Analysis: End of Gadaffi, Reasons for Fear Kikwete, Mugabe, Museveni...

Tanzania hatuhitaji NATO. Subiri utaona.
Jasusi,i will take your word my friend.BTW Obama kawaambia wapatane.Yani wawunde kamati ya truth and reconciliation kama ile ya South Afrika.Unadhani ni kwanini kama situation ni sawa na za huko Egypt etc?
 
US na Nato ndio wanaiendesha hii dunia kwa maslahi yao.
Hivi vita vya Libya uwezi kusema nguvu ya umma imemtoa Gaddafi, walioangusha utawala wa Gaddafi ni US na Nato waasi wapo kama vibaraka tu. Wamepewa kila aina za silaha na US na Nato, tumeona juzi walipokutana Waziri Mkuu wa Ujerumani Angela Merkel, na Waziri Mkuu wa Ufaransa Nicolas Sarkozy, jinsi ya kugawana matunda ya vita vya Libya.
Sarkozy anamwambia wazi Angela Merkel, nchi yako mbona imetoa mchango mdogo kwenye vita vya Libya, tusikae tukategemea hata kidogo eti siku moja US na Nato watawasaidia Watanzania, tizama Zimbabwe mpaka leo kweli Nato na US wanashindwa kumsaidia Morgan Tsvangirai kuungusha utawala wa Mugabe au Zimbambwe hakuna mafuta.
Sasa hivi kuna mauaji makubwa yanaendelea nchini Syria, US na Nato wamefanyaje zaidi ya kumwambia rais Syria Bashar al-Assad, kuheshimu haki za binadamu wanashindwa kuungasha utawala wake kwa sababu wana maslahi nae
.

Kuondoka kwa Qadaffi, lazima kuwe fundisho hata kwa JK wetu, pamoja sio siri mie ni mshabiki wa CCM, lakini yanaofanyika hapa nchini hatakama unaipenda CCM lazima tu itakufikia kooni na kusema basi, anaetutawala hawezi kazi, hawezi kufanya maamuzi magumu wala kutokutaka lawama, ili mradi eti akiondoka madarakani asiwe na adui! Lakini JK lazima akumbuke, yuko palekwa ajili yetu sie walalahoi, hayuko pale kumlinda Lowassa, Chenge, Mramba, Yona, Mkapa na Mkewe (kama walifanya madudu), hata Riz1 mtoto kama anajihusisha na ufisadi. Hakuna kisichowezekana hapa duniani, linaweza likaanza tu wimbi hapa Tanzania, ukashangaa walalahoi wakachukia nchi, huyo Mugabe, M7 na wengineo siku zao zipo, lazima tu wataondoka, JK hayuko sawa na hawa ila ni muoga mno kutumia madaraka yake kwa kisingizio cha kuogopa kuchukiwa na kuwa na maadui.
Leo hii hatuna maji, umeme, huduma za afya mbovu, miundo mbinu bomu, huduma za jamii ni kama hakuna, rushwa na wizi kwenye wizara na mashirika ya umma umekithiri, maliasili zetu zinapondwa na wachache bila ya wahusika ambao ni walalahoi kuwa kufaidika.
Halafu unataka tukae kimya na kusema, tuna amani?!
Hakuna hiko, tumechoka, na kwa sasa walalahoi wanajali zaidi sera kuliko chama,
 
Huyu bwana kama akikamatwa inabidi aje kwanza bongo na kumaliza ujenzi wa zile nyumba za waathirika wa mafuriko ya Kilosa, hatujasahau.JK,I thought Ghadafi was your friend, mbona mko kimya sana??
 
Obama kasema inabidi waunde tume a truth and reconciliation.Kwahiyo wale mliotaka kumwona Colonel kwenye kitanzi mmeliwa kubwa.Gaddafi si Saddam,mnafikiri kwa makamasi.Viva Afrika.
Wazalendo wa kweli wana kazi.Kuna mtu kaharibu akili za kizazi hiki.Mawazo ya kitumwa.Afrika tuna kazi kubwa mnoo!
 
Ha ha ha!Za CDM huwa huzioni kamanda?Mikutano na maandamano ya CDM ni zaidi ya hayo.Tatizo bongo hakuna NATO.Reason why?Hali halisi speaks for it self!

Mkuu jmushi1, hebu kwanza jiulize hii ni kwa sababu gani maandamano mpaka sasa unayaita ya CDM. Je,

  • Ni wana Chadema pekee ndio wanateseka umeme unapokosekana ?
  • Ni wana Chadema peke yao ndio wanaokufa mahospitalini dawa inapokosekana ?
  • Ni wana Chadema pekee wanapata taabu maji yanapokuwa shida ?
  • Ni wana Chadema ndio wanapata uchungu rasilimali za taifa zinapotapanywa ?
  • Ni wana Chadema tu wanalalamika jinsi mafisadi wanavyoota kama uyoga ?
  • Ni wana Chadema peke yao ndio wanaumia bei za vyakula zikipanda ?
  • Ni watoto wa wana Chadema tu ndio wanafeli kwa kukosa elimu bora ?
  • Ni wake wa wana Chadema tu ndio hawapati huduma nzuri wanapojifungua ?
Mkuu jmushi1, ningeweza kuendeleza hii listi mpaka page nzima ikajaa lakini nina hakika kwamba ni asilimia kubwa tu ya watanzania wanaoonja ladha ya maisha yanavyozidi kuwa magumu. Yawezekana maandamano bado hayajafanikiwa kwa sababu bado watu wanaamini kama unavyoonekana unaamini kuwa maandamano ni ya wanaChadema na si ya Watazania. Bila shaka watu kama Kikwete wakisoma mwelekeo wa hii thread wanapata faraja kuwa kuna Watanzania wanaobeza malalamiko dhidi ya serikali wakiyaita ya Chadema.

Lakini naomba nikuhakikishie kwamba Watanzania wanaamka, thanks to Chadema, na viti walivyovikalia Kikwete na genge lake vinaanza kupata joto na muda si mrefu wataanza kukosa raha. Nakumbuka upepo wa mageuzi ulipoanza, wengi wa Watanzania kama wewe hawakuamini kuwa mabadiliko yangewezekana lakini ndio yalifanikiwa kwa kiwango fulani ingawa si cha kuridhisha kwa wakati huo. Hivi sasa hata mwaka bado tangia uchaguzi wa 2010 lakini nakuhakikishia kwa mambo yanavyokwenda kuna hatari ya chombo kwenda mrama.

Libya kidogo hali ni tofauti kwani Gadafi aliingia madarakani kwa upanga na ni halali yake kuondolewa kwa upanga, hivyo ndivyo ilivyo historia, inasimama imara kumhukumu. Hapa kwetu hali ni tofauti kidogo kwani Kikwete ingawa aliingia madarakani kiutaratibu lakini haikuwa kihalali na yawezekana kutolewa kusiwe kiutaratibu bali itakuwa kihalali. Usishangae watu walioishi kama wafungwa jijini Tripoii leo hii wanajitokeza hadi mtoto wa miaka 19 ambaye kazaliwa Gadafi akiwa madarakani anamlaani kwa kuendesha utawala wa kimabavu.

Mkuu jmushi1, siku Watanzania, hasa wenye mawazo kama yako, watakapoyaunga mkono maandamano ya Chadema na kuyakubali kama yao wote waliochoka na utawala wa kinafiki, CCM itang'oka. Nakuhakikishia tena siku hiyo utashuhudia nguo za kijani zikivuliwa na kutupwa jalalani na watu hao hao ambao hukesha wakiimba CCM nambari wani na kuingia mitaani bila upinzani. Wengine tulikuwa na bahati ya kuishuhudia Romania siku wananchi walipoamua, maafande walilazimika kutupa silaha chini na kuungana na wanaRomania.
 
<br />
<br />

Umesahau na the lockerbie bombing nadhani hii pia ni fursa ya wazungu kulipa kisasi kwa kadafi.

Yes.. Lockerbie! na lini sisi Waafrika tutalipiza kisasi kwa Wazungu waliokuja kuuwa watu wetu wakati walipokuja kututawala? Unafurahia Wazungu kulipiza kisasi, kwa nini hutaji kwamba nasi tulipaswa kulipiza kisasi kwao?
 
Mkuu jmushi1, hebu kwanza jiulize hii ni kwa sababu gani maandamano mpaka sasa unayaita ya CDM. Je,
  • Ni wana Chadema pekee ndio wanateseka umeme unapokosekana ?
  • Ni wana Chadema peke yao ndio wanaokufa mahospitalini dawa inapokosekana ?
  • Ni wana Chadema pekee wanapata taabu maji yanapokuwa shida ?
  • Ni wana Chadema ndio wanapata uchungu rasilimali za taifa zinapotapanywa ?
  • Ni wana Chadema tu wanalalamika jinsi mafisadi wanavyoota kama uyoga ?
  • Ni wana Chadema peke yao ndio wanaumia bei za vyakula zikipanda ?
  • Ni watoto wa wana Chadema tu ndio wanafeli kwa kukosa elimu bora ?
  • Ni wake wa wana Chadema tu ndio hawapati huduma nzuri wanapojifungua ?
Mkuu jmushi1, ningeweza kuendeleza hii listi mpaka page nzima ikajaa lakini nina hakika kwamba ni asilimia kubwa tu ya watanzania wanaoonja ladha ya maisha yanavyozidi kuwa magumu. Yawezekana maandamano bado hayajafanikiwa kwa sababu bado watu wanaamini kama unavyoonekana unaamini kuwa maandamano ni ya wanaChadema na si ya Watazania. Bila shaka watu kama Kikwete wakisoma mwelekeo wa hii thread wanapata faraja kuwa kuna Watanzania wanaobeza malalamiko dhidi ya serikali wakiyaita ya Chadema.

Lakini naomba nikuhakikishie kwamba Watanzania wanaamka, thanks to Chadema, na viti walivyovikalia Kikwete na genge lake vinaanza kupata joto na muda si mrefu wataanza kukosa raha. Nakumbuka upepo wa mageuzi ulipoanza, wengi wa Watanzania kama wewe hawakuamini kuwa mabadiliko yangewezekana lakini ndio yalifanikiwa kwa kiwango fulani ingawa si cha kuridhisha kwa wakati huo. Hivi sasa hata mwaka bado tangia uchaguzi wa 2010 lakini nakuhakikishia kwa mambo yanavyokwenda kuna hatari ya chombo kwenda mrama.

Libya kidogo hali ni tofauti kwani Gadafi aliingia madarakani kwa upanga na ni halali yake kuondolewa kwa upanga, hivyo ndivyo ilivyo historia, inasimama imara kumhukumu. Hapa kwetu hali ni tofauti kidogo kwani Kikwete ingawa aliingia madarakani kiutaratibu lakini haikuwa kihalali na yawezekana kutolewa kusiwe kiutaratibu bali itakuwa kihalali. Usishangae watu walioishi kama wafungwa jijini Tripoii leo hii wanajitokeza hadi mtoto wa miaka 19 ambaye kazaliwa Gadafi akiwa madarakani anamlaani kwa kuendesha utawala wa kimabavu.

Mkuu jmushi1, siku Watanzania, hasa wenye mawazo kama yako, watakapoyaunga mkono maandamano ya Chadema na kuyakubali kama yao wote waliochoka na utawala wa kinafiki, CCM itang'oka. Nakuhakikishia tena siku hiyo utashuhudia nguo za kijani zikivuliwa na kutupwa jalalani na watu hao hao ambao hukesha wakiimba CCM nambari wani na kuingia mitaani bila upinzani. Wengine tulikuwa na bahati ya kuishuhudia Romania siku wananchi walipoamua, maafande walilazimika kutupa silaha chini na kuungana na wanaRomania.
Ok mkuu wangu.You are one of the great thinkers humu ndani,no doubt.Nakuaminia all the way na michango yako huwa naipitia.However hata kama sikubalini na wewe kwenye hili,sitothubutu kusema unatumia masaburi kufikiri kwasababu natambua you are wise,we just have different perceptions hapa.

Sasa swali langu ni kwamba,mbona bado ccm wako madarakani licha ya umma wote huo?

Ndiyo maana nikatumia picha yako uliyopiposti kusema kuwa si lazima wananchi wote wa Libya wawe hawampendi Gaddafi ama wanataka vita simply kwa kuangalia hizo picha.Kwa maana kwamba umma wa CDM unaowakusanya hawaipendi ccm lakini bado wako madarakani tu.Tuwaombe NATO?

However tuko pamoja.Lets hope Libya wil go back to where it was.
 
Ndugu zangu watanzania kwanza namshukuru mola kwa jinsi anavyozidi kuoyesha mwangaza wake siku hadi siku
niliwahi kuleta mada ya gadafi haapa miaka ya nyuma alipokuwa uganda akatukana sana sana wakristo
mwaka huu kabla ya kuanza kucxhapwa na nato nilimsikia td joshua akisema kuna kiongozi mkubwa wa waarabu ataangushwa bada ya w misri wengine tulimlilia sana sana mungu awe gaaddafi kwa hili alipoanza kuchapwa hakika tulisema akifika mwezi wa tisa anaongoza basi lazima tumuulize mungu alichokisema uganda juu ya wakristo ni sawa??
Unajua ukisali sio unasali mwambie mungu na reference..unataka fedha lazima ueleze uzifanyie nini??unaomba mke uwe na familia lazima umweleze makusudi ya kuwa na mke sio ilimradi umevaa suti ya kichina unatoka pale hata kuleta mkate unaokula mwenyewe asbh unashindwaa hizoz ni laana na ndicho tulichosimama na mungu amuonyeshe gadafi alichokisema ni laana kwake na familia hivinaandika nafurahi kusikia mtoto wa tatu wa gadafi amekamatwa na bado wapwa wake wote watapelekwe kunako wamjue mungu wa kweli
 
Nakubaliana na wewe kuwa mabadiliko yalitakiwa lakini si kwa shinikizo la NATO. Syria wamesema hawataki marekani . Haukuwa muda muafaka wa kumtoa kwa kufuata wave ya Misri na Tunis. Aisee usiwe na hasira na ukiritimba uliopo madarakani wa viongozi wa Africa, huu unakuwa supported na western iwapo wana maslahi yao. Inabidi tujue jinsi ya kutatua matatizo yetu si kutatuliwa. Hivi bushi alipataje uraisi wakati baba yake alikuwa raisi. Unajua familia ya bush wote ni matajiri kutokana na kuwepo seriakalini. nani alisema ni utawala wa kifamilia. Hawa jamaa wameuacha mbali itachukua miaka mia mbili kuwa na kufikiri kama wao.
<br />
<br />

Mkuu partly nakubaliana nawe na partly napingana nawe. Wakati nakubaliana nawe kuwa ni kweli mabadiliko bora ni lazima yaanzie ndani lakini pia tukiri kuwa nyakati nyingine circumstances hazifanani daima, dynamics na interplay za factors kadha wa kadha katika libya ndo zimesababisha hao Nato kuwa part and parcel ya kilichotokea. Kuna mchangiaji mmoja kaorodhesha baadhi ya factors hizo, lakini pia discontent za walibya (hata kama tunawaita wabenghaz) na mfumo wa kiutawala aliouasisi kadafi pia zimeplay role kubwa ya kinachotokea leo.
 
Obama kasema inabidi waunde tume a truth and reconciliation.Kwahiyo wale mliotaka kumwona Colonel kwenye kitanzi mmeliwa kubwa.Gaddafi si Saddam,mnafikiri kwa makamasi.Viva Afrika.
Wazalendo wa kweli wana kazi.Kuna mtu kaharibu akili za kizazi hiki.Mawazo ya kitumwa.Afrika tuna kazi kubwa mnoo!
I think you didn't understand well Obama a truth and reconciliation does not mean Gaddafi will not face a trial.
 
Ni mpuuzi tu atakayelinganisha hali ya Libya na kuifananisha na hapa kwetu. Libya kumekuwa hakuna uhuru wa habari, hakuna uhuru wa demokrasia, utawala wa ukandamizaji na visasi pamoja na tawala za kikabila. Hali kama hiyo haipo kabisa Tanzania, badala yake serikali imejitahidi kuweka uhuru wa habari, kupanua wigo wa demokrasia na uhuru wa kutoa maoni. Sasa mtu atapata wapi sababu ya kumtoa Rais madarakani?
 
Do you think Tanzanians are looking for only uhuru wa habari? pole.
 
Ni mpuuzi tu atakayelinganisha hali ya Libya na kuifananisha na hapa kwetu. Libya kumekuwa hakuna uhuru wa habari, hakuna uhuru wa demokrasia, utawala wa ukandamizaji na visasi pamoja na tawala za kikabila. Hali kama hiyo haipo kabisa Tanzania, badala yake serikali imejitahidi kuweka uhuru wa habari, kupanua wigo wa demokrasia na uhuru wa kutoa maoni. Sasa mtu atapata wapi sababu ya kumtoa Rais madarakani?
eti ..wakati kila mtu ana maisha bora eehn? kama ningekuwa na uwezo ningekupa mbwa wangu hapa ayafanyie kazi masaburi yako maana una kihehere cha kuwashwa!
 
Yes.. Lockerbie! na lini sisi Waafrika tutalipiza kisasi kwa Wazungu waliokuja kuuwa watu wetu wakati walipokuja kututawala? Unafurahia Wazungu kulipiza kisasi, kwa nini hutaji kwamba nasi tulipaswa kulipiza kisasi kwao?[/SIZE]
<br />
<br />

Mkuu nakubaliana nawe hili kama litawezekana itakuwa nzuri zaidi. Lakini pia revenge yetu haitakua kwa wazungu tu sababu ya colonialism bali hata kwa waarabu bado tunakumbuka ishu za slavery walizotufanyia waarabu hawa. So ukifika wakati mwafaka revenge yetu iende katika both directions
 
Back
Top Bottom