Ananilea Nkya apata Mrithi TAMWA. Ni Mwandishi wa RTD zamani...

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Sep 7, 2011
3,295
2,500
[h=2]Mabadiliko ya Uongozi TAMWA: Valerie Msoka achuku nafasi ya Ananilea Nkya[/h]


Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimepata Mkurugenzi Mtendaji mpya ambaye anachukua nafasi ya Ananilea Nkya anayemaliza muda wake baada ya kulitumikia shirika hilo kwa miaka kumi na moja.

Mkurugenzi huyo mpya wa TAMWA, Valerie Msoka ambaye ni miongoni mwa wanahabari wanawake 12 walioanzisha TAMWA, amefanya kazi za kutukuka katika ngazi ya kitaifa, kikanda na kimataifa.

Valerie Msoka atakabidhiwa rasmi ofisi Alhamisi tarehe 27 Septemba katika sherehe fupi itakayofanyika kuanzia saa 3.30 hadi ya 5.00 asubuhi.

Sherehe hiyo itakayofanyika katika ofisi za TAMWA zilizoko eneo la Sinza-Mori, Dar es Salaam inatarajiwa kuhudhuriwa na wahariri na wanahabari kutoka vyombo vya habari mbalimbali, wawakilishi wa mashirika ya wanahabari, Wakurugenzi Watendaji kutoka mashirika ya kiraia na viongozi wa TAMWA wa zamani na sasa.

Valerie Msoka alifanya kazi Radio Tanzania Dar es Salaam, shirika la utangazaji la Uingereza BBC idhaa ya Kiswahili na Kiingereza kabla ya kujiunga na Umoja wa Mataifa.

Kadhalika Valerie Msoka mwenye shahada ya Uzamiri katika fani ya Uandishi wa habari wa Kimataifa (M.A in International Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha City nchini Uingereza, amefanya kazi kwenye maeneo ya vita ikiwemo Iraq, Sudan, Rwanda, Congo na Burundi.

Valerie Msoka anachukua uongozi wa TAMWA wakati shirika hili likiwa linajiandaa kuanza kutekeleza mradi mkubwa wenye lengo la kuimarisha vuguvugu katika harakati za kujenga usawa wa kijinsia na kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

TAMWA itatekeleza mradi huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Chama Cha Wanasheria Wanawake nchini (TAWLA), Chama Cha Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) na Kituo cha Usuluhishi (CRC).

Wilaya kumi zitanufaika na mradi huo ambazo ni Wete (Pemba Kaskazini), Unguja Magharibi (Unguja Urban West), Wilaya ya Unguja kusini (Unguja South district), Kisarawe (Pwani), Newala (Mtwara), Mvomero (Morogoro), Lindi vijijini na Ruhangwa (Mtwara), Kinondoni na Ilala, (Dar es Salaam).

Ananilea Nkya
Mkurugenzi Mtendaji



MY TAKE: Tunasubiri kuona kama TAMWA itarejea kuwa msaada kwa wanahabari wanawake ama itaendelea kufanya harakati zaidi na kusahau taaluma ya Habari
 
Afadhali amelazimishwa kujiudhuru alikuwa ni disgrace kwenye fani ya habari. Badala ya kutetea misingi ya taasisi yake akajaribu kupora majukumu ya mama Bisimba
 
Ni mama hodari sana Lucy Nkya, tunakuomba uendelee na harakati zako kama kawaida, ni mmoja wa wanawake jasiri sana ktk nchi yetu.
 
yule mama mpalestina ni jembe kweli kweli...kila la kheri mmachame !
lakini wanasema ingawa simba ni mkali lakini anazaa !
 
Ni mama hodari sana Lucy Nkya, tunakuomba uendelee na harakati zako kama kawaida, ni mmoja wa wanawake jasiri sana ktk nchi yetu.
Come on, Ananilea Nkya na Lucy Nkya ni watu wawili tofauti mkuu. By profession the former ni mwanahabari na the latter ni Doctor wa magonjwa ya wanadamu. The former amestaafu baada ya kumaliza muda wake TAMWA na the latter aliachishwa Unaibu Waziri baada ya kukataliwa na Madaktari.
 
Naye ni mpiganaji kama Ananilea Nkya??
Tupeni taarifa zaidi wenye CV yake.
 
Afadhali amelazimishwa kujiudhuru alikuwa ni disgrace kwenye fani ya habari. Badala ya kutetea misingi ya taasisi yake akajaribu kupora majukumu ya mama Bisimba
Shame on you, I should say more, but your face made me to have a sympathy
 
Alikuwa jasiri, siyo mwoga kamwe, ni mmoja wa wanawake washoka wa nchii hii.
 
yule mama mpalestina ni jembe kweli kweli...kila la kheri mmachame !
lakini wanasema ingawa simba ni mkali lakini anazaa !

Uzazi umeuhusishaje tena na hii habari, Smile yako inaonekana ni ya kinafiki.
 
Last edited by a moderator:
Big up Ananilea Nkya!! Sasa Msoka kazi ya Nkya utaiweza? Mziki wake hadi serikali inakoma ubishi. I like hili jembe la kimachame, ni hodari na mtekelezaji na haogopi mabomu. SSM watakuwa wanashehereka sasa. Ila naomba aendelee kubaki TAMWA na awe front tu katika kupambana na utesaji wa nchi hii kwa raia na kwa wale akina mama wanaoteswa na watoto wa kike pia.
 
Huyu mpya alishawahi kuajiriwa radio tanzania?hapo ndipo tatizo linapoanzia sababu radio tanzania sasa hivi inaitwa tbccm taifa..
 
Back
Top Bottom