa ujumla.

“Sisi ni chombo cha kutetea wanyonge, tusiogope kupaza sauti, tukiogopa historia itatushitaki kwa sababu historia ina tabia ya kujirudia, watu wengi wanapenda kupata nafasi kama yetu, lakini hawajaipata, sisi tuliopata hebu tupaze sauti tutetee haki za wangonye,” alisema.

Alisema toka aingie TAMWA miaka 11 iliyopita, kwa kushirikiana na wanachama wa TAMWA wamehakikisha hakuna utaratibu wa kupigana ‘Scoup’ katika habari inayohusu masuala ya jamii.

“Tumehakikisha kila chombo cha habari kinakuwa na habari inayohusu masuala ya jamii ikiwemo ya watoto. Tulihakikisha habari zetu tunazipeleka katika kila chombo. Hili lilikuwa gumu kidogo mwanzoni kueleweka katika vyombo vya habari.

“Kwa sababu walituhoji iweje habari hii mmeipeleka chombo kile halafu mnaileta na hapa, tuliwaelimisha tuhakahikisha katika habari muhimu jambo hili linaondoka kabisa, tunashukuru vyombo vya habari vilituelewa na tumefanya kazi vizuri ya kuelimisha jamii,” alisema Nkya.

Alisema anavishukuru vyombo vya habari, kwani vimeifanya jamii kuelewa umuhimu wa kufuatilia masuala ya habari.

“Nawashukuru sana Watanzania wa sasa kwa sababu wanaamka asubuhi wanafuatilia habari, Watanzania wa leo wanatenda jambo panapotokea masuala ya ukandamizaji.

“Tusiposimama kutetea haki za watoto wetu, hakuna atakayetetea, tuogope kusema mtoto yule aliyebakwa si mtoto wangiu, atakua mwenyewe, tusisubiri hadi abakwe mtoto wako, kila mtu asimame kutetea haki za watoto wa Kitanzania,” alisema.

Akizungumza wakati wa kupokea nyaraka mbalimbali za ofisi, Mkurugenzi mpya, Valerie Msoka alisema, kazi kubwa iliyoko mbele yake ni utekelezaji wa mradi wa miaka miwili wa kujenga usawa wa kijinsia na kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake.

“Mama Nkya amefanya mambo mengi sana ikiwemo TAMWA kuwa na ofisi zake..lakini pia kazi nyingine ni kuhakikisha tunahamasisha wanawake kushiriki kuchangia maoni katika katiba mpya.

“Lakini niseme tu kwamba, mwaka 1987 TAMWA ilipoundwa kulikuwa hakuna wanawake wanaoongoza vyombo vya habari, Mwaka 2012 bado ni wa kuhesabu. Lakini wanaweza kuwa manaibu..hivyo changamoto inabaki kuwa palepale, kuwa wanawake tunaweza kuongoza vyombo vya habari,” alisema Msoka.

 

Nilidhani tu kaondoka Ukurugenzi... lakini hii inaonyesha anaondoka kabaisa TAMWA;

Kaomba kusogea nje ya hicho cho CHAMA... Was it a democracy ???
 
Back
Top Bottom